Naogopa kuwa mama

Naogopa kuwa mama

Watoto wa shangazi yangu waliishi maisha kama hayo uliyoelezea hapa. Siku haina jina wala taarifa mama yao (shangazi) aliugua ghafla akakimbizwa hospital kufika madaktari wakasema hamjaleta mgonjwa bali mmeleta mwili wa marehemu.

Hakuna rangi waliacha kuona wale binamu zangu kwa namna marehemu mama yao alivyokuwa kawadekeza aseeeeee, wanaishi maisha magumu mno!! Hao wakike wamezalishwa bila utaratibu, ni wavivu hakuna mtu anawakubali kuishi nao. Mmoja kaolewa ndoa tatu na zote zimemshinda sababu ya uvivu anaishia kuachika.

Maisha ni maamuzi yako ingawa malezi na makuzi ni muhimu sana hasa unapoanza maisha ya kujitegemea.
Ooh jamani🥺🥺
 
Mb
Mbna Kama mama angu huyo kbsa mama hat ng'ombe apige tekea ukuta saa nane za usku lzma aamke bas ahata ukinyata kwenda kukojoaa utasikia anauliziaa wee Nani , Basi hat ukitaka kisafiri saa kumi na moja yey atamka kabla yako
Sijui hua wanalalaga saa ngapi yani
 
Ulivyosimulia kama Mama yangu, tofauti Mazingira yetu ni shamba/kijijini.

Mama zetu walifundishwa kufanya kazi haswa kama mama wa familia.


Hata ufanyaje huwezi kuwa kama mama yako. Huna haja ya kuogopa.
Wamama wa aina hiyo ndio wanaishia.

Sasa mambo yamebadilika.
Kazi nyingi ambazo zilifanywa na Mama wa familia zinafanywa na wadada wa kazi.
Hua tu nawaza anapumzika mda gani, isije ikatakiwa na mimi niwe hivyo uwiii😬😬
 
Kama hiki ulichokieleza hapa ni ukweli basi Kwakweli ww atakaekuja kukuoa atapata tabu sana yaani atakua na bahati mbaya labda ubadilike huko mbeleni kitu ambacho kwasasa ni kigumu.
Hapana hatapata tabu, kwasababu mimi sio mvivu🥺🥺
 
Hongera Kwa mama yako maana Mimi siwezi kuwa kama yeye hata robo,yaani mwanangu mkubwa wa kujitegemea alale aamke nimeshampikia chai,nguo zake nimemfulia,anachelewa kurudi pengine Hana sababu ya msingi Mimi nimsubirie nihakikisha amekula,bado usiku nikachungulie kama kashusha neti!! Yaani anawajibika Kwa mtoto wa 18+kama anahudumia wasiojiweza? Hivi haya ya kweli au unatania?
Ni kwamba anajali kupitiliza na hapendi kusaidiwa kazi,,. She is a good woman at all
But naogopa maana nahisi sitaweza kuwa kama yeye🥺
 
Huwezi kuwa kama mama yako ila anayoyafanya yawe funzo kwako.

Huenda mama yako hataki wasaidizi wa kazi kwa maana ya kutaka kuwafundisha mwenyewe nafasi ya mwanamke kwenye familia kwa vitendo.

Nimependa ulivyosema huwezi kuishi mwenyewe(unaogopa), changa karata zako vizuri hata ikitokea ukapata mwenza basi awe mwenye kuendana na wewe maana inaoekana unadeka sana pia.

Muhimu: Tengeneza mazingira ya kumsaidia majukumu wewe pamoja na hao ndugu zako ili nae apate kupumzika.
Asante kwa ushauri mzuri rafiki, ubarikiwe sana
 
Hujawahi kufua wala kupika wala kufagia uwanja wala kuosha vyombo wala kudeki.

Mmemgeuza mama yenu punda? Kumsaidia kazi mnasubiri hadi awaambie?

Mitoto ya hovyo na mivivu! 😎

-Kaveli-
Sio kweli bhana, sisi sio wavivu,
Mama hapendi kusaidiwa, unaweza ukajioshesha vyombo na akaja kurudia vyote, au unaweza ufue akaja kurudia tena
So naogopa maana kuwa kama yeye najiona kabisa sitaweza
 
Natumai wazima wote,.

Iko hivi, kila siku zinavyoenda ndivyo ambavyo naogopa kuja kuitwa mama hapo baadae (Mungu anisaidie niondokane na hii hofu😓🥹🙏), hiii inatokana na lifestyle ambayo namwona mama yangu anaishi.

Huyu mwanamke sielewi huwa anapumzika mda gani, yeye ndie mtu wa mwisho kulala kila siku. Yaani hawezi kulala kama kuna mtu bado hajaingia nyumbani, na anahakikisha kila mtu amekula amelala anafunga milango ndipo na yeye alale. Na hata akiingia kulala halitapita nusu saa anapita tena vyumba vyote kuhakikisha mmefunga madirisha, mmeshusha neti na mmejifunika vizuri (anaweza akaamka hata mara 4 kwa usiku mmoja).

Haitaishia hapo, bado kuna sisi ambao inabidi asubuhi tuende kazini na wengine shuleni, wanaoamka usiku kusoma na wanaoamka kusali, kila mtu anamtajia mda wake wa kumwamsha hajawahi kukataa wala kupitiliza kutuamsha, always anakua on time.

Sijawahi kushuhudia ni saa ngapi ameamka ila kila tukiamka asubuhi tayari tunamkuta akiwa macho, kashafanya usafi na kashapika chai tunakunywa tunamwacha Nyumbani. Hatujawahi kuona au kushuhudia akilala mchana, Labda itokee anaumwa (napo ni mara chache sana ). Sijui hua anapumzika mda gani

Hajawahi kuishi na msaidizi wa kazi maisha yake yote, lakini hakuna aliyewahi kufua, kudeki, kupika, kuosha vyombo wala kufagia. Sio kwamba hatutaki kumsaidia Hapana, ni kwamba hatujawahi kuona uwanja ukiwa mchafu, vyombo vichafu na mda wowote ukirudi nyumbani unakuta chakula tayari na usafi wote ushafanywa na nguo zote ziko kambani zinakauka.

Licha ya hayo yote vilevile bado hajawahi kuacha kwenda kazini na shughuli zake nyingine zote za ujasiriamali hajawahi kuacha kufanya, hajawahi kuacha kwenda kwenye jumuiya wala kanisani hata jumapili moja, na kwenye dharura zote iwe hospitali au kikao chochote atakachohitajika mzazi awepo basi ni yeye ndio atakuwepo tena kwa wakati. Na sijawahi kumwona akilalamika, akinung’unika wala akimlaumu mtu kwamba hakuna anayemsaidia kazi hata siku moja.

Haya maisha yake yananiogopesha na yananifanya niogope hata kuwaza jinsi nitakavyoishi na watoto wangu huko mbeleni. Sometimes i wish ningekua wakiume labda ningeishi tu kama baba yangu anavyoishi😓😓😓 (Em assume mtu anafanya haya maisha yake yote)
We sio wife material
 
Sio kweli bhana, sisi sio wavivu,
Mama hapendi kusaidiwa, unaweza ukajioshesha vyombo na akaja kurudia vyote, au unaweza ufue akaja kurudia tena
So naogopa maana kuwa kama yeye najiona kabisa sitaweza

ok.

-Kaveli-
 
Back
Top Bottom