Naomba anaejua anifundishe jinsi ya kuanza kuhubiri neno la Mungu

Naomba anaejua anifundishe jinsi ya kuanza kuhubiri neno la Mungu

Nenda kasomee kama sio kipawa ulchozaliwa nacho
 
Je ndani yako unahisi unapenda kufundisha na kuhubiri neno la MUNGU ?

Jibu likiwa ndio fanya hivi

Soma biblia na uanze kufanya tafakuri kwa kuandika mahali fulani mfano waweza kusoma zaburi na kupitia hiyo zaburi ukachukua mstari unaosema bwana ndie Mchungaji Wang u. zaburi 23.

Mstari huu unaweza kuutumia kuhubiri kwa watu waliokata tamaa na Maisha ili wajue umuhimu wa kuanza na Mungu na kumkabidhi Mungu Masha yao.


Pili Kama lugha ya kiingereza imekaa vizuri anza kusoma vitabu vya mchungaji anaitwa Joel osteen Kama become better you . n.k. utapata revelation (mafunuo) mengi yakuwapa WATU.

Tatu
Hii ni ukumbusho kuwa na maarifa ya kuhubiri na kuwa. Anointed
(kupakwa mafuta) ni mambo mawili tofauti.

Ili upenye na kuwa na kibali jitahidi ufike viwango vya kuwa anointed kwa kujitakasa na kuwa msafi Sana

Uzinzi , negativity , bad conscience na kushindwa kuwa mtohaji haya mambo yote yanaweza Ku-block njia yako ya huduma.

Mwisho :
Kibali ndo kila kitu hivyo anza huduma yako na toa huduma yako bure ili utengeneze kibali ktk maisha yako ya kiroho.
 
eti ufundishwe utafikiri ni kama kucheza step za kwaito.
 
Kondoo wa bwana
Nakushauri kama unataka uielewe dini isome na uielewe mwenyewe..coz we kusema uje kufundisha "kondoo" inaonekana vilivyopo Katika biblia havieleweki inabidi atokee mtu outta nowhere atuelekeze...ila so far endelea tu ..
 
Ili uweze kuhubiri vizuri,nenda kasome chuo cha biblia,vipo vingi,mtu asikudanganye eti ukisoma Biblia tu unaw3za kuhubiri,mbona watu wengi wana Biblia na hawana wanachojuwa kwenye Biblia? Nenda shule zipo nyingi.
 
Jheone ya Reoo! Kaza sauti kama mashimo utatoboa....Mtafute mbongo movie mmoja awe anaandaa script za maigizo ya miujiza.
 
Hongera sana kwakuwa una nia njema, ushauri wangu, usikimbilie kusoma kabla ya kulijua neno, kwasababu unaweza kusoma lakini usipolijua neno utashindwa kuhubiri.

unalijuaje neno?
1. mpokee Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako huku ukiyaacha ya kale
2. Tafuta msaada wa kiroho katika kanisa lililo karibu na wewe.
3. Soma Bibilia na fuatilia mafundisho ya Mungu, kwenye Tv na kwenye radio station(hapa kuwa muangalifu, kuna baadhi ya Tv na Radio hazihubiri neno la Mungu wamekomaa na miujiza)

4. Kundi la Watsap sikushauri sana maana wengine wameanzisha makundi ya watsap kama ngazi ya kupandia, ataweka mada lakini akivutia kwake

Ubarikiwe saa
 
Kwa imani yako, acha dhambi, pata toba, omba nguvu ya Roho Mtakatifu...kisha anza kazi ya Mungu..!
 
Habari wakuu

Kama kichwa kinavyosema hapo juu naomba msaada,pia kama Kuna group za Whatsapp naomba kuunganishwa.
Onana na Roho Mtakatifu, kila kitu kitaenda sawia endapo hiyo ni karama yako!
 
Back
Top Bottom