Naomba kuelezwa : Iran akimiliki Nuclear Israeli inamhusu nini?

Naomba kuelezwa : Iran akimiliki Nuclear Israeli inamhusu nini?

Labda kuna sheria za kimataifa ndiyo sikatai. Najiuliza tu Iran akimiliki nuclear Israeli inam-bother nini?

Je, Israel hana nuclear? Nadhani anayo. Kwanini sasa amemvamia Iran?

Yaani mimi ninunue AK47 huyu jirani yangu aanzishe vita? Naomba kueleweshwa na non-mashabiki wa vita.
Unaweza kukubali jirani yako kichaa amiliki bunduki?

Vv
 
Kila siku kwa miaka 25 Ayatollah amekuwa akijiapiza kuwa "Israel itatoweka kwenye uso WA dunia"

Akili za waajemi kama bodaboda, angalia wanavyotupa makombora, jiulize wangekuwa na kitu HIROSHIMA si wangerusha Hadi Kizimkazi hapo jirani!
Alright, kwa hiyo kwasababu ya vitisho vya kila siku ndivyo vilivyomfanya Israel amvamie Iran kabla hajawa na Silaha za Nuclear.

Iran ana Nuclear? Kwanini hazitumii kwenye haya majibizano!
 
Una bifu na jirani yako mlevi, wewe unamiliki bastola halafu jirani yako mlevi yupo kwenye mpango wa kununua AK47 Utamwacha anunue?
Ndicho anachokifanya Israel kuzuia jirani mlevi asitumie ile 47
 
Una bifu na jirani yako mlevi, wewe unamiliki bastola halafu jirani yako mlevi yupo kwenye mpango wa kununua AK47 Utamwacha anunue?
Ndicho anachokifanya Israel kuzuia jirani mlevi asitumie ile 47
Unatuchukulaje walevi wewe creature?
 
Anaogopa kufutwa kwenye uso wa dunia, lakini kashachelewa hata sasa anaweza kufutwa
 
Kumiliki nuclear sio tatizo, bali tatizo n matumizi ya hiyo nuclear.

Matumizi ya nuclear sio tatizo, tatizo unatumia kufanya nini/lengo gani.

Nchi nyingi zinamilikiwa nuclear kwa lengo la silaha ila hayana tishio kwa mataifa mengine mfano USA.

Iran ina nuclear Ila kwa lengo la vita ndo mana wana sehemu ya siri ya hiyo nuclear kitu ambacho ni kosa mana hairuhusiwi kuwa n sehemu ya siri.

Kosa la kwanza la Iran n kuwa na eneo la siri kwa ajili ya hizo nuclear ndo wanaona hawa makobazi watakuja kuwa tishio.
Sheria za kimataifa zinaruhusu nchi yoyote kumiliki Nyuklia ilimradi nchi husika haitishii nchi zingine wakati inategeneza nuclear. Kama nimekupata vizuri.

Lakini Marekani amekuwa kwenye vita kibao lakini ana Nuclear, Russia yupo kwenye vita hadi sasa lakini ana nuclear.

Silaha zinatengenezwa kwa ajili ya nini sasa? Maana silaha ni ya vita mura. Uwe umetangaza vita wakati unatengeneza au haujatangaza ....ukishatengeneza silaha hiyo silaha ni ya vita.
 
India, Pakistan,UK,US,France, Russia,China,North Korea,wote hao Wana Nuclear,tatizo Iran and chuki na Israel and kawaapiza kua atawamaliza kwa Bomb,mtu huyo utaruhusu awe na Bomu??
 
Alright, kwa hiyo kwasababu ya vitisho vya kila siku ndivyo vilivyomfanya Israel amvamie Iran kabla hajawa na Silaha za Nuclear.

Iran ana Nuclear? Kwanini hazitumii kwenye haya majibizano!
Hana.
 
Back
Top Bottom