Iko hivi, wapinzani wanajua Magufuli aliwamaliza wakakosa sera na kutupwa kule. Wakakosa hoja, na ushawishi. Wakadharaulika na kukosa kura. Hii yote ni kutokana na uzalendo, ujasiri, ubunifu, uchapakazi, utambuzi, akili na maono ya Magu.
Na kwa sababu siyo wabunifu ikabidi wakimbilie mitandaoni na kuanza kutukana, kupiga propaganda za kuchafua, lakini kwa miaka 5 haikuwasaidia! Watanzania wakaonyesha support kubwa sana kwa Magu.
Ndiyo maana hata baada ya kifo cha Magu bado wanateswa sana na kivuli cha Magu. Wanatumia nguvu sana kuonyesha Magu si kitu. Lakini kuna tofauti kubwa Kati ya propaganda na uhalisia! Na bahati mbaya mambo aliyoyafanya ni halisi na siyo superficial Kama lawama zao. Huwezi ukakosoa ujenzi wa miundo mbinu ambao hata kipofu anaona umepunguza foleni, umerahisha usafiri, umepunguza gharama za usafiri na maisha! Uwezi ukakosoa nidhamu ya watumishi wa umma kuimarika kwa kiasi kikubwa, huwezi ukalazimisha kwamba uchumi haujakuwa, huwezi ukadanganya kwamba majambazi wameongezeka, ajali zimeongezeka, rushwa imeongezeka wakati vyote hivyo vimepungua kwa kasi ya ajabu.
Kwa hiyo wanavyompamba SSH ili aache mbinu za Magu ambazo ni proved zimewapiga mieleka miaka 5, kwa mahesabu kwamba akilegeza watapata upenyo.
Na wakikata upenyo Muda ukifika utaona watakavyomshambulia SSH!