Habari wataalam wa ujenzi?
Naomba kufahamu makadirio ya bati na mbao ambazo nitatumia kuezeka nyumba hii ya vyumba vyumba vitatu vya kulala, sebule, dining, stoo na choo cha public. Vipimo ni 11m x 9m. Kwasasa nimeshafunga linta.
BATI (92pcs)
No of Sheet = (11×9)÷(0.6×2.7)×1.5 = 92 sheets
Twende kwenye uhalisia kuproove
Tuassume nyumba yako haina kona kona hivyo tunapaua kwa mgongo wa tembo
Kama utatumia angle ya 45, king post itakuwa ni nusu ya urefu wa tie beam.
Kingpost = 0.5×9= 4.5m
Rafter = sqrt(4.5²+4.5²)= 6.3m+ Overhang (0.3m)= 6.6m
Idadi ya bati per roofing line = (11m+Overhang (0.4×2))/0.6 = 19.6 (approx 20)
Katika 6.6m zinaingia bati 2 na kubaki uwazi wa 1m
Jumla ya bati nzima = 2x20x2 = bati 80 (pande zote mbili)
Bati moja vinaingia vipande vya 1m vitatu, na jumla vinahitajika vipande 40 (20 upande mmoja, 20 upande mwingine)
Jumla ya bati za kuziba vipande = 40/3 = 13.3
JUMLA = 80+13 = Bati 93
MBAO 2×4 (125pcs), MBAO 2x2 (40pcs)
Idadi ya kench = (11m/1.2m)+1 = 10
Kench moja huwa inatumia mbao mara 5 ya urefu wa tie beam
So idadi ya mbao (2×4) = (10x5x9)/3.6 = 125
Mbao za 2x2 = (11m+0.4mx2)×6×2/3.6= 39.3 (Approx 40)
MISUMARI YA BATI 15PKT
No of pkt = (92 /6)= 15
Summary
Bati 92pcs to 94pcs
Mbao 2x4 125pcs
Mbao 2x2 40pcs
Misumari ya bati 15 pakt