Naomba kuelezwa kuhusu Shahada ya Uzamili ya Public Health

mutu murefu

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2017
Posts
996
Reaction score
2,636
Wasalaam wana jamvi!

Mimi ni kijana ambaye baada ya kumaliza degree yangu mwaka juzi nikaunganisha kusoma master. Kwa sasa nasoma master of public health (MPH) hapa Muhimbili nategemea kumaliza mwaka huu.

Naombeni kujua kutoka kwa wadau wanaoijua hii ishu ninayosomea kazi zake katika private sectors na international organizations

Je ni kweli zipo kama tunavyoambiwa? Na salary zake zipoje? Na pia nitapenda kama mtanipa mawazo mbalimbali na mapendekezo kuhusiana na mada husika.

Naamini kuna watu pia watajifunza kwenye mada hii.

Asanteni!
 
MPH siku hizi inasemekana haina soko sana kama zamani wakati wasomi walipokuwa wachache..
Siku hizi naskia hata anayesoma MMED lazima asome na MPH kwahio MMED woote wanaweza kufanya na kazi zakiutawala kama MPH kwahio soko linachange hivyo.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuuliza walioko kwenye system..
I stand to be corrected

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini wewe Mutu MUREFU kipi kilikusahaulisha hadi toka unaanza kusomea issue hii ushindwe kuuliza then uje kuuliza leo ukiwa unakaribia kumaliza?

Kwanini kabla wakati unaanza hukuuliza kwanza ili ujue kama inafaa au haifai ili ubadilishe mapema?hapa naona utajipa stress tu muhimu omba Mungu umalize akusaidie upate pakujishikiza ila kosa ulilifanya toka mwanzo.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
First degree yako ulifanya Kwenye medical or non medica course?
 
MPH siku hizi inasemekana haina soko sana kama zamani wakati wasomi walipokuwa wachache..
Siku hizi naskia hata anayesoma MMED lazima asome na MPH kwahio MMED woote wanaweza kufanya na kazi zakiutawala kama MPH kwahio soko linachange hivyo.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuuliza walioko kwenye system..
I stand to be corrected

Sent using Jamii Forums mobile app

Oh sawa asante kwa mawazo yako mkuu shukrani
 
Lakini wewe Mutu MUREFU kipi kilikusahaulisha hadi toka unaanza kusomea issue hii ushindwe kuuliza then uje kuuliza leo ukiwa unakaribia kumaliza?

Kwanini kabla wakati unaanza hukuuliza kwanza ili ujue kama inafaa au haifai ili ubadilishe mapema?hapa naona utajipa stress tu muhimu omba Mungu umalize akusaidie upate pakujishikiza ila kosa ulilifanya toka mwanzo.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk

Niliulizia nikaambiwa iko vizuri na ina soko... sasa juzi kati kuna mtu akaniambia haina soko now ndo mana nikaja kwenu wajuvi wa mambo mnisaidie
 
Bachelor of health systems management from mzumbe university

Bachelor degree yako Ni marketable kwa sasa kwa level yako Kuliko masters

Mpango wa Sasa hivi wa Serikal ni kuunganisha Hospital zote a Rufaa, Mikoa mpaka a Wilaya Na Mfumo wa Tehama hivyo ndani ya Muda mfupi kutakuwa Na mahitaji ya watu wa IT, sasa advantage yako Itakuwa Wewe Ni Mtu wa IT Tena ya upande wa Health

Kama uta fanikiwa kupata ajira then Baada ya Muda mfupi wa experience hiyo Masters yako Kama utafanikiwa kumaliza ndio Itakuwa added advantage ya kupata nafasi ya senior level but inategemeana Na uwezo wako wa kufanya kazi sio cheti peke yake.
 
Haina soko kwa sasa kuna mdada namfahamu alimaliza mwaka juzi hadi sasa yupo tu mtaani anaungaunga maisha...

PH ilikuwa zamani
 
Bachelor degree yako Ni marketable kwa sasa kwa level yako Kuliko masters

Mpango wa Sasa hivi wa Serikal ni kuunganisha Hospital zote a Rufaa, Mikoa mpaka a Wilaya Na Mfumo wa Tehama hivyo ndani ya Muda mfupi kutakuwa Na mahitaji ya watu wa IT, sasa advantage yako Itakuwa Wewe Ni Mtu wa IT Tena ya upande wa Health

Kama uta fanikiwa kupata ajira then Baada ya Muda mfupi wa experience hiyo Masters yako Kama utafanikiwa kumaliza ndio Itakuwa added advantage ya kupata nafasi ya senior level but inategemeana Na uwezo wako wa kufanya kazi sio cheti peke yake.

Okay sawasawa mkuu nashukuru sana kwa mawazo yako mazuri
 
Unasoma soma tu hovyo
Nenda kazni fanya kazi ndo ujue unaongeza wapi

Sent using Jamii Forums mobile app

Nilimaliza 2017... nikapata kazi kufundisha chuo cha diploma nikafanya kazi kwa mwaka mmoja na kitu (since july 2017 mpaka november 2018) ndipo nikaja kusoma hapa (ni one year kwa muhimbili)

My interest ni kupata kazi international organizations maana niliambiwa wanalipa pesa ndefu sana kwa MPH
 
Unaona sasa matatizo yko unasomea mshahara ko ikitokea umekosa hzo int org n sawa na kupoteza mda

Du kweli wonders will never end.

Hivi unaanzaje kusoma kitu usichokipenda na usichojua hatima yake. Kama unapenda kufanya kazi kwenye health sector hats ukiwa Nurse, you name it. Kazi zipo nyingi Sana BUT, unatafuta ajira ama unataka kutoa huduma au kujenga carrier au kupata pesa.

Ukimaliza fanya kazi ya kuvolunteer miezi miwili kwenye mojawapo ya hospitality, onyesha umahiri wako utapata kazi nje ya hapo, Betting inalipa zaidi kuliko kukaa bure.
 
Mkuu in most cases watu wengi husomea vitu vyenye soko la ajira... na hata mimi kipindi naenda kusoma niliulizia about this nikaambiwa iko vizuri... ni hivi recently tu mtu akaniambia kuwa haina soko ndipo nikaona niulize wadau humu
 
Du kweli wonders will never end.

Hivi unaanzaje kusoma kitu usichokipenda na usichojua hatima yake. Kama unapenda kufanya kazi kwenye health sector hats ukiwa Nurse, you name it. Kazi zipo nyingi Sana BUT, unatafuta ajira ama unataka kutoa huduma au kujenga carrier au kupata pesa.

Ukimaliza fanya kazi ya kuvolunteer miezi miwili kwenye mojawapo ya hospitality, onyesha umahiri wako utapata kazi nje ya hapo, Betting inalipa zaidi kuliko kukaa bure.

Mkuu sio kwamba sina kazi kabisa hapana... nina kazi tayari ninafundisha chuo... but kufundisha sio interest yangu na my professional yangu ni health secretary (katibu wa afya). My interest ilikua kufanyia international organizations na ndipo nikashauriwa nisomee MPH. (Ndo mana nkauliza humu leo maana info niliopewa awali na niliopewa juzi kati znaniweka dillema ndo mana nikaja hapa nipate hakika)

But hata kama ntakosa huko international organizations haina shida maana masters itaniongezea salary kwny kazi yangu nikimaliza narudi kazini kufundisha chuo.
 
Back
Top Bottom