Prakatatumba abaabaabaa
JF-Expert Member
- Aug 2, 2022
- 1,842
- 6,087
Nimekuja kwenu kupata elimu kutoka kwa wazoefu,
Mimi ni mtumishi Mwalimu nipo kigoma, kwa mara ya kwanza nilipata shamba Hekari 6 kigoma, nikafikiri cha kufanya nikaona nilime migazi hekari zote sita, migazi ni mti unaotoa mafuta ya mawese, pamoja na mafuta ya mise, mafuta yanayotumika kutengenezea sabuni za gwanji. Miti ya kisasa aina ya tenera inaanza kutoa migazi baada ya miaka 4 mpaka 5.
Nimepata tena Hekari 30 za pamoja, nafikiria kupanda zao la muda mrefu, ulimaji kwa kigoma naona ni mgumu siwezi kulima mahindi au maharage kwa sababu asilimia kubwa wanatumia jembe la mkono, nilipo sijawahi kuona tractor zikifanya kazi, na nguvu kazi ni warundi na gharama ya kulima Hekari 30 naona ni kubwa, nina mawazo mawili, wazo la kwanza nilitaka nilime mkonge au katani Hekari zote 30, pia wazo la pili nilitaka nilime mikorosho.
Swali langu je naweza toa miche ya mikorosho uko kusini na ikakubali vizuri kwa ukanda huu wa kigoma? Au wazo gari unaloliona ni bora ili hii ardhi iwe productive?