Naomba kufahamishwa kuhusu hili juu ya former first lady, Janeth Magufuli

Naomba kufahamishwa kuhusu hili juu ya former first lady, Janeth Magufuli

WINGER_TEREZA

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2015
Posts
242
Reaction score
457
Wanajamvi habarini,

Ama baada ya salam naomba nijielekeze moja kwa moja kwenye mada yangu. Kwa ninavyofahamu mke wa hayati John Magufuli, Janeth Magufuli, alikuwa Mwalimu na kama sijakosea alikuwa ni Mwalimu wa shule ya Msingi ila alikoma kushika chaki mara tu baada ya Hayati Magufuli kushinda uchaguzi na kuwa Rais wa Tanzania mnamo mwaka 2015.

Nadhani "alistafishwa" kushika chaki ili apate muda wa kutosha wa kukitumikia cheo chake kipya cha "First Lady" alichokipata baada ya Mumewe kushika wadhifa wa Urais.

Sasa nigependa kufahamu vipi our former first lady, Janeth Magufuli, atarudi Shuleni kuendeleza majukumu yake aliyokuwa "amestafishwa" ya Ualimu mara baada ya cheo chake cha "First Lady" kukoma kutokana na msiba wa Mume wake ambaye alikuwa ni Rais wetu mpendwa? Au atakaa tu nyumbani na kula pensheni au hapo inakuwaje wajuvi?

Asante, naomba kuwasilisha
 
Ingekuwa wewe ndio mama Janeth ungerudi tena kufundisha baada ya mumeo ambae alikuwa raisi kufa?
Jibu lako ingekuwa ni wewe naamini pia ndio jibu la swali lako ulilouliza.
Zingatia pia kuwa mshahara wa mwalimu wa shule ya msingi ni 320,000/
Kwani umeulizwa utaje mshahara wa mtu!!
 
Ingekuwa wewe ndio mama Janeth ungerudi tena kufundisha baada ya mumeo ambae alikuwa raisi kufa?
Jibu lako ingekuwa ni wewe naamini pia ndio jibu la swali lako ulilouliza.
Zingatia pia kuwa mshahara wa mwalimu wa shule ya msingi ni 320,000/
Hahahaha, sawa Mkuu kwa huo mshahara ulioweka hapo nimekuelwa.
 
Tulikwambia sisi ni wapiga ramli?
Subiri amzike mumewe kisha uende ukamuulize huo upuuzi wako.
Kwani wapiga ramli ndio wanaopaswa kuulizwa maswali? Kama hutaki kuulizwa maswali uwe una soma comments na post tu sio lazima kila mada uchangie acha kujifanya unajua kila kitu.
 
Ingekuwa wewe ndio mama Janeth ungerudi tena kufundisha baada ya mumeo ambae alikuwa raisi kufa?
Jibu lako ingekuwa ni wewe naamini pia ndio jibu la swali lako ulilouliza.
Zingatia pia kuwa mshahara wa mwalimu wa shule ya msingi ni 320,000/
Wewe, Kuna walimu shule ya Msingi wanakula hadi 2m, inategemea na umri kazini na elimu. Me mshua wangu anakula 1,300,000/- basic salary.
 
Kwani wapiga ramli ndio wanaopaswa kuulizwa maswali?, kama hutaki kuulizwa maswali uwe una soma comments na post tu sio lazima kila mada uchangie acha kujifanya unajua kila kitu.
Najua deep down umejua kua swali lako ni la kijjnga ndio maana unapanic,
Nenda kauze mitumba achana na mambo ya watu.
 
Ingekuwa wewe ndio mama Janeth ungerudi tena kufundisha baada ya mumeo ambae alikuwa raisi kufa?
Jibu lako ingekuwa ni wewe naamini pia ndio jibu la swali lako ulilouliza.
Zingatia pia kuwa mshahara wa mwalimu wa shule ya msingi ni 320,000/
Una mkopo nmb
 
Back
Top Bottom