Kuna mambo ambayo kupata ukweli wake dunia hii ni kazi sana. Ila ufahamu wa HIV katika jamii zetu hasa za kiafrika, siyo suala la kusoma kwenye vitabu vya watu wanaoishi New York, wengi wameona ndugu, wazazi, watoto etc wakiteketea taratibu. Naamini hata jukwaani lazima kutakuwa na baadhi ya waliojionea hayo au pengine wengine wanaumwa pia, hivyo ukisema HIV ni fix watu wataokota mawe. Kikubwa tuanze kuboresha mifumo yetu ya elimu ili tuweze kutengeneza dawa zetu za kujitibu, na pia tushutumu mataifa makubwa kwa kufanya biashara katika afya za watu, corona iliwaua wengi angalia walivyochakarika kutafuta kinga. Wangeamua siku nyingi ungekuta HIV ni historia.