Naomba kufahamishwa, utamaduni wa kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa viongozi waliokwishafariki ulianzia wapi?

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Kufuatia maandalizi ya maadhimisho ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa baba wa taifa la tz, hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere, naomba kufahamishwa kama kumewahi kuwa na desturi au utamaduni kwa jamii za kiafrika; kusherehekea siku za kuzaliwa kwa viongozi waliotangulia mbele za haki au hata kwa ndg na jamaa!

Je, sherehe hizo bajeti yake inatoka kwenye fungu gani? Zina umuhimu gani?
 
Nadhani ni utamaduni wa huko ughaibuni kama dini za sasa zilivyofanya tukaziiga,hivyo pia hata bethidei nazo hivyohivyo.Tupo kizungu zaidi.
 
Nasherehekeaje kuja uchi duniani badala ya kusherehekea mwaka huu hadi ujao nimeshakuwa nguzo kuu ya msaada kwa Ndugu, Rafiki na Jamaa kwa kuwa mfano bora wa kuigwa uwajibikaji bora kifamilia, kijamii, kidini, kibiashara, kielimu, kikazi?

Au hata kuwa na kampuni yenye watu hata 100 baada ya miaka mitano ambao watakuwa wamenufaika kupata vipato vya kugharamia familia zao na kukuza uchumi wa Taifa?

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Kufuatia maandalizi ya maadhimisho ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa baba wa taifa la tz, hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere, naomba kufahamishwa kama kumewahi kuwa na desturi au utamaduni kwa jamii za kiafrika; kusherehekea siku za kuzaliwa kwa viongozi waliotangulia mbele za haki au hata kwa ndg na jamaa!

Je, sherehe hizo bajeti yake inatoka kwenye fungu gani? Zina umuhimu gani?
Upande mmoja Ni fursa ya kupiga pesa ya Nchi na kwa upande wa pili ni kuendeleza unafique na uzandiki wa wanasiasa wetu.

Kuna viongozi wameshaweka mashada mengi ya maua kwenye kaburi la Nyerere na Karume, ilhali huenda hawajawahi kuweka hata moja kwenye makaburi ya wazazi wao!
 
Kufuatia maandalizi ya maadhimisho ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa baba wa taifa la tz, hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere, naomba kufahamishwa kama kumewahi kuwa na desturi au utamaduni kwa jamii za kiafrika; kusherehekea siku za kuzaliwa kwa viongozi waliotangulia mbele za haki au hata kwa ndg na jamaa!

Je, sherehe hizo bajeti yake inatoka kwenye fungu gani? Zina umuhimu gani?
Huoni kwamba hiki ni kitu special? Baba wa taifa miaka mia ni kitu special.
 
Ughaibuni wapi ambao huwa wanasherekea kumbukumbu za aina hiyo?
Nadhani ni utamaduni wa huko ughaibuni kama dini za sasa zilivyofanya tukaziiga,hivyo pia hata bethidei nazo hivyohivyo.Tupo kizungu zaidi.
 
Kufuatia maandalizi ya maadhimisho ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa baba wa taifa la tz, hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere, naomba kufahamishwa kama kumewahi kuwa na desturi au utamaduni kwa jamii za kiafrika; kusherehekea siku za kuzaliwa kwa viongozi waliotangulia mbele za haki au hata kwa ndg na jamaa!

Je, sherehe hizo bajeti yake inatoka kwenye fungu gani? Zina umuhimu gani?
Ngoja na Muasisi wetu naye afaidi hela za tozo na zile za IMF. Naye anastahili kula kwa urefu wa kamba yake hata kama alishatutoka kitambo.

Wewe huoni yule jamaa aliyetokwa na jasho kwenye jua la saa 8 mchana wakati akienda kuomba msamaha baada ya kudukuliwa; leo hii anafanya utalii wa ndani nchi nzima kwa kutumia chopa ya jeshi?
 
Kazi kwelikweli
 
Haya mambo Birthday, kitchen party Valentine nk. hayakuwepo kwa waafrika sasa kumekucha...
Suala sio kuwepo au kutokuwepo mkuu.
Swali ni je, kuna tija yoyote kwa taifa?
Na je, ni utamaduni wa kiafrika kumfanyia 'birthday party' mtu aliyekwisha fariki???
 
Lanlady yote uliyoandika hapa napigilia nyundo kukuunga mkono kwa point hii chini.Nanukuu

''Je, sherehe hizo bajeti yake inatoka kwenye fungu gani? Zina umuhimu gani?''......................Lanlady
mwisho wa kunukuu
 
Back
Top Bottom