MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,016
- 16,813
Dalili zote unaonyesha upo katika Kundi la Wagonjwa wa Akili na unahitaji Tiba ya haraka sana.Naomba kwa wataalamu humu mniambie Mimi ni mtu wa Aina gani kwa izi sifa zangu;
- Mimi ni mkorofi (tokea utotoni napenda Sana ugomvi na sehemu zenye ugomvi na shari)
- Mimi ni mkimya (yaani sipendi kuongea na pia sipendi mtu aniongeleshe kwa muda mrefu nachukia sana yaani natak nikiwa na wewe ukae kimya usiniulze maswali mengi)
- Ninapenda kampani au watu wasio wapole wapole yaani napenda watu waliochangamka(wahuni wahuni)
- Nayachukia mahusiano(ya kimapenzi) naweza kumtongoza msichana ila baada ya kukubali nkikaa nae kidogo nachoka na naachana nao.
- Mara nyingne Ni muongeaji Sana kwa watu nisiowajua ama ninaowajua ila wakati mwingne nakuwa mkimya Sana naweza maliza muda sijaongea na mtu
- Sinaga aibu.
- Napenda Sana kuishi/kukaa pekeangu pekeangu muda mwingne natamani dunia nzima ningebaki mwenyewe.
- Nina huruma Sana.
- Sipendi sehemu zenye starehe starehe (hii sjui kutokana na malezi) mf birthday party izi ama sehemu za kuchanganyika na watu, napenda Mambo ya fujofujo.
- Nikimbembeleza mtu au mpenzi wangu roho inaniuma Sana najiona Kama sjui Nini yaani kiufupi sipendi maswala ya kubembelezana (ata Mimi sipendi kubembelezwa.
- Napenda Sana uadui na pia kuwa kwenye mazingira magumu(waga ninakuwaga na mawazo Sana ) na bila kuwa na mawazo sifanyagi vitu vizuri(malezi nilokulia).
- Sipendi kufatilia mtu na Mimi sipendi kufatiliwa Mambo yangu.
- Story zangu waga haziko romantic napenda story za matukio matukio ya ajabu na ya kiume sinaga story za kuvutia za mapenzi
Hayo ni machache tu, je me ni mtu wa aina gani maana yake nashindwa kuelewa! Msaada tafadhali🙏
Tatizo lilianza miaka mingi iliyopita baada ya wazazi kutengana Sasa mimi sikujua majirani walikuwa na shida gani na mamangu lakini hawakunionyesha uungwana ata kidogo walinitenga Sana ata kuingia majumbani mwao ilikuwa shida walinizuia ama wakiniruhusu waliniweka pekeangu chini Apo ndo mwanzo wangu wa kuanza kujitenga ila nilitamani kukaa na watuBro, pole sana
Kwa maelezo yako unashida ya akili yaani mental illness,
Kama hutojali tutajie tatizo lilianza lini , sasa hivi una umri gani?
Uliwahi kuwa na tabia ya kubishana na mzazi,walimu au wakubwa zako? Wakati wa utoto ulikuwa ukipigana na wenzio mara kwa mara shuleni?
Umri Ni 20,s, wewe umeweza kunijua zamani nilinyanyaswa Sana kuanzia level ya familia mpk mtaani kwaivyo niliona Mimi si kitu make mtu akinifanya kitu Sina pa kwenda kushtaki ivyo nilijitahidi kupambna mwenyewe ata watu wazima waliponionea nilijaribu kulipiza kisasi na Kama akinikamata kwa Mara ya pili na Mimi nililipiza kwa kuharibu kitu chake Cha maana nayeye haumie kama Mimi.Kwa maelezo yako,wewe utakuwa
1. Kijana wa kiume
2. Umri wako ni kati ya miaka 22-32
3. Kuna matatizo ya kisaikolojia unayo baada ya aidha kunyanyaswa utotoni kwa kuonewa, kunajisiwa, kupigwa au kuteswa. Hivyo una hasira ya ndani kwa ndani kwa uliyotendewa
4. Kiasili wewe ni mtu mpole, lakin kutokana na uliyotendewa utotoni unaona kama kuwa 'mpole' ni unyonge, au kutulia ni uoga. Hivyo unapenda 'ujipapatue' kuwa wewe si mnyonge tena na ni 'mpambanaji' hiyo inapelekea wewe kuwa mkorofi.
5. Una restlessness na upweke ndani yako ambayo inakufanya upende uwe kwenye mikusanyiko ya watu na kwenye kelele. Ili kukufanya usiyawaze yaliyokupata huko siku za nyuma.
Kwa kuhitimisha you are troubled person deep inside. Una matatizo ya kisaikolojia. Inawezekana ulikuwaga bullied ulipokuwa mdogo. Ndo maana unashindwa kujitambua wewe ni nani. Maana wewe deep inside ni mtu mzuri, lakin uliyopitia yamekufanya uwe mkorofi ili usiwe mnyonge tena.
Pole sana mkuu, tafuta muda uende hospital yoyote ya magonjwa ya akili.Tatizo lilianza miaka mingi iliyopita baada ya wazazi kutengana Sasa mimi sikujua majirani walikuwa na shida
Kwa kweli huyu anapaswa kuwa milembeMaelezo yako yanaenda mbele na kurudi nyuma.
Ww ni mpole mara hapohapo ni mkorofi. Hapohapo una huruma huku unapenda ugomvi. Hapo hapo hupendi kuongea mara huwa unaongea.
Labda tu niseme ww ni kichaa.
Shukrani mkuu nitafanyia kazi ushauri wakoPole sana mkuu, tafuta muda uende hospital yoyote ya magonjwa ya akili.
Kwa maelezo yako machache ulipokuwa utotoni ulikuwa unaelekea kupata(au ulipata) baadhi ya mgonjwa ya disruptive impulse-control and conduct disorders. Ambayo baadhi yake huwa yanaishia kumfanya mtu awe psychopathy ukubwani.
Nenda hospital utafanikiwa kwa sababu tayari ushajua tatizo lako
Sasa hapo Mwamba tulia..ya zamani yamepita. Sasa hivi wewe ni dume,na kwa uliyoyapitia umeshakomaa kwelikweli. Hakuna mtu anaweza kukufanya kitu chochote.Umri Ni 20,s, wewe umeweza kunijua zamani nilinyanyaswa Sana kuanzia level ya familia mpk mtaani kwaivyo niliona Mimi si kitu make mtu akinifanya kitu Sina pa kwenda kushtaki ivyo nilijitahidi kupambna mwenyewe ata watu wazima waliponionea nilijaribu kulipiza kisasi na Kama akinikamata kwa Mara ya pili na Mimi nililipiza kwa kuharibu kitu chake Cha maana nayeye haumie kama Mimi.
Nishawai pia kuishi mtaani & kulala kwenye majengo mabovu na vibanda
Siku za nyuma pia nilishajaribu kujiua
Ayo machache mengine ukitaka pia ntaeleza naomba msaada wa mawazo ya Nini Cha kufanya
Wewe ni mtu mzuri tu huna shida yoyote. Tulia sasa ujipange upya kimaisha. Jitahid pia kulala mapema na kupata usingizi wa utulivu wa muda mrefu. Kunywa maji mengi na urelax...mambo yatakuwa sawa tu kakaYa kiufupi Mimi sijijui Sina tabia permanent ila ninahisi huruma ndo tabia yangu ya asili
Pia puuzia humu wengine wanaokuita majina ya ajabu kama kichaa, mwehu, mwendawazimu nk. Wengi wao wanaokuita hivyo wao ndo vichaa. Tena kama humu JF yamejaa machizi. Unaweza shangaa mtu anakutukana bila sababu. Achana nao. Ukiweza pata muda unaweza kwenda kumtafuta mtaalamu wa mambo ya saikolojia mkae nae mzungumzeShukrani mkuu nitafanyia kazi ushauri wako
Duuuh hii hali imewakumba wengi sana abusive....usijione uko peke yakoTatizo lilianza miaka mingi iliyopita baada ya wazazi kutengana Sasa mimi sikujua majirani walikuwa na shida gani na mamangu lakini hawakunionyesha uungwana ata kidogo walinitenga Sana ata kuingia majumbani mwao ilikuwa shida walinizuia ama wakiniruhusu waliniweka pekeangu chini Apo ndo mwanzo wangu wa kuanza kujitenga ila nilitamani kukaa na watu
Tabia ya kubishana na wazazi na wakubwa ilianza miaka ya baadae kidogo na sikuishia kubishana nao ata kupigana nao ingali nilikuwa mdogo hii ilitokana na tabia ya wao kupenda kunipiga piga ovyo
Mashuleni na mtaani Hali ilikuwa ivo ivo(siyo walimu Wala wanafunzi nilipigana nao) ile Hali ya kutengwa tengwa ilikaa akilini na nilikuwa najihisi Mimi sina faida yoyote kwa mtu yyte na ata mtu akinialika kwenda kwao au kwenye sherehe yoyote sikwenda niliona Hawa wanaenda kunitenga
Yapo mengi Sana ila ayo Ni machache zaidi ukitaka mengine ntaongeza.
Mkuu Wyatt hapa sijaelewa[emoji23][emoji23]
Wewe unahitaji amaombezi kupitia mchungaji au shehe. Hilo litakuwa pepo mkuu.Naomba kwa wataalamu humu mniambie Mimi ni mtu wa Aina gani kwa izi sifa zangu;
- Mimi ni mkorofi (tokea utotoni napenda Sana ugomvi na sehemu zenye ugomvi na shari)
🙏
Nimejitahidi Sana kusahau yaliyopita ila yanakuja automatic yenyewe yaani saiv matendo ya zamani kwa asilimia kubwa nimeacha ila Sasa saiv ndo naona kabisa nachanganyikiwa yaani Kuna muda nakuwa Kama chizi sjui kwanini Hali hi naipata.Duuuh hii hali imewakumba wengi sana abusive....usijione uko peke yangu
Kikubwa piga chini past..deal na present na future, badilisha fikra hii itakusaidia sana mkuu, pole