Naomba kufahamishwa utaratibu wa kufungua duka la dawa muhimu za binadamu

Naomba kufahamishwa utaratibu wa kufungua duka la dawa muhimu za binadamu

Travis_Kitengo

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2021
Posts
329
Reaction score
919

Habari, za wakati huu wana Jf,

Mimi kijana mwenzenu mpambanaji nimekuja hapa kuomba kufahamishwa utaratibu wa kufungua duka la dawa muhimu za binadamu (DLDM). Kitaalamu mimi ni afisa muuguzi II, mahali nilipo nimeona fursa ya kufungua duka la dawa muhimu ila tatizo sielewi utaratibu ukoje.

Naomba wenye hii biashara mje mnipe abc muhimu Mtanzania mwenzenu kama vile masuala ya vibali, mtaji wa kuanzia, kodi, aina ya dawa za kuuza, faida etc

Naomba kuwasilisha.
​
 
Uza dawa zote haramu , na zinazopigwa marufuku kwenye maduka ya dawa, tofauti na hapo utakuwa unasaidia jamii kupata pcm na panadol kwa ukaribu tu.
 
Lazima ukutani (pembezoni mwa milango ya duka lako) uandike 'DAWA MUHIMU ZA BINADAMU' kwa mwandiko wa kwenda chini yaani wima.

Hapo utakuwa umeshamaliza Kila kitu nadhani.
 
Kuna rafiki yangu alitaka kufungua Kuna taratibu alipewa baadhi naweza kushea na wewe
1. Vibali kutoka TFDA
2.Tin namba
3.mmliki wa duka hutakiwi uuze wewe ajili mtu akuuzie.
4.muuzaji lazma aende akasomee kozi ya phamasia ile ya miezi 2 sijui mitatu ada 400000
5.kuna umbali maalumu kutoka duka Moja la dawa lilipo na duka jingine
6.umbali kati ya zahanati/hospitali na unapotaka kufungua duka lilipo vinazingatiwa
7.chumba lazma kigawiwe mara mbili, kiwe na store,
8. Mambo ya TRA cjui
9. Mambo ni mengi sana. Hayo ni baadhi tu
 

Habari, za wakati huu wana Jf,

Mimi kijana mwenzenu mpambanaji nimekuja hapa kuomba kufahamishwa utaratibu wa kufungua duka la dawa muhimu za binadamu (DLDM). Kitaalamu mimi ni afisa muuguzi II, mahali nilipo nimeona fursa ya kufungua duka la dawa muhimu ila tatizo sielewi utaratibu ukoje.

Naomba wenye hii biashara mje mnipe abc muhimu Mtanzania mwenzenu kama vile masuala ya vibali, mtaji wa kuanzia, kodi, aina ya dawa za kuuza, faida etc

Naomba kuwasilisha.
​
Nenda kwa mfamasia mkuu wa wilaya atakupa muongozo sehemu gani ufungue hiyo dldm yako .

Ila kwa haraka haraka sehemu husika ya kufungua dldm lazima izingatie umbali kutoka dldm moja mpaka nyingine, umbali kutoka hospitali au zahanati nk.

Cheti cha pharmaceutical technician kinachotambulika, kuajiri mtu aliyesoma pharmaceutical technician.

Dawa zipi zinaruhusiwa kwenye dldm na zipi haziruhusiwi.

Makabati ya aluminium nk.
 
Back
Top Bottom