Naomba kuijua biashara mtandaoni ya Gwac, nasikia watu wengi wamejiunga

Naomba kuijua biashara mtandaoni ya Gwac, nasikia watu wengi wamejiunga

PAZIA 3

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
1,102
Reaction score
1,919
Habari za Leo?

Jamani, nimeshirikishwa fursa na mtu mmoja, anasema, Kuna biashara mtandao inaitwa Governmentwide Acquisition Contract (GWAC).

Watu wanawekeza pesa na ukishawekeza baada ya siku moja, unaanza kurudishiwa asilimia 10 ya pesa uliyowekeza kila siku mfululizo kwa mwaka mzima.

Tayari kuna watu wananufaika nayo, ikiwemo huyo aliyenishirikisha. Yeye amewekeza laki 3, maana yake anarudishiwa elf 30 kila siku, Leo anaingia siku ya 5. Uhakika wa kudumu kwa kampuni hii haujulikani, lakini Kuna watu wamesharudisha mitaji Yao Sasa wanalipwa faida zaidi.

Swali langu nikwenu, mmeshaisikia hii fursa?
 
Mimi ndo kwanza naiskia kwako!

Unapewa asilimia 10 ya Pesa kila siku?

Kampuni inapataje faida Sasa?
Haya ndiyo maswali najiuliza pia, lakini mpaka Sasa huyu mtu na jamaa zake wengine wamelipwa zaidi ya siku 10, maana yake wamesharudisha mitaji Yao, lakini bado wanaendelea kulipwa asilimia 10 zao🤔🙌
 
Mkuu mwambie jamaa yako atume link humu tufaidi mema ya nchi..TUPO TAYARI KUTAPELIWA KWA MOYO MMOJA
 
hzo kampuni zipo hzi kampuni huwa zipo ulaya sema wanazuia zisitoke nje ya ulaya sasa kuna wahuni huwa wanafanya manyanga wanazileta huku africa kinyemela , wanaojiunga wa kwanza kwanza wanapiga hela ila baada ya mda mchezo wakiustukia wanapigwa ban ndo unaskia kampuni imekufa , kilochopo ni kujilipua tuu ila ujue kabisa inaweza dumu sku 10 , mwez , au mwaka .,.. sku ikifa huna pa kulalamika high risk high gain
 
Na wewe ukakubali kabisa baada ya kuambiwa hiyo biashara mtandaoni?unamiaka mingapi?
 
Biashara ya pesa huwa haitwi mtu ila inatokea gafla bin vuu, umezama.

Ila hizi za kupigiwa simu, unaitwa ili wewe ukawe deal!.
 
We ni
FB_IMG_17365466209773502.jpg
 
Wale waanzao ndo wanaofaidii .... hizi biashara za rahisi rahisi hazijawahi mwacha mtu salaamaaa
 
Habari za Leo?
Jamani, nimeshirikishwa fursa na mtu mmoja, anasema, Kuna biashara mtandao inaitwa GWAC.
Watu wanawekeza pesa na ukishawekeza baada ya siku moja, unaanza kurudishiwa asilimia 10 ya pesa uliyowekeza kila siku mfululizo kwa mwaka mzima. Tayari kuna watu wananufaika nayo, ikiwemo huyo aliyenishirikisha. Yeye amewekeza laki 3, maana yake anarudishiwa elf 30 kila siku, Leo anaingia siku ya 5. Uhakika wa kudumu kwa kampuni hii haujulikani, lakini Kuna watu wamesharudisha mitaji Yao Sasa wanalipwa faida zaidi.
Swali langu nikwenu, mmeshaisikia hii fursa?
Hizo fursa ni nzuri sana ila jitahidi ufanye tafiti imeanza lini maana nyingi huwa zina duration ya mwaka mmoja au zaidi....wa kwanza kula wa mwisho huliwa.
 
Habari za Leo?
Jamani, nimeshirikishwa fursa na mtu mmoja, anasema, Kuna biashara mtandao inaitwa GWAC.
Watu wanawekeza pesa na ukishawekeza baada ya siku moja, unaanza kurudishiwa asilimia 10 ya pesa uliyowekeza kila siku mfululizo kwa mwaka mzima. Tayari kuna watu wananufaika nayo, ikiwemo huyo aliyenishirikisha. Yeye amewekeza laki 3, maana yake anarudishiwa elf 30 kila siku, Leo anaingia siku ya 5. Uhakika wa kudumu kwa kampuni hii haujulikani, lakini Kuna watu wamesharudisha mitaji Yao Sasa wanalipwa faida zaidi.
Swali langu nikwenu, mmeshaisikia hii fursa?
Jichanganye
 
Mpaka naileta hapa hii issue, maana yake Mimi mwenyewe siamini. Lakini haiondoi ukweli kwamba, mpaka sasa waliojiunga, wanalipwa kabisa. Nimependa comments za baadhi ya wadau wanaosema, issues kama hizi, huwa zipo nchi za wenzetu lakini huku zinaingizwa kinyemela. Siku wakistuka waanzilisha, wanafunga biashara hiyo au link hiyo, kwahiyo, watakaoathirika ni wateja wapya watakaokuwa na muda mfupi tangu kujiunga na kufungwa Kwa hiyo link
 
  • Thanks
Reactions: apk
10% Kila siku?

Ukiweka milioni Kwa mwaka unapata 36.5M

Badae mtakuja kulaumu serikali mmetapeliwa, Hawa watu ningekua na uwezo siku ya kuja kulalamika unawaweka wote sehemu Moja unawacharaza viboko
 
Back
Top Bottom