Naomba kufahamishwa kwa kina kuhusu picha maarufu ya Monalisa

Naomba kufahamishwa kwa kina kuhusu picha maarufu ya Monalisa

Mona Lisa (pia huitwa La Gioconda ambayo kwa Kiitalia ina maana ya mwanamke mchangamfu) ni mchoro maarufu wa mwanzoni mwa karne ya 16, kazi ya na mwanasayansi na mchoraji Leonardo da Vinci.

Inaaminika kuwa ni mmoja kati ya michoro mashuhuri zaidi duniani kote. Kwa sasa mchoro huu unapatikana katika jumba la maonyesho (makumbusho) la mjini Paris (Ufaransa) maarufu kama Louvre.

LABDA TUMSOME MCHORAJI LEONARDO DA VINCI
220px-Possible_Self-Portrait_of_Leonardo_da_Vinci.jpg

Leonardo da Vinci alivyojichora
Leonardo Da Vinci (Vinci, Toscana, Italia, 15 Aprili 1452Amboise, Ufaransa, 2 Mei 1519) alikuwa mtu mwenye vipajivingivingi[1] kutoka nchini Italia.

Kifupi, alikuwa mwanahisabati, mhandisi, mwanasayansi, mgunduzi, mwanaanatomi, mchoraji, mchongaji, msanifu majengo, mwanabotania, mwanamuziki na mwandishi.

Ndiye mwakilishi bora wa tapo la Renaissance.

Leonardo alikuwa mdadisi wa kila kitu asilia. Alitaka kujua kila kitu kinavyofanya kazi. Alikuwa hodari sana katika kusoma, kuunda na kutengeneza vitu vya aina mbalimbali tena vya kupendeza.[2]

Mwanahistoria wa sanaa Helen Gardner alisema hakuna mtu aliyewahi kuwa kama yeye kwa sababu alikuwa na shauku na vitu vingi sana: "...Akili yake na utu wake vinaonekana kuwa zaidi ya mtu, ni mtu wa ajabu na tofauti".

Leonardo siku zote alikuwa akifiria kugundua mambo mapya. Vitu vingi alivyogundua havikuwahi kufanywa. Hata hivyo, tunajua fikra zake, kwa sababu aliweka kwenye vijitabu na kuandika na kuvichora mara kwa mara.

Baadhi ya nadharia alizofikiria ni pamoja na helikopta, kifaru, baiskeli, kikokotoo, roboti na vifaa vinavyogeuza nishati ya juakuwa umeme.

Leonardo aliweza kufanya vitu vya aina nyingi vya kijanja, lakini alikuwa maarufu sana kama mchoraji. Watu wengi hufikiria kwamba Leonardo alikuwa mmoja kati ya wachoraji bora wa historia yote. Amefanya michoro mingi sana. Miongoni mwa picha zake, mbili zilizo maarufu zaidi duniani ni Mona Lisa na Karamu ya mwisho.

Mchoro mwingine unaojulikana sana ni Vitruvian Man. Unajulikana sana hata Homer Simpson na Garfield ambazo zilichorwa kwa mraba na mzunguko ili kuonekana kama mchoro.
Leonardo alizaliwa tarehe 15 Aprili 1452, mkoani Toscana, katika mji mdogo wa kilimani wa Vinci, katika mabonde ya Mto Arno, karibu na Florence nchini Italia.

Babu yake, Ser Antonio, anajivunia kwa kuweka kumbukumbu ya maelezo. Wazazi wa Leonardo walikuwa hawajaoana. Baba yake alikuwa mwanasheria, Messer Piero Fruosino di Antonio da Vinci.[3][4] Mama yake, Caterina, alikuwa mhudumu. Yawezekana alikuwa mtumwa kutoka Mashariki ya Kati.[5][6] Jina kamili la Leonardo lilikuwa "Leonardo di ser Piero da Vinci", ambalo lina manaa ya "Leonardo, mtoto wa Bwana Piero kutoka Vinci".

Leonardo alitumia miaka yake mitano ya awali akiishi katika nyumba ya shambani na mama yake. Halafu akaja kuishi Vinci na baba yake, mke wa baba yake aliyeitwa Albiera, mabibi/mababu zake na wajomba zake, Francesco.

Wakati Leonardo ameshakua, aliandika vitu viwili tu kuhusu maisha yake ya utotoni. Alikumbuka kwamba alivyokuwa amelala kwenye kitanda chake cha watoto nje ya nyumba yao ndege mkubwa alikuwa akipaa na kumzungukazunguka juu yake. Mikia yake ikawa inamfutafuta sura yake.[7] Kumbukumbu nyingine muhimu ya Leonardo ilikuwa vipi aligundua pango milimani wakati anapeleleza. Alikuwa na hofu kubwa sana huenda kukawa na kiumbe kikubwa cha ajabu kimejificha mle ndani ya pango. Lakini pia alikuwa na hamu na shauku ya kujua kilichopo mle ndani.

Giorgio Vasari aliandika kuhusu maisha ya Leonardo kwa ufupi baada ya kifo chake. Ameelezea hadithi za kuvutia kibao kuhusu utundu aliokuwa nao Leonardo. Anasema kwamba Leonardo alichora bamba la taarifa la mbao-mzunguko likiwa na picha ya mijoka inayotema moto. Messer Piero alichukua michoro ya mwanawe hadi Florence na kuiuza kwa wauzaji wa bidhaa za kisanaa
Leonardo alianza kuchora tangu yungali bado kijana. Alifunzwa usanii na mchongaji na mchoraji Verrocchio.

Sehemu kubwa ya maisha yake alimtumikia tajiri mmoja maarufu wa Italia.

Mwaka 1516 Leonardo alikwenda Amboise, Ufaransa, baada ya kupata mwaliko kutoka kwa mfalme Fransisko I. Kati ya mizigo aliyosafiri nayo ulikuwemo mchoro maarufu wa Monalisa.

Leonardo aliishi mjini Amboise, katika nyumba yake nzuri aliyopewa na Mfalme huyo wa Ufaransa, miaka yake ya mwisho, toka mwaka huo mpaka mwaka 1519.

Afya yake haikuwa nzuri kwa sababu alipatwa na ugonjwa wa kiharusi toka mwaka 1517, lakini taarifa za ugonjwa wake zikatolewa wiki chache kabla ya kifo chake.
Alifariki huko Amboise tarehe 2 Mei 1519 akiwa na umri wa miaka 67, akazikwa St. Hubert.
 
vitu nilivyogundua humo kuna ishu kama ya freemason,kuna society inaitwa skull n bones, kuna khits, kuhusu kanisa, kuhusu mnara wa paris kuhusu mstari wa greenwich, kuhusu machiano na olympics kuhusu mungu venus na mambo meeeengi sana na kubwa zaidi ni kwamba ile picha ya monalisa inabsura mbili ikiwamo ya huyo jamaa da vinci, na humo anasema kwamba ktk wale wafuasi wa yesu 12 na pia kuhusu maria magdalena kwamba alikuwa na mahusiano na jesus aah we jaribu kusoma vizuuri hicho kitabu utaelewa tuu.
Lete mambo mkuu
 
Jina kamili la Leonardo lilikuwa "Leonardo di Ser Piero da Vinci", ambalo lina maana ya "Leonardo, mtoto wa Bwana Piero kutoka Vinci".
------------------------------------------------
Nimependa sana utambulisho wa aina hii, kwa nini haukuendelea hadi sasa, mfano:
Mimi ningeitwa "bdo, mtoto wa Bwana Mbuya kutoka Matepwende - Namtumbo".

Hapa ndio tungefahamiana ni akina nani wanaume wa Dar, Arachuga, Chato, ama Pemba.

Hahahahhahah
 
vitu nilivyogundua humo kuna ishu kama ya freemason,kuna society inaitwa skull n bones, kuna khits, kuhusu kanisa, kuhusu mnara wa paris kuhusu mstari wa greenwich, kuhusu machiano na olympics kuhusu mungu venus na mambo meeeengi sana na kubwa zaidi ni kwamba ile picha ya monalisa inabsura mbili ikiwamo ya huyo jamaa da vinci, na humo anasema kwamba ktk wale wafuasi wa yesu 12 na pia kuhusu maria magdalena kwamba alikuwa na mahusiano na jesus aah we jaribu kusoma vizuuri hicho kitabu utaelewa tuu.
Dah mkuu una macho mangapi mbona mimi naona sura moja tu
 
Mkuu, Da Vinci Code ni fiction, not factual.
Hiyo fiction vipi,mbn ROMA kinawapa stress,na kwanini kipigwe marufuku pale kama hakina ukweli mwingi,acheni kuamini mambo ya upande mmoja,jitahidi kuyajua mengi mno kadri uwezavyo na iwezekanvyo,then choose your own way,acha uvivu na uwoga wa maarifa,DA VINCI CODE IS MORE THAN A GREATEST NOVEL mkuu!

Sent from my TECNO-Y6 using JamiiForums mobile app
 
Inaitwa Gioconda au ukipenda monalisa ni kazi ya Leonardo da vinci mtaalam wa kuchora kutoka Firenze ipo pale ufaransa katika nyumba ya sanaa ya Louvre sijawahi kwenda paris au kuisoma historia ya Leonardo da vinci ila nilipata bahati mwaka jana kwenda Firenze ila nitaisaka historia yake maana hii picha kwa wale wachoraji ina tafsiri nyingi sana hata ile nyengine nayo wataliani wanaiita ultima chena au kwa kiswahili itakuwa chakula cha mwisho kile cha yesu na wanafunzi wake pia ina maana nitaisaka kwa kweli niisome
Last supper,kna nyingine,,,,madona of the rock
 
Hiyo fiction vipi,mbn ROMA kinawapa stress,na kwanini kipigwe marufuku pale kama hakina ukweli mwingi,acheni kuamini mambo ya upande mmoja,jitahidi kuyajua mengi mno kadri uwezavyo na iwezekanvyo,then choose your own way,acha uvivu na uwoga wa maarifa,DA VINCI CODE IS MORE THAN A GREATEST NOVEL mkuu!

Sent from my TECNO-Y6 using JamiiForums mobile app
Kuwapa Roma stress na kupigwa marufuku hakumaanishi kwamba ni factual. Kuna vitabu vingapi ambavyo ni fiction na vimepigwa marufuku sehemu mbali mbali? Mfano mzuri ni "the satanic verses".
 
Hiyo fiction vipi,mbn ROMA kinawapa stress,na kwanini kipigwe marufuku pale kama hakina ukweli mwingi,acheni kuamini mambo ya upande mmoja,jitahidi kuyajua mengi mno kadri uwezavyo na iwezekanvyo,then choose your own way,acha uvivu na uwoga wa maarifa,DA VINCI CODE IS MORE THAN A GREATEST NOVEL mkuu!

Sent from my TECNO-Y6 using JamiiForums mobile app
Na hapo chini umejijibu mwenyewe. DA VINCI CODE NI NOVEL.
 
Inaitwa Gioconda au ukipenda monalisa ni kazi ya Leonardo da vinci mtaalam wa kuchora kutoka Firenze ipo pale ufaransa katika nyumba ya sanaa ya Louvre sijawahi kwenda paris au kuisoma historia ya Leonardo da vinci ila nilipata bahati mwaka jana kwenda Firenze ila nitaisaka historia yake maana hii picha kwa wale wachoraji ina tafsiri nyingi sana hata ile nyengine nayo wataliani wanaiita ultima chena au kwa kiswahili itakuwa chakula cha mwisho kile cha yesu na wanafunzi wake pia ina maana nitaisaka kwa kweli niisome
Ukirudi Fanya kuanzisha Uzi maana nina shahuku yakufahamu
 
Ukisema imechorwa na msanii Leonardo Da Vinci, unakua haujamtendea haki. Unaweza ukamuita polymath Leonardo Da Vinci maana ni mmoja wa watu extraordinary ambao wamewai kutokea duniani. Jamaa alikua ni architect, engineer, doctor, na mtu mbunifu zaidi kutokea duniani.
Unajua kuzaliwa/kutokea kwa Leonardo da Vinci kulikuaje?
 
Back
Top Bottom