Kampuni inapoanzishwa shareholders huchangia mtaji. Mtaji ndo unakupa equity kwenye kampuni. Kwa mfano unaweza kuanzia kampuni yenye share 20,000 kwa mtaji wa TZ 10,000,000. So kila mwana hisa atalazimika kununu hisa na kiasi cha pesa anazotoa ndo kinathamanishwa na hisa atakazokuwa nazo. Kwa mfano mkiwa wawili mmoja akatoa TZS 7,500,000 atakuwa na hisa 15,000 sawa na 75% na atakaye toa 5,000,000 atakuwa na hisa 5000 sawa na 25% ya kampuni.
Sasa baada ya kutoa kiasi cha mtaji mnaohitaji ikiwa bado kuna uhitaji wa kuongeza mtaji mnaweza kuongeza kwa njia mbili.
1. Kuongeza hisa zikafika say 30,000,000 halafu mkanunua hizo shares 10,000,000 zilizoongezeka ili kuongeza mtaji.
2. Kuacha hisa kama zilivyo na kuamua kukopa fedha popote pale. Mwanahisa pia anaweza kuikopesha kampuni.
Mkopo wowote ni lazima uidhinishwe na Board ya kampuni. So mtaandaa kikao na kuandika muhutasari unao onyesha kuwa Board imeridhia kukopa na condition za mkopo ikiwemo interest.
Then mtaandaa mkataba ambao utasainia na mwenyekiti wa Board, na mkopeshaji husika.
Deni litasomeka kama liability kwenye vitabu vya kampuni na malipo ya mkopo hayana kodi. Ila yule anayepokea marejesho hatalipa akipokea principal amount ila atatakiwa kulipa kodi akipokea faida (interest) hii itakatwa kodi kama personal income tax.
Kingine cha kuzingatia ili usiingie kwenye migogoro ni kuangalia riba iwe within the market interest. Kwa mfano kwa sasa riba nyingi hazizidi 17%. Kujipa mkopo wa 30% inaweza kuonekana kama aina fulani ya kuhujumu kampuni. Vyombo husika vinaweza kufuatilia kujua kama ulikuwa na motive gani na hivyo kukuletea shida.
Kwa sasa ni hayo tu.