Naomba kujua tofauti Kati ya Ujasusi na Ugaidi

Vyo
Ujasusi ni ugaidi wa kiistaarabu
 
Ni kweli kabisa Sir Chief
Wakati wa harakati za Ukombozi Afrika ya KUSINI
Umkontho we swize,yaani Jeshi la ANC waliwafanyia Makaburu vitendo vyote vya kudai haki kwa njia ambazo Leo tunapita Ugaidi,Makaburu waliita Ni vitendo vya kigaidi,lakini ANC waliita Ni mapambano ya kudai uhuru.

PLO ya Arafat ya Palestine waliwafanyia Waisrael vitendo vya kibabe ambavyo Waisrael waliita Ugaidi,lakini PLO waliita Ni mapambano ya kudai uhuru.

Wapiganaji wa Northern Island waliwafanyia kinyama serikali ya Uingereza,vitendo hivyo vilifanywa kwa staili ambayo Waingereza waliita vitendo vya Ugaidi lakini wao waliita harakati za kijeshi za kudai uhuru.

Kashmir mziki Ni huohuo,wapigania uhuru wanwafanyizia India,na washindi wanadai Ni mashambulizi ya kigaidi.

Kwa hiyo Ni ngumu kujua tendon hili Ni la kijasusi na tendo hili Ni la kigaidi.
 
Mbona ujasusi ni kitu rasmi?

Imewahi Kutokea miaka ya nyuma na ya hivi karibuni Majasusi wa Mossad kwenda Nchi mabalimabali kuwaua viongozi wa Kipalestina waliokua tishio kwa usalama wa Taifa la Israel.
Wamewaua kwa njia mabalimabali ikiwa Ni pamoja na kuwategea mabomu,kuwalenga kwa bastola,Bunduki na vipigo.
Mauaji haya yalifanyika Nchi za Ulaya na Afrika ya Kaskazini.

Je Mossad kama shirika rasmi la ujasusi walifanya Ugaidi dhidi ya viongozi hao wa Kipalestina?
 
Asante mkuu
 
Ndio
 

Inawezekana pia ukawa hujaelewa vizuri dhana ya ujasusi na ugaidi. Au pia kwani hao waliouwawa walikuwa na matishio gani kwa Israel?

Hebu zifahamu dhana hizi hapa kisha ujijijibu mwenyewe,
*Counterintelligence
*Counterterrorism

*Ujasusi ni kitendo cha ukusanyaji kwa siri taarifa za siri. Taarifa zenyewe zinaweza kumhusu mtu, shirika, kampuni, serikali au taifa. taarifa zenyewe zinaweza kuwa zinahusu uchumi, usalama wake, mipango yake au hata afya yake.

Mara nyingi mbinu/njia zinazotumiwa na Majasusi ni kujifanya;
Mfanyabiashara
Mwanafunzi
Kasisi
Shekhe
Mtalii
Mwanamichezo
Mwandishi wa habari
Na kadhalika.

*Ugaidi ni kitendo cha kutumia nguvu/ vitisho vya nguvu katika kushinikiza madai yafuatiliwe au yafanyiwe kazi.

Hivyo basi shirika kama Mossad haliwezi kufanya ugaidi bali, majukumu yake ni kufanya ujasusi na kupambana na wanaoifanyia ujasusi nchi yao pamoja na ugaidi.
 
Pia elewa kitendo cha kukusanya taarifa za siri iwe nchini kwako au kwenye nchi nyingine huo ni ujasusi sasa itategemea ni wapi taarifa hizo ulipoagizwa au zitakwenda kutumika kivipi, zikitumika kwa ajili ya kudhuru jamii au kuitia hofu huo ndio ugaidi sasa. Na hao waliotumia taarifa hizo katika kuidhuru jamii/ kuitia hofu hao ndio magaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…