Naomba kufahamishwa kwa kina kuhusu picha maarufu ya Monalisa

Mona Lisa (pia huitwa La Gioconda ambayo kwa Kiitalia ina maana ya mwanamke mchangamfu) ni mchoro maarufu wa mwanzoni mwa karne ya 16, kazi ya na mwanasayansi na mchoraji Leonardo da Vinci.

Inaaminika kuwa ni mmoja kati ya michoro mashuhuri zaidi duniani kote. Kwa sasa mchoro huu unapatikana katika jumba la maonyesho (makumbusho) la mjini Paris (Ufaransa) maarufu kama Louvre.

LABDA TUMSOME MCHORAJI LEONARDO DA VINCI

Leonardo da Vinci alivyojichora
Leonardo Da Vinci (Vinci, Toscana, Italia, 15 Aprili 1452Amboise, Ufaransa, 2 Mei 1519) alikuwa mtu mwenye vipajivingivingi[1] kutoka nchini Italia.

Kifupi, alikuwa mwanahisabati, mhandisi, mwanasayansi, mgunduzi, mwanaanatomi, mchoraji, mchongaji, msanifu majengo, mwanabotania, mwanamuziki na mwandishi.

Ndiye mwakilishi bora wa tapo la Renaissance.

Leonardo alikuwa mdadisi wa kila kitu asilia. Alitaka kujua kila kitu kinavyofanya kazi. Alikuwa hodari sana katika kusoma, kuunda na kutengeneza vitu vya aina mbalimbali tena vya kupendeza.[2]

Mwanahistoria wa sanaa Helen Gardner alisema hakuna mtu aliyewahi kuwa kama yeye kwa sababu alikuwa na shauku na vitu vingi sana: "...Akili yake na utu wake vinaonekana kuwa zaidi ya mtu, ni mtu wa ajabu na tofauti".

Leonardo siku zote alikuwa akifiria kugundua mambo mapya. Vitu vingi alivyogundua havikuwahi kufanywa. Hata hivyo, tunajua fikra zake, kwa sababu aliweka kwenye vijitabu na kuandika na kuvichora mara kwa mara.

Baadhi ya nadharia alizofikiria ni pamoja na helikopta, kifaru, baiskeli, kikokotoo, roboti na vifaa vinavyogeuza nishati ya juakuwa umeme.

Leonardo aliweza kufanya vitu vya aina nyingi vya kijanja, lakini alikuwa maarufu sana kama mchoraji. Watu wengi hufikiria kwamba Leonardo alikuwa mmoja kati ya wachoraji bora wa historia yote. Amefanya michoro mingi sana. Miongoni mwa picha zake, mbili zilizo maarufu zaidi duniani ni Mona Lisa na Karamu ya mwisho.

Mchoro mwingine unaojulikana sana ni Vitruvian Man. Unajulikana sana hata Homer Simpson na Garfield ambazo zilichorwa kwa mraba na mzunguko ili kuonekana kama mchoro.
Leonardo alizaliwa tarehe 15 Aprili 1452, mkoani Toscana, katika mji mdogo wa kilimani wa Vinci, katika mabonde ya Mto Arno, karibu na Florence nchini Italia.

Babu yake, Ser Antonio, anajivunia kwa kuweka kumbukumbu ya maelezo. Wazazi wa Leonardo walikuwa hawajaoana. Baba yake alikuwa mwanasheria, Messer Piero Fruosino di Antonio da Vinci.[3][4] Mama yake, Caterina, alikuwa mhudumu. Yawezekana alikuwa mtumwa kutoka Mashariki ya Kati.[5][6] Jina kamili la Leonardo lilikuwa "Leonardo di ser Piero da Vinci", ambalo lina manaa ya "Leonardo, mtoto wa Bwana Piero kutoka Vinci".

Leonardo alitumia miaka yake mitano ya awali akiishi katika nyumba ya shambani na mama yake. Halafu akaja kuishi Vinci na baba yake, mke wa baba yake aliyeitwa Albiera, mabibi/mababu zake na wajomba zake, Francesco.

Wakati Leonardo ameshakua, aliandika vitu viwili tu kuhusu maisha yake ya utotoni. Alikumbuka kwamba alivyokuwa amelala kwenye kitanda chake cha watoto nje ya nyumba yao ndege mkubwa alikuwa akipaa na kumzungukazunguka juu yake. Mikia yake ikawa inamfutafuta sura yake.[7] Kumbukumbu nyingine muhimu ya Leonardo ilikuwa vipi aligundua pango milimani wakati anapeleleza. Alikuwa na hofu kubwa sana huenda kukawa na kiumbe kikubwa cha ajabu kimejificha mle ndani ya pango. Lakini pia alikuwa na hamu na shauku ya kujua kilichopo mle ndani.

Giorgio Vasari aliandika kuhusu maisha ya Leonardo kwa ufupi baada ya kifo chake. Ameelezea hadithi za kuvutia kibao kuhusu utundu aliokuwa nao Leonardo. Anasema kwamba Leonardo alichora bamba la taarifa la mbao-mzunguko likiwa na picha ya mijoka inayotema moto. Messer Piero alichukua michoro ya mwanawe hadi Florence na kuiuza kwa wauzaji wa bidhaa za kisanaa
Leonardo alianza kuchora tangu yungali bado kijana. Alifunzwa usanii na mchongaji na mchoraji Verrocchio.

Sehemu kubwa ya maisha yake alimtumikia tajiri mmoja maarufu wa Italia.

Mwaka 1516 Leonardo alikwenda Amboise, Ufaransa, baada ya kupata mwaliko kutoka kwa mfalme Fransisko I. Kati ya mizigo aliyosafiri nayo ulikuwemo mchoro maarufu wa Monalisa.

Leonardo aliishi mjini Amboise, katika nyumba yake nzuri aliyopewa na Mfalme huyo wa Ufaransa, miaka yake ya mwisho, toka mwaka huo mpaka mwaka 1519.

Afya yake haikuwa nzuri kwa sababu alipatwa na ugonjwa wa kiharusi toka mwaka 1517, lakini taarifa za ugonjwa wake zikatolewa wiki chache kabla ya kifo chake.
Alifariki huko Amboise tarehe 2 Mei 1519 akiwa na umri wa miaka 67, akazikwa St. Hubert.
 
Lete mambo mkuu
 
Jina kamili la Leonardo lilikuwa "Leonardo di Ser Piero da Vinci", ambalo lina maana ya "Leonardo, mtoto wa Bwana Piero kutoka Vinci".
------------------------------------------------
Nimependa sana utambulisho wa aina hii, kwa nini haukuendelea hadi sasa, mfano:
Mimi ningeitwa "bdo, mtoto wa Bwana Mbuya kutoka Matepwende - Namtumbo".

Hapa ndio tungefahamiana ni akina nani wanaume wa Dar, Arachuga, Chato, ama Pemba.

Hahahahhahah
 
Dah mkuu una macho mangapi mbona mimi naona sura moja tu
 
Mkuu, Da Vinci Code ni fiction, not factual.
Hiyo fiction vipi,mbn ROMA kinawapa stress,na kwanini kipigwe marufuku pale kama hakina ukweli mwingi,acheni kuamini mambo ya upande mmoja,jitahidi kuyajua mengi mno kadri uwezavyo na iwezekanvyo,then choose your own way,acha uvivu na uwoga wa maarifa,DA VINCI CODE IS MORE THAN A GREATEST NOVEL mkuu!

Sent from my TECNO-Y6 using JamiiForums mobile app
 
Last supper,kna nyingine,,,,madona of the rock
 
Kuwapa Roma stress na kupigwa marufuku hakumaanishi kwamba ni factual. Kuna vitabu vingapi ambavyo ni fiction na vimepigwa marufuku sehemu mbali mbali? Mfano mzuri ni "the satanic verses".
 
Na hapo chini umejijibu mwenyewe. DA VINCI CODE NI NOVEL.
 
Ukirudi Fanya kuanzisha Uzi maana nina shahuku yakufahamu
 
Unajua kuzaliwa/kutokea kwa Leonardo da Vinci kulikuaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…