Naomba kujua Nyumba zinazonukia, Wanafanyaje?

Ukifika Ukerewe utashangaa na roho yako,unakijua kibambala?kikipikwa hcho kinanukia shombo humo ndani wiki tisa[emoji16]
 
Kwanza hakikosha usafi wa nyumba yako ni wa hali ya juu.
Pili,nyumba isiwe na vitu vingi. Vitu vingi vinanyima hewa kuingia na kutoka.
Tatu,tumia air freshener. Ziko za kuspray na ziko za umeme ambazo unazitundika na kuzicontrol jinsi utakavyo.
 


Kuna huu mshumaa


Halafu kuna hivi vijiti ambayo vinatema tu harufu nzuri sana ya manukato 24/7.

Hivi vijiti vyaitwa "seagrass diffusers".

 
Lengo la kutaka nyumba kunukia (tofauti na uhalisia wake) huwa ni nini? Je ni kuficha harufu mbaya(ya uchafu)? Kama kuna uchafu unatoa harufu mbaya si ni bora kuutoa huo uchafu?
 

Hahaa.... Wale samaki wa Oriental ukiwa kaangia ndani harufu ni wiki nzima aisee!
 
Mkuu air freshener pekee haifanyi nyumba kunukia kihivyo. Wengi hutumia vyetezo na kuchomea kwa manukato ya kiarabu nenda kwenye maduka ya kiarabu ulizia utazipata. Kwenye gari mimi hutumia air freshener za kijapan inaitwa JDM.
 
Acha kabisa aisee.

Bora kuwapikia nje huko.

Kuna M-Nigeria mmoja yeye lunch yake samaki huwa hawakosekani! Basi akija job wakati wa lunch huwa anawapasha kwenye microwave, basi hiyo shombo watu huwa wanatamani kuondoka kwenye lunchroom![emoji3][emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…