Naomba kujua ukweli kuhusu 'kiama'

Naomba kujua ukweli kuhusu 'kiama'

hukumu(kiama) ya mwanadamu inaanza mara tu baada ya mtu kufa. aliyetubu dhambi na kupatana na Mungu atapelekwa Mbinguni na asiyetubu ataenda motoni. wale wa zamani walioangamizwa sio kwamba ni waovu zaidi yetu bali ni matashi ya Mungu kuchagua njia ya kutunyoosha viumbe wake. ulichofundishwa ktk imani yako ni kweli kabisa, kishike. tenda mema acha mabaya. penda kutubu kila unapomkosea Mungu.
Sawa mkuu nimekishika nilichofundishwa na kukifata mpaka muda huu ila bado hujanipa majibu ya maswali yangu.
 
Haya mambo ya kiroho kwa kiasi kikubwa yana utata sana. Tunaambiwa mtu yaani nafsi anapatikana kutokana na muunganiko wa mwili na roho (pumzi ya uhai) na kwamba mtu huyo anapokufa mwili uoza lakini roho ubaki ikisubiri siku ya kiama. Sasa swali ni kwamba kama kiama kinaanza muda au siku ile mtu anapokufa iweje adhabu iwe ni kwa roho tu na siyo kwa mwili pia wakati kipindi cha kutenda dhambi vilikuwa pamoja?

Na kama mateso yanaanza mara moja baada ya mtu kufa basi ni dhahiri kwamba wale wenzetu waliofariki karne nyingi zilizopita hadi siku ya kiama itakapofika watakuwa wamepata mateso makubwa zaidi (ya muda mrefu) kuliko wale watakao wamekufa miaka michache (mfano mwaka mmoja, miwili kumi n.k.) kabla ya hiyo siku ya kiama. Na kama wakianza kutumikia adhabu zao baada ya kiama hao waliokufa na kupata mateso karne nyingi zilizopita kuliko wengine watapunguziwa adhabu au la?!

Kingine mtu anazaliwa na kudumu duniani kwa dakika, masaa, siku au miaka michache tu lakini siku ya kiama anakuja kutumikia adhabu jehanamu milele! Daah...mimi hata sielewi bana.
Mkuu mimi pia ndio maana leo nimevunja ukimya nikauliza labda tutapata msaada humu ndani
 
Kwakuwa umeuliza kwa imani zote nami nisemi kidogo. Katika uisilam kiama ni siku ngumu kuliko ugumu wowote ambao mwanadamu anaweza waza. Ni siku ya hukumu. Kabla ya kusimama kiama ni wazi kuwa viumbe wote watakafu(wakiwemo maaika wote mpaka mtoa roho-Izraeli).
Kisha watu watafufuliwa kutoka katika matumbo ya ardhi wakiwa katika hali tofauti tofauti.kulingana na matendo yao. Hata hivyo bado siku hiyo itakuwa ngumu sana isipokuwa tu kwa wale waliridhiwa na mola wao.
Hapo ndipo watu watahukumiwa kwa matendo yao. Kuna mchakato mrefu.sana siku hiyo. Hakuna kujuana hapo baba hatamjua mwana wala mwana hatamjua mama. Kila mtu nafsi yake itakuwa imeshughulishwa na mambo yake. Kisha watu watahukumiwa kwa kuulizwa juu ya.yale waloyatenda. Na pindi watakapo danganya,itafungwa midomo yao kisha kila kiungo kipekee kitatoa ushahidi wa kila ulichokifanya.
Kwa wale wanodhani ukifa ndio kiama chako,hakika hawapo sahihi hata.kidogo. Kufa ni katika kitendo cha kufika.mwisho.wa dumia.na mwanzo wa akhera. Kaburi watu watu wataanza kukutana na kheri zao ama shari zao kulingana na matendo yao. Hapo ni adhabu kwa makosa hadi itakapo fika kiama. Na adhanu hii haipunguzi.adhabu atakayoipata mwanadamu siku ya kiama baada ya kuhukumiwa.
Hakika kiama ni siku nzito na tunamuomba Molla wetu atufishe.ili hali yu radhi na sisi ili tuweze kuongoka adhabu zake. Amin.
Mkuu nashukuru sana kwa ufafanuzi ila kama hutojali naomba unipe na hatima za watu wa kale kama kwenye maswali yangu nambari 2,3 na 4.
Shukrani
 
all livings things hapa dunian vimeshapitia kihama in a sense of exntiction the major one ilikua the permian exntiction ambayo ilitokea almost miaka milioni 250 iliyopita na almost 96% of species were wiped out.

Kihama cha all mankind katika karne yetu kinaweza kusababishwa na either kimondo chenye ukubwa kuipiga dunia, au vita ya nuclear katika ya nchi kubwa au ugonjwa wowote wa mlipuko unaosababishwa na super virus au bacteria.

Pia kuharibu ozone layer kutokana na uchafuzi wa mazingira kunaweza kuchangia kuleta kihama kwetu binadamu na all land animals. Bila ozone layer ambayo imechukua zaidi ya miaka milioni 120 kutengenezwa kutokana na oxygen ilikuwa inatoka baharini na kufanya chemical reaction na sunrays maisha ya viumbe hai ardhini yasingewezekana kwasababu ya dangerous radiation kutoka kwenye jua.

Lakini kiama cha dunia kama dunia ni almost miaka billion moja ijayo in which jua litakua limetumia hydrogen yake vya kutosha na likisha'exhaust elements zote kama fuel then litapanuka kwa ukubwa in which dunia inaweza kuwa swallowed na gravity ya jua.
That is what we can prove....I like it.
 
majibu ya maswali yako kwa upande wa ukirsto iko hivi ,moja ni kweli siku ya kiama ipo na kwenye biblia inafahamika kama siku ya hukumu soma biblia matahyo 24:14 "tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja"pia siku hii kibiblia inafahamika kama har-magedon soma ufunuo 16:14-16.
majibu ya swali la pili kuhusu kwanini Mungu aliwaangamiza wanadamu wa kipindi cha kwanza bila kusubiri siku ya kiama , ni kweli Mungu aliwangamiza wanadamu hawa bila kusubiri siku ya kiama ilikuwa ni kwa sababu Mungu alitoa agizo kwa wanadamu hawa juu ya nini wanawapaswa kufanya na nini hawapaswi kufanya lakini wanadamu hawa walishindwa kutii agizo hili soma Mwanzo 3:1-4 basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, msile matunda yote ya miti ya bustani? mwanamke akamwambia nyoka matunda ya miti ya bustani twaweza kula lakini matunda ya mti wa katikati ya bustani Mungu amesema msiyale wala msiyaguse msije mkafa ......
majibu ya swali la tatu , sikweli kwamba wanadamu wa Enzi hizo walikuwa na dhambi nyingi kuliko sisi bali wanadamu wa sasa na wakipindi hicho wanafanana kwa matendo na dhambi kinacho wasaidia wanadamu wa sasa ni ule upendo wa Mungu kuelekea ulimwengu huu kupitia damu ya mwanaye Yesu kristo ambapo Mungu aliupenda ulimwengu huu tena soma yohana 3;16
Majibu ya swali la nne kuhusu wanadamu wa Enzi hizo watafufuliwa ili kuhukumiwa ni kweli watafufuliwa tena na kuhukumiwa hukumu ya haki ukiacha ya kipindi kile amabayo iliwakumba hata ambao hawakuwa na makosa au dhambi soma 2petro 4-9

Mkuu awali ya yote nikushukuru kunijibu maswali yangu yote lakini pili ngoja nichukue biblia nipitie hivyo vifungu kwanza halafu ndo nitakua na neno la kuhoji.
 
Pitia jukwaa la jamii intelligence,kule angalau utapata majibu kwa kiasi.

Ila usiache kuutafuta ukweli kupitia google,youtube nk

Kaanze kutafuta hii makitu reincarnation.
Shukrani kwa muongozo
 
Kilikua kiama chao, nasi tunasubir kiama chetu
Sasa Amenn kwa hiyo wale moto hautowahusu? Na vipi sasa walokufa kwa maji (enzi za nuhu) wengine kwa moto (sodoma na gomola) na vipi sisi kiama chetu na adhabu ya moto wa milele hauoni hapo kama kutakuwa hamna fair justice?
 
all livings things hapa dunian vimeshapitia kihama in a sense of exntiction the major one ilikua the permian exntiction ambayo ilitokea almost miaka milioni 250 iliyopita na almost 96% of species were wiped out.

Kihama cha all mankind katika karne yetu kinaweza kusababishwa na either kimondo chenye ukubwa kuipiga dunia, au vita ya nuclear katika ya nchi kubwa au ugonjwa wowote wa mlipuko unaosababishwa na super virus au bacteria.

Pia kuharibu ozone layer kutokana na uchafuzi wa mazingira kunaweza kuchangia kuleta kihama kwetu binadamu na all land animals. Bila ozone layer ambayo imechukua zaidi ya miaka milioni 120 kutengenezwa kutokana na oxygen ilikuwa inatoka baharini na kufanya chemical reaction na sunrays maisha ya viumbe hai ardhini yasingewezekana kwasababu ya dangerous radiation kutoka kwenye jua.

Lakini kiama cha dunia kama dunia ni almost miaka billion moja ijayo in which jua litakua limetumia hydrogen yake vya kutosha na likisha'exhaust elements zote kama fuel then litapanuka kwa ukubwa in which dunia inaweza kuwa swallowed na gravity ya jua.
Kama sijakosea ulichomaanisha ni kwamba,
Kuna kiama ambacho maana yake viumbe vyote vitakufa lakini no judgement day wala life after death yani ukimaliza shughuli yako duniani basi. Au?
 
Mapepo yanakili uwepo wa Mungu, uwepo wa Yesu, uwepo wa kuzimu, uwepo wa siku ya hukumu na uwepo wa shetani.

Ndugu yangu, kuzimu kupo na siku ya hukumu hipo. Watu wataunguzwa na kuwa weusi kama mkaa vile. Na hata mapepo yenyewe yanapaogopa huko kuzimu.
 
Hv nyie mnatumia biblia tofauti au?
mkuu kwa kuwa umekuwa na mashaka pitia mafungu yafuatayo,
1wathesalonike 4:13-17, ila hasa zingatia msitali wa 16,17
--kwa sabab Bwana mwenyewa atashuka kutoka mbinguni na mwaliko mkuu, na sauti ya malaika mkuu,na parapanda ya Mungu nao walio KUFA KATIKA KRISTO WATAFUFULIWA KWANZA, kisha sisi tulio hai tutanyakuliwa pamaja nao mawinguni,

ufunuo 1.7, tazama yuaja na kila jicho litamwona, nahao waliomchoma na KABILA ZOTE ZA DUNIA, wataomboleza kwa ajiri yake,

kasome pia ufufuo wa kwanza
ufunuo 20;4-6

na ufufuo wa pili
ufunuo 20:11-5
nimeshindwa kupest hyo mafungu.. ila naomba usome ukiweza yaweke hapa..

mwisho ni mji mtakatifu
ufunuo 21:1-4

mkuu ukisoma mafungu hayo kwa uwezo wa ROHO WA MUNGU, utajua kuwa kiama ni hakika, angalizo tu yapasa uwe unaiamini biblia yenye vitabu 66,

Barikiwa sana
 
Hv nyie mnatumia biblia tofauti au?
mkuu kwa kuwa umekuwa na mashaka pitia mafungu yafuatayo,
1wathesalonike 4:13-17, ila hasa zingatia msitali wa 16,17
--kwa sabab Bwana mwenyewa atashuka kutoka mbinguni na mwaliko mkuu, na sauti ya malaika mkuu,na parapanda ya Mungu nao walio KUFA KATIKA KRISTO WATAFUFULIWA KWANZA, kisha sisi tulio hai tutanyakuliwa pamaja nao mawinguni,

ufunuo 1.7, tazama yuaja na kila jicho litamwona, nahao waliomchoma na KABILA ZOTE ZA DUNIA, wataomboleza kwa ajiri yake,

kasome pia ufufuo wa kwanza
ufunuo 20;4-6

na ufufuo wa pili
ufunuo 20:11-5
nimeshindwa kupest hyo mafungu.. ila naomba usome ukiweza yaweke hapa..

mwisho ni mji mtakatifu
ufunuo 21:1-4

mkuu ukisoma mafungu hayo kwa uwezo wa ROHO WA MUNGU, utajua kuwa kiama ni hakika, angalizo tu yapasa uwe unaiamini biblia yenye vitabu 66,

Barikiwa sana
 
Kama sijakosea ulichomaanisha ni kwamba,
Kuna kiama ambacho maana yake viumbe vyote vitakufa lakini no judgement day wala life after death yani ukimaliza shughuli yako duniani basi. Au?
yes mkuu ukifa ndo habari yako inaashia hapo utabakia kuwa tu kama fossils after million and million of years.

Unaweza kuja kutumika hata kama coal hapo baadaye. Lakini kinachokua kimekufa ni cells na your consciousness lakini atoms ambazo zimeutengeneza mwili wako zitaendelea kuwepo for the next billions and billions years labda had mwisho wa universe ambao we call it the big crunch.
 
Niweke nguvu wapi sasa mkuu?
Mungu aliyekuumba ndiye anafahamu mahitaji yako. Kidogo unachopata saidia wasiojiweza,achana na mambo ya kidunia waheshimu na wasaidie wazazi wako over.
 
Mkuu nashukuru sana kwa ufafanuzi ila kama hutojali naomba unipe na hatima za watu wa kale kama kwenye maswali yangu nambari 2,3 na 4.
Shukrani
pitia 1wathesalonike 4;13-17
utapata majib mkuu.. yapo wazi kabisa.
2petro 3:3-7
mkijua kwanza neno hili ya kwamba watakuja na dhihaka zao,watu wenye kudhihaki,wafuatao tamaa zao wenyewe, na kusema ipo wapi ahadi ile ya kuja kwake?kwa maana tangu hapo babu zetu walipolala vitu vyote vinakaa hali hyo hyo tangu mwanzo wa kuumbwa, maana hufumba macho yao wasione kuwa tangu mwanzo zilikuwepo mbingu tangu zamani na nchi pia imefanywa kutoka ktk maji kwa neno la Mungu...

kwa hyo Dunia ile ya mwanzo, ilighalikishwa kwa maji ikaangamia lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto kwa neno LILO HILO ZIKILINDWA HATA SIKU YA HUKUMU NA YAKUANGAMIA KWAO WANADAMU WASIO MCHA MUNGU..
 
THERE IS NO GOD,ENJOY YOUR LIFE TO THE MAXIMUM! BE HAPPY

Karibu katika ulimwengu huru

...........Free ideas.......
 
mkuu kwa kuwa umekuwa na mashaka pitia mafungu yafuatayo,
1wathesalonike 4:13-17, ila hasa zingatia msitali wa 16,17
--kwa sabab Bwana mwenyewa atashuka kutoka mbinguni na mwaliko mkuu, na sauti ya malaika mkuu,na parapanda ya Mungu nao walio KUFA KATIKA KRISTO WATAFUFULIWA KWANZA, kisha sisi tulio hai tutanyakuliwa pamaja nao mawinguni,

ufunuo 1.7, tazama yuaja na kila jicho litamwona, nahao waliomchoma na KABILA ZOTE ZA DUNIA, wataomboleza kwa ajiri yake,

kasome pia ufufuo wa kwanza
ufunuo 20;4-6

na ufufuo wa pili
ufunuo 20:11-5
nimeshindwa kupest hyo mafungu.. ila naomba usome ukiweza yaweke hapa..

mwisho ni mji mtakatifu
ufunuo 21:1-4

mkuu ukisoma mafungu hayo kwa uwezo wa ROHO WA MUNGU, utajua kuwa kiama ni hakika, angalizo tu yapasa uwe unaiamini biblia yenye vitabu 66,

Barikiwa sana

Kwann unipe limit ya kutumia biblia ya vitabu 66.? Kwann nisitumie bibilia inayozidi vtabu zaid ya 66? Wap yesu au mungu amemrisha bibilia inayopaswa kutumika n vitabu 66?
 
Hakuna kiama mkuu, hizo ni hadithi za kiama ni kama zile movie za fiction za Hollywood. Kama huamini mtafute Kiranga
 
Back
Top Bottom