Upatikanaji wake kwa Sasa umekuwa mgumu maana wakulima wengi hawapandi kutokana na soko lake kuyumba ivyo wameenda kwenye Mbaazi lakini unaweza kuipata maeneo ya Babati, Manyara au Singida
Kuna aina tatu za Ngwara ambazo ni Nyeupe, Nyeusi na langi ya udongo
Ivyo ukiwa kama mkulima inabidi ijue ipi inapendelewa sokoni maana kwa upande wa Singida wanapenda iyo langi ya udongo kuliko Nyeusi
Pia unaweza kuipanda yenyewe ama ukachanganya na Mahindi
Huwa zinapandwa katikati ya msimu maana ukiwai sana huwa zinaharibiwa na mvua