Naomba hii Ndoto niliyoiota Usiku wa leo isiwe ya Kweli

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Nimeota kumbe Gari Chiba lilishachomwa Moto Kitambo tu na kwamba kwa sasa Picha ya Gari inatafutwa ili Snipers watafutwe na walipige Risasi vile vile na Watafutwe Wataalam walirejeshe kama lilivyokuwa Siku hiyo ndipo Chiba akabidhiwe Kelele ziishe Mtaani.

Chiba na Wewe kuwa Mvumilivu Kwanza kwani Wataalam bado wanahangaika Kulikongoroa kama lilivyokuwa hivyo ukiona unakwepwa lilikohifadhiwa jua bado Mafundi wa Gereji Kuu Wilaya ya Ilala, baadhi wa Makumbusho na wa Dodoma wanahangaika nalo.

Ila Chiba umewashika Watu pabaya mno kwani wao Walijua hutorejea kabisa hivyo likatokomezwa kabisa pamoja na Watendaji waliokosea Mission nao Kutokomezwa mazima sasa Wewe umerejea badala ya Kuulizia Mafuta ya Alizeti ya Kwenu umekimbilia kutaka Ndinga ( Motokaa ) yako.

Kazi ipo.......!!!!!!!
 
Duuh hizi ndoto zako uache kunywa mataputapu sasa
 
Jamaa kaenda kwa upole sana, jamani naombeni ile gari yangu.........
 
Mambo ya huku kwetu ya kiswahili Sana AISEH!!

Ina maana waliii..........!!!!??hadi aiseh Hawa jamaa hawa !!

Ngoja tuone!
 
Aisee, kama kweli hiyo nayo ni kashfa ya kufa mtu. Kama ule upanga wa dhahabu uliyopotea mikononi mwao miaka ile.
 
ndoto ya kimweri
 
Unamuita Chiba wakati wewe ndo ulimtia ulemavu! Mungu anakuona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…