A
Anonymous
Guest
Habari, wana-JamiiForums.
Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu ninayetarajia kuingia mwaka wa tatu hivi karibuni. Nimebaini kuwa HESLB imeweka kiasi cha TSh 2,310,000 kama jumla ya malipo ya MA (boom) kwa mwaka, badala ya TSh 2,400,000 kama ilivyoelezwa kwenye mkataba wangu.
Aidha, kiasi kilichoonyeshwa kwa kila awamu ya malipo (disbursement) ni TSh 577,500 badala ya TSh 600,000.
Naomba kufahamu kama HESLB imefanya mabadiliko katika mfumo au viwango vya malipo ya boom kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo (continuing students), tofauti na masharti yaliyokuwa kwenye mikataba yao. Au je, hili limetokea kwenye akaunti yangu pekee, huku wanafunzi wengine wakiendelea kupata kiasi kilichoainishwa kwenye mikataba yao?
Ningependa kupata ufafanuzi kutoka kwa wanafunzi wenzangu wenye hali kama hii au mtu yeyote mwenye taarifa sahihi kuhusu suala hili.
Asanteni.