Naomba kufahamu tabia za wanyakyusa

Hapo kwenye kazi kupeana kindugu umegusa penyewe huwa wana umimi

Mimi miongoni mwa makabila nilichanganyia upande wa mama unyakyusa upo na nina jina la huko

Na nasema ukweli kuna kazi ambazo nilishawahi kufanya nilizipata kwa sababu ya jina .. kwenye interview Kama wapo kwenye panel na kwakua hawa watu ni wasomi hivyo wana nafasi za juu ukiitwa jina wanajua huyu ni wa nyumbani tayari umepita kwanza badala ya kukuuliza maswali ya interview utaskia unatoka mbeya sehemu gani na mimi siwezi kukana kwamba mimi sio mnyakyusa labda ni mzaramo au mndengereko mwenye jina la kinyakyusa nilolitoa kwa mama no way na mbeya kwenyewe sipajua basi nakubali naenda na flow nisokose fursa [emoji1787]
 
Kwenye kile kipindi cha Matukio cha Redio Free asilimia kubwa ya matukio yalikua yanatoka mbeya. Mara mtu kachunwa ngozi mara mtu kunyonywa damu😅
 
Kuna mzungu mmoja ni pastor huku chuga alikuja dukani nilikua niko nam -Close Up mdada fulani wa kizungu nipate japo namba huyu pastor aliniharibia aisee. Anaongea kimasai balaa na kiswahili kama cha hao machalii wa Ngarero na ngalimited utadhani ni mmasai kabisa. I real need some copious details kuhusu wanyaki nami niwe mnyaki
 
Inawezekana jina lako hasa la ukoo / ubini linaanza na Mwa. Hata mimi watu wengi huniambia ni mchaga na kiuhalisia sio mchaga
Oya upo mbalizi sehem gani tarafani,iwambi,au kule karibu na Wenda,maana mbalizi kubwa kweli
Umenikumbusha kitambo kweli tupo Kwa shule tunaluka ukuta tunakimbilia tarafani kununua chipsi za jero jero nimepamis sana mbalizi
 
Waaminifu mno,wajasiri sana na Wasiri sana na wachagpa kazi sana na wana msimamo ndio maana majeshini wanapendwa sana na sehemu za post nyeti

Mbeya wameshatoa wakuu wa majeshi tofauti kibao kuanzia usalama wa taifa,JWTZ,Polisi na magereza
 
Beesmom niwahi tall and dark jf nimebaki mimi tu😅🏃🏃
Nawapenda sana aina nyie ila tatizo mapenzi yalishanikifu mkuu....we huoni ninavyochezea vichwa vya watu humu....naburudika kufanya Ivo Lakini moto wa kuwa na Mpenz sina....hata Ivo mwisho wa siku tunazikwa.Nayachukia mapenzi kiukweli
 
Nataka nijifunze kua mnyaki aisee inawezekana nikapata fursa nyingi. Ajitolee mmoja anifunze.
 
Wanyaki sio wachoyo kweny vyakula Ile mijamaa Haina dhiki za vyakula kabisa miviazi,miparachi,mindizi,miwali Yani kwao imejazana tu sema shida Yao moja wanajikubali sana ila kabila lao ni moja kati ya makabila yenye wanawake wenyeheshima na kufanya kazi Kwa bidii
 
Inabidi upewe dada wa Kinyakyusa awe trainer wako utachagua Ikupa,Bupe,Tusekile,Atuganile,Gwantwa au Negwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…