Naomba kujua sababu ya gari kuchemsha (overheat)

Kuna "sabuni" ya kusafishia radiator kama hiyo, inaitwa "radiator-flush" kama hii


Mwaga maji yote, halafu maji haya kama lita mbili; usiwashe gari kwa kama saa moja hivi kususdi yale kutu yote, halafu washa injini kwa kama dakaika 20, kisha mwaga yote ndipo uweke coolant mpya.
 
Bado upo nje ya nchi?
Kuna gari kilikuu tata piston 2 inachemsha nimechek mfumo wa upozaji uko sawa nimechonga head na nimebadirisha gasket nimeweka namba2 bado inachemsha pump iko sawa timing iko sawa gari inawaka vizuri nipe mawazo yenu tatizo ni nini had bado inachemsha iyo engine ni overhead cam shaft
 
Unatumia maji ya Dawasco au coolant kwenye rejeta?
 
ukitumia maji ya kununua dukani hapo vipi??? coolant inauzwa sh ngapi dukani??
 
Baada ya kuchonga (resurfacing) head gasket, ulifanya any pessure test kwenye hiyo cylinder head kuangalia kama kuna leakage kwenye hizo valves?

Ku-resurface head pekee haitoshi, kwasababu kama cylinder head ilikuwa warped (injini kuchemsha), valves huwa hazikai vizuri tena kwenye lile tundu la mduara (valve seat). Hizi valveseat zinabadilika kuwa na umbo la yai na hivyo kusababisha leakage (compression loss, overheating - kuchemsha kwa injini).
 
Mkuu mimi gari yangu inatabia ya kujizima kwenye foleni,au ikiwa silencer,nimejaribu kupandisha silnce lkn bado tatizo lipo?service naw kila kitu kipo vizuri,tatizo nini?
Badili camshaft position sensor
 
Samahan bro. .gari yangu voxy ghafla imeanza kupunguza maji ingawa nikidogo kila asubuhi yanaenda kwenye reseve bottle. Tatizo nini. Pia ikifika spidi 100 alaf ukaachia mafuta ikifka 80 inakuwa inakatakata mafuta na siyo misi
Badili mfuniko wa rejetor huo ndio unakuletea tatizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…