Naomba kufahamu kama hawa jamaa walikufa au walipona

Naomba kufahamu kama hawa jamaa walikufa au walipona

Huyu dereva wa hii truck
Ni kama alikuwa amechoka
Kingine naona kama breki zilifeli

Ova
No breki hazikufeli, kawaida gari manual kama hio canter ikiwa gia namba 5 na mwendo wa highway kusimama ni ngumu yani unatakiwa upangue gears chap ndio ukate speed, tofauti na automatics ukikata speed tu kwa breki gear zinavuka zenyewe haraka na gari inasimama hata kama ulikuwa 150km/h!

Huyo jamaa kafosi breki bila kupangua gears na hakuwa na jinsi zaidi ya kuchochola.
 
Kuna video inatrend jamaa wawili wako kwenye gari ndogo wanajirekodi video. Kufumba na kufumbua gari ya mbele yao inafunga break ghafla wanaipiga kwa nyumba hawaja kaa sawa dreva anataka kuitoa pembeni wanakutana na Basi uso kwa uso na wote wananyamaza kimya kwenye video. Je wamekufa?
Niliiona mpaka mwisho ila nilipoiriwaindi wakapona, kweli mungu mkuu.
 
Naona unaleta joke Sasa uliiona wapi live au na je uliriwaindi ongea Kama mwanaume uliyebalahe .
Habari yako inaanzia angani na inaishia angani, haielezi hiyo video uliiona wapi, lini na tukio ni la wapi.
JF ni ya GT's.
 
Hao jamaa hawakuwa wana ji record bro kuna camera nyuma yao kwenye cabin. Dereva ni mpuuzi sana huyo.

Kwanza anafuata gari inayo overtake kwa nyuma karibu kabisa halafu eneo lisiloruhusiwa ku overtake (angalia kuna kama daraja hapo). Unawezaje kufuata mtu nyuma hivyo na huoni huko mbele kuna kitu gani?

Halafu hata distance aliyokuwa akimfata ni ndogo sana ndio maana wa mbele alipo break tu yeye kashindwa kusimama kwasababu alikuwa karibu sana.

Ajali nyingi baranarani ni za uzembe wa madereva wasiojua defensive driving.
 
Hii kitu mbaya sana, ishawi kutukuta wakati tunasafirisha msiba, dereva alifuata iveco iliyokuwa imebeba maiti vile iveco inamaliza kuover take lori sie tupo ubavuni, hamadi fuso hiyo. Dereva wetu wa Coaster alikula chocho sema gari ilipaa na kwenda kutua kwenye migomba na ndio kilichosaidia. Bahati nzuri gari haikupinduka na wala hakuna aliyeumia. Hapo ndo niliona Ukuu wa Mungu!!!!
 
Wewe ndio juma kilaza umeshindwa kuelewa kwamba nimeuliza swali.
Tanzania kuna shida moja. Watumiaji wa soacial media wengi kazi yao ni ku-post au ku-share picha au clip ambazo hazina maelezo yoyote. Clip kama hii kupata ukweli wake inaweza kuwa vigumu kabisa.
 
Tanzania kuna shida moja. Watumiaji wa soacial media wengi kazi yao ni ku-post au ku-share picha au clip ambazo hazina maelezo yoyote. Clip kama hii kupata ukweli wake inaweza kuwa vigumu kabisa.
wewe kama hujui inabidi ukae pembeni kuna ambao wameiona watajibu
 
wewe kama hujui inabidi ukae pembeni kuna ambao wameiona watajibu
Ndiyo maana nikasema ni vigumu, na wakati mwingine jibu utakalopata ni uongo unaotokana na uvumi. Utasikia ''nasikia walikufa wote''. Mwingine anasema ''mbona wala hawakuumia!''. NB: Fikiria kabla ya kubwabwaja. Hii ni forum na kila mtu anatoa mchango wake ili kupanua mjadala na mawazo. Kutojua kilichowapata hakufanyi mtu asichangie. Mbona wewe umechangia na huna jibu?
 
Back
Top Bottom