COLD WAR: PHASE 2- Stalin's Russia.
Vladmir Illyich Lenin kiongozi wa kwanza wa USSR alikufa mwaka 1924. Ikumbukwe aliukuwa anaumwa kisukari na alishanusurika na vifo vya risasi mara mbili tofauti hivyo kupelekea afya yake kuzorota hadi kufa.
Lenin alipenda arithiwe na Leon Trotsky ambaye alikuwa ni rafiki yake wa karibu na ndiye aliyetengeneza muundo wa jeshi la Urusi The Red Army pamoja mifumo ya kiintelijensia kipindi hicho ambayo ilikuwa ni The Cheka baadae uliitwa OGPU,NKVD,NKGB,KGB ambao saa hizi inaitwa FSB na SVR. Pia alisaidia sana kutengenezwa kwa chombo cha kijeshi cha upelelezi (Military Intelligence) ambacho mpaka leo hii kipo kinaitwa The GRU.
Leon Trotsky alikuwa ni Myahudi na kipindi hicho wayahudi wengi walikuwa wanatengwa sana Urusi. Hivyo Stalin pamoja na genge lake waliwawahi wakina Trotsky na kundi lake hivyo Joseph Dhughashili A.K.A Comrade Joseph Stalin akawa kiongozi wa Urusi.
Stalin alitofautiana na Lenin na Trotsky katika kusema Ukomunisti ni lazima uimarike kwanza USSR kisha Upelekwe katika mataifa mengine.
Katika hili Stalin alikuwa sahihi kwasababu bila kufanya hivyo Urusi isingeweza kushinda vita ya pili ya Dunia na umoja ungekuwa umesambaratika mapema.
Stalin alianza FIVE YEARS PROGRAM ambapo alianza kuimarisha Uchumi wa Urusi kwa ajili ya kutawala dunia. Aliongeza kasi ya watu kupata elimu hasa aliwekeza sana katika Upelelezi wa Kiviwanda unaoitwa CORPORATE ESPIONAGE na Military Intelligence. Katika haya majaribio ya kipelelezi Moscow iliweza kupandikiza Majasusi wengi Ulaya, Asia na Marekani.
Ikumbukwe baada ya mapinduzi ya Urusi kulikuwa na wimbi kubwa la wakimbizi kutoka Urusi kuelekea mataifa mbalimbali ya Ulaya. Hivyo walipokelewa vizuri na kupewa Uraia wa Marekani, Uingereza, Ufaransa, Hispania, Ujerumani, China na mataifa mengi.
Moscow ilitimia mwanya huu kupenyeza majasusi katika nchi za Magharibi hasa katika Viwanda, majeshi na serikali. Hawa wanaitwa SLEEPER AGENTS ambao wao kazi yao ilikuja kuonekana wakati wa vita ya pili ya dunia na baada yake.
Mataifa ya Magharibi yaliupuuzia umoja wa nchi za Kisovieti kwasababu ulikuwa ni maskini sana kiuchumi na mbaya zaidi mwaka 1919 Urusi walishindwa vita na Nchi ya Finland hivyo ikawa ni aibu.
Huku nyumbani Stalin alitengeneza kitu kinachoitwa A Closed Society, ambapo mfumo wa kijasusi wa Urusi ulikuwa katika kila kona na kila kitongoji. Kuanzia walimu, wanafunzi, wanajeshi, airport, walinzi wa mipaka,raia wa kawaida na nk.
Stalin alisaini mkataba unaoitwa THE CONCORDE AGREEMENT ambao uliwazuia vijana wa Urusi chini ya miaka ya 40 wasitoke nje ya URUSI; hii ilisaidia sana kuzuia influence ya magharibi nchini Urusi lakini pia ilikuwa inapunguza maendeleo ya kasi nchini humo kwasababu haukuwa unasaidia innovation na biashara.
End of Phase two; stay tuned for phase 3