Lumbi9
JF-Expert Member
- Oct 12, 2014
- 8,666
- 12,178
Ndio ndio🤣🤣🤣akapange muende kulala sio
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio ndio🤣🤣🤣akapange muende kulala sio
Wana cha kujifunza basi hawa watoto, makucha mareeefu wakirud hime kuperuz internet tu. Hakuna wanacho learnNaona vile mama anawafunzeni Ukakamavu na kujiamani zaidi. Mama bora hujali familia yake.
Duuh 🥺🥺, mimi sio mvivu mkuu unanielewa vibayaNimeshangaa sana aisee.
Naona hii itakuwa kwenu tu. Sababu kikawaida watoto wa kike ndio hufunzwa na kumsaidia mama yao tangu wadogo. Na wakiwa wengi hupangiwa zamu. Mama huwa anaamua afanye kazi au aache unless kama watoto hawapo nyumbani. Ila mama anakuwa kama bosi na kazi yake ni kusimamia tu.
Kwa mwandiko naweza kusema wewe utakuwa kati ya 20 mpaka 27, not more than that, kama ni zaidi ya hapo basi itakuwa ajabu zaidi. Sababu utakuwa na akili za kitoto kupitiliza. Na bila shaka mama yenu atakuwa amewadekeza kupitiliza, that's why hamuwezi hata kuona aibu na kumuomba kumsaidia. Na that's why umepata ujasiri wa kuja kuandika humu bila kujua ni kitu cha ajabu na cha aibu kilichokosa utu. Watoto wa Kishua probably, out of touch with reality.
Na kwa hayo malezi aliyowalewa mtakuja kupata tabu sana soon enough, hasa ndoani. Hakuna mwanaume atakayekubali kuona nyumba na familia vipo hovyo sababu mke anaenda kazini.
Ee Mungu wangu🥺.. Sisi sio wavivu mkuuHao ndio wanawake sasa, sio nyie makolokolo,takataka kabisa vibint vya siku hiz.
Halaf kufanya kaz wao wana enjoy hawana kwere, ila mnajipendekeza kuwaonea huruma kwa jinsi mlivyojaa uvivu hasidi wakubwa nyie
Sasa unaogopa nini hapo mkuu?Ee Mungu wangu🥺.. Sisi sio wavivu mkuu
Msaidie kufanya kazi hata kama hapendiKila siku naamka sa12 na nusu, nakuta kila kitu kashafanya . Na hata kama bado huwa hapendi kusaidiwa
Kinachofanya msimsaidie mama ni nini mkuuEe Mungu wangu🥺.. Sisi sio wavivu mkuu
NimenukuuNatumai wazima wote,.
Iko hivi, kila siku zinavyoenda ndivyo ambavyo naogopa kuja kuitwa mama hapo baadae (Mungu anisaidie niondokane na hii hofu😓🥹🙏), hiii inatokana na lifestyle ambayo namwona mama yangu anaishi.
Huyu mwanamke sielewi huwa anapumzika mda gani, yeye ndie mtu wa mwisho kulala kila siku. Yaani hawezi kulala kama kuna mtu bado hajaingia nyumbani, na anahakikisha kila mtu amekula amelala anafunga milango ndipo na yeye alale. Na hata akiingia kulala halitapita nusu saa anapita tena vyumba vyote kuhakikisha mmefunga madirisha, mmeshusha neti na mmejifunika vizuri (anaweza akaamka hata mara 4 kwa usiku mmoja).
Haitaishia hapo, bado kuna sisi ambao inabidi asubuhi tuende kazini na wengine shuleni, wanaoamka usiku kusoma na wanaoamka kusali, kila mtu anamtajia mda wake wa kumwamsha hajawahi kukataa wala kupitiliza kutuamsha, always anakua on time.
Sijawahi kushuhudia ni saa ngapi ameamka ila kila tukiamka asubuhi tayari tunamkuta akiwa macho, kashafanya usafi na kashapika chai tunakunywa tunamwacha Nyumbani. Hatujawahi kuona au kushuhudia akilala mchana, Labda itokee anaumwa (napo ni mara chache sana ). Sijui hua anapumzika mda gani
Hajawahi kuishi na msaidizi wa kazi maisha yake yote, lakini hakuna aliyewahi kufua, kudeki, kupika, kuosha vyombo wala kufagia. Sio kwamba hatutaki kumsaidia Hapana, ni kwamba hatujawahi kuona uwanja ukiwa mchafu, vyombo vichafu na mda wowote ukirudi nyumbani unakuta chakula tayari na usafi wote ushafanywa na nguo zote ziko kambani zinakauka.
Licha ya hayo yote vilevile bado hajawahi kuacha kwenda kazini na shughuli zake nyingine zote za ujasiriamali hajawahi kuacha kufanya, hajawahi kuacha kwenda kwenye jumuiya wala kanisani hata jumapili moja, na kwenye dharura zote iwe hospitali au kikao chochote atakachohitajika mzazi awepo basi ni yeye ndio atakuwepo tena kwa wakati. Na sijawahi kumwona akilalamika, akinung’unika wala akimlaumu mtu kwamba hakuna anayemsaidia kazi hata siku moja.
Haya maisha yake yananiogopesha na yananifanya niogope hata kuwaza jinsi nitakavyoishi na watoto wangu huko mbeleni. Sometimes i wish ningekua wakiume labda ningeishi tu kama baba yangu anavyoishi😓😓😓 (Em assume mtu anafanya haya maisha yake yote)
She is a good woman ever,.Nimenukuu
"""Hajawahi kuishi na msaidizi wa kazi maisha yake yote, lakini hakuna aliyewahi kufua, kudeki, kupika, kuosha vyombo wala kufagia. Sio kwamba hatutaki kumsaidia Hapana, ni kwamba hatujawahi kuona uwanja ukiwa mchafu, vyombo vichafu na mda wowote ukirudi nyumbani unakuta chakula tayari na usafi wote ushafanywa na nguo zote ziko kambani zinakauka"""
Mama angu Ni MTU wa kipekee Sana vyotee ulivyo elezea umemuelezea yeye MTUPU
Inabidi u sucrifice your dreams to others you love (sons & daughters)She is a good woman ever,.
But naogopa sidhani kama nitaweza kuwa kama yeye, for real 🥺🥺