Katika dini yetu ya budha (budhisim) kuna mambo makuu mawili.
1. Samsara
Hii ni imani kuwa kuna maisha baada ya kifo, wazungu waita (life after death) kwamba unapofariki utazaliwa sehemu nyingine kama mwanadamu au kiumbe kingine kutegemeana na karma yako, soma karma chini ujue ni nini.
2. Karma
Hii inamaanisha ni malipo utayopata baada ya kufa. Mfano ulikua mtu mwema na mtoa msaada kwa wasio na kitu hata kama ulikua huna uwezo sana basi ukifa utazaliwa katika hali nzuri sana. Unaweza ukazaliwa ukawa tajiri sana na mtu mwenye mafanikio makubwa.
Hivyo basi samsara huwa determined na karma yako, kama ulikua tajiri na kuwadharau maskini hukawii kuzaliwa mbwa koko hapo baadae. Budhisim ni imani moja tamu sana