Habari mkuu.
Nashukuru kwa kufanya followup, naamini kuna watu watajifunza kupitia uzi huu.
Nilifanikiwa kumaliza MPH pale MUHAS mwaka 2019, namshukuru Mungu nilipata award ya mwanafunzi bora kwa MPH class of 2019. Naamini baadhi ya classmates wangu wapo humu (nawasalimu naamini mshanijua tayari, it was a wonderful experience kuwa nanyi, i miss u sana)
Baada ya kuhitimu nilianza kufanya part time kufundisha chuo masomo ya research, epidemiology and biostatistics. Baadae nkapata kufanya kazi za muda mfupi kwy projects za mashirika mbalimbali kama
1. Schupa Tansania E.v - Germany
2. Finnish christian Medical society - Finland
3. Finnish Rotary doctors Bank - Finland
Katika kipindi hicho nimezunguka nchi almost 10 za ulaya sababu ya hizo projects (kwa ajili ya training, workshops and conferences).
Lakini pia nimekua nafanya research consultancy kwa masters students wanaohitaji assistance kwa gharama nafuu sana.
Currently, ni zonal project coordinator wa shirika fulani (sitalitaja kwa sasa, maana nna wiki moja since nianze kazi).. ni coordinator kwa mikoa mitatu ya kusini.
Kiufupi i feel proud kusoma MPH, kama nisingesoma sjui ningekua wapi. Nawaasa ndugu zangu usikatishwe tamaa na mtu yoyote ukiamua kufanya kitu muonbe Mungu wako yeye ndo anajua kesho yako.
Asanteni wakuu