Naomba kuelimishwa kama ungekuwa na shamba Hekari 30, ungelima au ungelifanyia shughuli gani?

Nafkir wakt unawaza upande nn pia waza hzo changamoto unazkabili vp,,mfano kama hamna tractor na hujawah kuona huon kama ukipambna siku moja hzo nyenzo zkapatkana utakua umefankiwa??
 
Lima citrus, hili wazo sijawahi skia mtu akilishobokea ni kilimo kilichojificha.

Kama Kuna access ya maji kwa urahisi, miti kama limao na ndimu ndio mahala pake.

Tafuta mbegu ya muda mfupi sana na mbolea ya kukuzia, kukubwa maji yawepo.
Haya mazao kukiwa na maji hayana msimu ukichuma maua yanachanua.
 
Endelea na kilimo cha migazi, labda unaweza kuweka na miti ya mbao mfano mikaratusi au cedrella....mifugo inahitaji usimamizi wa karibu, ukicheza tu unapoteza hela.

Unapokuwa kwenye ajira na ikiwa hiyo ajira ndiyo inaendesha maisha yako, hakikisha uwekezaji unaofanya nje ya ajira usiwe ni ule wa kukulazimu kutumia muda mwingi kusimamia kwa kuwa muda huo hutopata unless uwe ni mtoro kazini jambo ambalo siyo zuri....miti ya mbao au migazi inaweza kujiendesha yenyewe wewe ukiwa mbali.
 
Soko la limao lipo?, nafikiri ekari 5-10 nipande coconut.
 
Kwanini usilime avocado zile maarufu kutoka Burundi maana msimu wake uwa parachichi kwa tz ni chache hivyo kuwa na bei nzuri
 
Pia kuhusu kilimo kama ardhi ni mwinuko wa wastani hanza na ngombe wa makisai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…