T 1990 ELY
JF-Expert Member
- Sep 7, 2014
- 12,674
- 29,643
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haya bn totoDuuh sikuona hii comment, niko na kilo chache lakini nina mwili mzuri 😂😂
😁😁😁Sijisumbui kwenda gym sababu umbo ni namba 9 hili halina gym mazoezi yanadunda
Basi uwe unaamka kumsaidia mama shughuli za asubuhi kabla ya kwenda kazini.Hapana mkuu, mimi sio mvivu
Labda 22 hivi.Ulikua unahisi na miaka mingap Eroni?
Kuogopa nikukata tamaa, uwoga ni hofu na hofu sio mpango wa Mungu ni washetani, tumbo likishaingia hofu mwili wote unakataa kuamini unaweza, akishindwa mmoja sio kwamba kila mmoja atashindwa na sababu ni nyingi kupelekea watu kukata tamaa au kushindwa.My dear ogopaaa
Ujue nimewaza nikasema over my black dead body!Hongera Kwa mama yako maana Mimi siwezi kuwa kama yeye hata robo,yaani mwanangu mkubwa wa kujitegemea alale aamke nimeshampikia chai,nguo zake nimemfulia,anachelewa kurudi pengine Hana sababu ya msingi Mimi nimsubirie nihakikisha amekula,bado usiku nikachungulie kama kashusha neti!! Yaani anawajibika Kwa mtoto wa 18+kama anahudumia wasiojiweza? Hivi haya ya kweli au unatania?
Wewe ni mchaga wa wapi?Sijisumbui kwenda gym sababu umbo ni namba 9, hili halina gym mazoezi yanadunda
Mhaya wa Muleba, mngoni wa Manda, Mzaramo wa Bagamoyo, Muha wa Ziwa TanganyikaWewe ni mchaga wa wapi?
Mhaya wa Muleba, mngoni wa Manda, Mzaramo wa Bagamoyo, Muha wa Ziwa Tanganyika
Hii shepu yangu hata ya wachaga haipoIlikuwaje ukawa na shepu la kichaga ilhali we sio mchaga?
Ni ya peke yangu🤸
I say usijidanganye, wamama wanaumwa sana wakiwa wazee, hasa wakishafikia kwenye mid fifties maumivu huwa hayaishi.Hao ndio wale wamama ambao kamwe hutasikia ana maumivu ya mgongo au miguu sijui inamuuma atazeeka na nguvU zake. Watoto wake watajua umuhimu wake siku wakibaki wenyewe. Na kila mmoja wao atasema hakika YULE ALIKUWA MTU NA NUSU
🤣🤣🤣akapange muende kulala siompaka leo unafanya nini nyumbani leejay, nenda kapange tuje tulale, utakuwa mama vere suni
Mbna Kama mama angu huyo kbsa mama hat ng'ombe apige tekea ukuta saa nane za usku lzma aamke bas ahata ukinyata kwenda kukojoaa utasikia anauliziaa wee Nani , Basi hat ukitaka kisafiri saa kumi na moja yey atamka kabla yakoNatumai wazima wote,.
Iko hivi, kila siku zinavyoenda ndivyo ambavyo naogopa kuja kuitwa mama hapo baadae (Mungu anisaidie niondokane na hii hofu😓🥹🙏), hiii inatokana na lifestyle ambayo namwona mama yangu anaishi.
Huyu mwanamke sielewi huwa anapumzika mda gani, yeye ndie mtu wa mwisho kulala kila siku. Yaani hawezi kulala kama kuna mtu bado hajaingia nyumbani, na anahakikisha kila mtu amekula amelala anafunga milango ndipo na yeye alale. Na hata akiingia kulala halitapita nusu saa anapita tena vyumba vyote kuhakikisha mmefunga madirisha, mmeshusha neti na mmejifunika vizuri (anaweza akaamka hata mara 4 kwa usiku mmoja).
Haitaishia hapo, bado kuna sisi ambao inabidi asubuhi tuende kazini na wengine shuleni, wanaoamka usiku kusoma na wanaoamka kusali, kila mtu anamtajia mda wake wa kumwamsha hajawahi kukataa wala kupitiliza kutuamsha, always anakua on time.
Sijawahi kushuhudia ni saa ngapi ameamka ila kila tukiamka asubuhi tayari tunamkuta akiwa macho, kashafanya usafi na kashapika chai tunakunywa tunamwacha Nyumbani. Hatujawahi kuona au kushuhudia akilala mchana, Labda itokee anaumwa (napo ni mara chache sana ). Sijui hua anapumzika mda gani
Hajawahi kuishi na msaidizi wa kazi maisha yake yote, lakini hakuna aliyewahi kufua, kudeki, kupika, kuosha vyombo wala kufagia. Sio kwamba hatutaki kumsaidia Hapana, ni kwamba hatujawahi kuona uwanja ukiwa mchafu, vyombo vichafu na mda wowote ukirudi nyumbani unakuta chakula tayari na usafi wote ushafanywa na nguo zote ziko kambani zinakauka.
Licha ya hayo yote vilevile bado hajawahi kuacha kwenda kazini na shughuli zake nyingine zote za ujasiriamali hajawahi kuacha kufanya, hajawahi kuacha kwenda kwenye jumuiya wala kanisani hata jumapili moja, na kwenye dharura zote iwe hospitali au kikao chochote atakachohitajika mzazi awepo basi ni yeye ndio atakuwepo tena kwa wakati. Na sijawahi kumwona akilalamika, akinung’unika wala akimlaumu mtu kwamba hakuna anayemsaidia kazi hata siku moja.
Haya maisha yake yananiogopesha na yananifanya niogope hata kuwaza jinsi nitakavyoishi na watoto wangu huko mbeleni. Sometimes i wish ningekua wakiume labda ningeishi tu kama baba yangu anavyoishi😓😓😓 (Em assume mtu anafanya haya maisha yake yote)