Chief Ortambo Ikumenye
JF-Expert Member
- Nov 16, 2017
- 247
- 503
- Thread starter
-
- #21
Mbona wengine wameelewa mkuu? Up your IQ utaelewa tu mbona. Halafu nimeweka kwa lugha rahisiNiwe mkweli sijakuelewa kabisa kabisa.
Au ni hicho kizungu au ni nini sijui?
Kibishi tu hivo hivo maisha yenyewe hayaa ambayo hatuishi milele, sio vibaya kujaribuHiyo ya mimi na wifeitafika kweli?
Tulivyo na visirani, sijui.
Unakera sana, ni vile hujajua tu. Kama hujui kitu usipende kumwaga shombo, chukua time kukijua, na sio unaanza ku comment ushuzi.Kumbe kitu chenyewe tayari unakijua.......mkuu vepee?
Unakulaga ndumu?
Wewe unatafuta kesi ya kukwepa Kodi na uhujumu uchumiIkiwa kwa mfano kuna kampuni ya watu wawili (upo wewe na wife) na si huwa tunasikia kwamba kampuni ni mtu kisheria.
Sasa mfano shareholders (wewe na wife) mkaazimia kuikopesha kampuni ambapo ije kusomeka kwenye financials kama shareholders loan.
Sasa maswali yangu ni haya yafuatayo
1. Ili kujiweka safi dhidi ya TRA na mamlaka nyinginezo kama BRELA, kuna documentations zipi au taratibu zipi za kufuata ili kukamilisha hiyo transaction? (Je Board Resolution yaweza kutosha kusema kwamba shareholders wameazimia kuikopesha kampuni kiasi fulani kwa riba na tenor fulani?
2. Je, huo mkopo si una qualify kwa kampuni kulipa riba iliyokubaliwa? Au kuna any restrictions zozote
3. Na kwa mfano nikiamua kwamba niweke riba ya let say 25% au 30% per annum, je kunaweza kuwa na tatizo lolote?
Lengo langu haswa kuhusu hili swala na swali ni kwamba mimi ni mtu napendelea sana kufanya uwekezaji, sasa kulingana na long term vision nimeona kwamba kunaweza kuwa na advantage endapo nikiwa natumia kampuni kufanya hizo investments badala ya mimi kama private person.
Nahisi kwamba kuna advantage fulani fulani na ndo najaribu kuzi explore.
Nakwepaje kodi na hiyo practice ipo allowed kisheria?Wewe unatafuta kesi ya kukwepa Kodi na uhujumu uchumi
Halafu uhujumu uchumi kesi yake Haina dhamana
Unaweza kutuona vilaza ila Kuna namna unaweza onekana umekwepa Kodi, mfano unajikopesha hapo afu unajikopesha na riba, unakampuni ya kukopesha ela? Wataona unaiingiza kampuni kwenye mikopo Ili mwisho wa siku faida iwe 0 maana ndo ile umeihamishia kwenye mkopoNakwepaje kodi na hiyo practice ipo allowed kisheria?
ukitoa mkopo sio lazima uwe una kampuni ya kukopesha au leseni. Kuna mikopo ambayo haipo regulated popote mfano hii ya watu kukopeshana kimtaani, mbona haikatazwi?Unaweza kutuona vilaza ila Kuna namna unaweza onekana umekwepa Kodi, mfano unajikopesha hapo afu unajikopesha na riba, unakampuni ya kukopesha ela? Wataona unaiingiza kampuni kwenye mikopo Ili mwisho wa siku faida iwe 0 maana ndo ile umeihamishia kwenye mkopo
All the best mkuu Mimi sio expert wa hizo mambo just shared the little I know
"".....ila atatakiwa kulipa kodi akipokea faida (interest) hii itakatwa kodi kama personal income tax.""Kampuni inapoanzishwa shareholders huchangia mtaji. Mtaji ndo unakupa equity kwenye kampuni. Kwa mfano unaweza kuanzia kampuni yenye share 20,000 kwa mtaji wa TZ 10,000,000. So kila mwana hisa atalazimika kununu hisa na kiasi cha pesa anazotoa ndo kinathamanishwa na hisa atakazokuwa nazo. Kwa mfano mkiwa wawili mmoja akatoa TZS 7,500,000 atakuwa na hisa 15,000 sawa na 75% na atakaye toa 5,000,000 atakuwa na hisa 5000 sawa na 25% ya kampuni.
Sasa baada ya kutoa kiasi cha mtaji mnaohitaji ikiwa bado kuna uhitaji wa kuongeza mtaji mnaweza kuongeza kwa njia mbili.
1. Kuongeza hisa zikafika say 30,000,000 halafu mkanunua hizo shares 10,000,000 zilizoongezeka ili kuongeza mtaji.
2. Kuacha hisa kama zilivyo na kuamua kukopa fedha popote pale. Mwanahisa pia anaweza kuikopesha kampuni.
Mkopo wowote ni lazima uidhinishwe na Board ya kampuni. So mtaandaa kikao na kuandika muhutasari unao onyesha kuwa Board imeridhia kukopa na condition za mkopo ikiwemo interest.
Then mtaandaa mkataba ambao utasainia na mwenyekiti wa Board, na mkopeshaji husika.
Deni litasomeka kama liability kwenye vitabu vya kampuni na malipo ya mkopo hayana kodi. Ila yule anayepokea marejesho hatalipa akipokea principal amount ila atatakiwa kulipa kodi akipokea faida (interest) hii itakatwa kodi kama personal income tax.
Kingine cha kuzingatia ili usiingie kwenye migogoro ni kuangalia riba iwe within the market interest. Kwa mfano kwa sasa riba nyingi hazizidi 17%. Kujipa mkopo wa 30% inaweza kuonekana kama aina fulani ya kuhujumu kampuni. Vyombo husika vinaweza kufuatilia kujua kama ulikuwa na motive gani na hivyo kukuletea shida.
Kwa sasa ni hayo tu.
UMENIWAZISHA VYEMA..!!!mbona kama imekaa kiutata ni kama unafanya money laundering maana kampuni ni yako tena changa alafu ni mkurugenzi na mmiliki unajikopesha pesa kwa mlolongo huo na jinsi nchi hii ilivyojaa wanaa hawachelewi kukutia mbaroni kwa kesi ya kutakatisha pesa si unaikopesha kampuni alafu tena kampuni ikurudidhie hiyo pesa na kwa vile ww ndio top kwenye kampuni bila shaka utakuwa mmoja wa signatory kwenye benki akaunti ya kampuni.!
Bonge la swalii ila mtoa majibu HAKUNA.Hiyo ya mimi na wife itafika kweli?
Tulivyo na visirani, sijui.
Nimeeleza hapo. Itisha kikao cha board, andaa muhtasari. Deposite hela kwenye account ya kampuni. Then utakuwa unaionyesha kwenye vitabu vya mahesabu vya kampuni.Hiyo option ya kuongeza hisa si inabidi kufanya alteration ya Memart of which ni process yenye mlolongo mrefu.
Hapo kwenye riba nimekuelewa, kwamba inatakiwa iwe ina reflect market.
Issue yangu kubwa sasa, ni namna gani hii process inaweza kukamilika ya mimi kuikopesha kampuni. Kuna taratibu zipi za kufuata ili isionekane baadae kuna taratibu zilivunjwa
Unamuweka alafu unampa share 1 au 2. Kama umempa share nyingi jua umetafuta matatizo ya siku zijazo (unless awe mwanamke mwenye akili na busara).Ninachojua kufungua kampuni Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, ni lazima wamiliki waanzilishi wawe kuanzia wawili. Hiyo kanuni naiona ni changamoto kubwa kwani maono na ndoto za Maisha ni za mtu binafsi. Sasa ikiwa unataka baadaye kampuni irithishwe kizazi chako ambapo wakati wa kufungua huna watoto wakubwa, utafanyaje zaidi ya kumuweka pia mke wako (ingawa moyoni hautaki) hata kwa share ndogo Ili kutimiza kanuni ya kuwa zaidi ya mtu mmoja?