Naomba kujua ukweli kuhusu 'kiama'

Naomba kujua ukweli kuhusu 'kiama'

Habari zenu wana JF,

Kuna kitu nimekiwaza na kukitafakari kwa muda wa kama siku 3 hivi lakini bado sijapata majibu yake. Basi nipo hapa kuomba msaada wa kueleweshwa kiundani kwa watu wenye uelewa wa mambo ya kidini awe muislam, mkristo budhaa na hata asiye na dini.

Suala kubwa linalonitatiza ni kuhusu ukweli wa siku ya kiama, jehanamu na pepo. Je kweli hivi vitu vipo kweli? Nikiri wazi kabisa kwamba mimi ni mkristo mkatoliki na nimekua nikifundishwa haya kama sio kukaririshwa toka nikiwa mdogo katika mafundisho ya komunio ya kwanza na kipaimara kwamba kuna hivyo vitu 3 nilivyovitaja.

Yafuatayo ni maswali ambayo najiuliza na ningefurah kama nitapata majibu ya kina na kuridhisha.

1. Je ni kweli kuna siku ya kiama?

2. Na kama kweli ipo kwanini MUNGU aliwaadhibu na kuviangamiza baadhi ya vizazi kwa matendo yao machafu na kutosubiri siku ya kiama?

3. Je hawa walioadhibiwa na kuangamizwa siku za nyuma walikuwa waovu kuliko sisi wa zama hizi?

4. Je hao walioangamizwa wataletwa tena mbele ya hukumu? Na nini hatima yao na ilihali walishaadhibiwa kwa kuangamizwa?

Baada ya kupata ufafanuzi wa kutosha wa maswali hayo nadhani suala la pepo na jehanamu nitaweza kulielewa kwa urahisi.

Inawezekana kabisa kuwa kuna mada kama hii imeshawahi kujadiliwa kama hamtojali naomba kuwekewa link yake.

NB: Nimetumia zama za nabii Nuhu na gharika kuu kuuliza maswali hayo.

Shukrani.

Hivi huyu Kiama ana undugu na yule changudoa wa bongo movie (Esther Kiama)?
 
Hakuna kitu kama hicho. Mambo ya kijinga sana kuamini sijui kiama, moto, sijui peponi ni ujinga tu. Kifupi mambo ya Dini ni ya kufikirika tu ili kukutisha uwe mtumwa wa imani, na ukizidisha maimani ya hizo riwaya zilizoletwa kwenye majahazi, unaishia kuua watu bure na kuwa hata gaidi kwa kudhani unafanya kazi ya Mungu kumbe umesharukwa akili. We ishi kwa amani, usiue, usidhulumu, na machafu achana nayo utaishi vizuri basi.
Hata hizo imani unazoziponda hapa haziruhusu kuua kama watu wengine wanafanya.
 
Wewe huna Elimu ya hizo riwaya zako, soma vizuri tena, unajua maana ya Alpha na Omega? Mungu unajua destiny ya kila binaadamu na mwisho wake, sasa kwa nini anajua utaenda motoni halafu anakuacha hata ukiomba vipi utachomwa tu kwa kuwa alishapanga! So why worry your self?
Usipende kuzungumza usichokuwa na elimu nacho ni hatari sana
 
Habari zenu wana JF,

Kuna kitu nimekiwaza na kukitafakari kwa muda wa kama siku 3 hivi lakini bado sijapata majibu yake. Basi nipo hapa kuomba msaada wa kueleweshwa kiundani kwa watu wenye uelewa wa mambo ya kidini awe muislam, mkristo budhaa na hata asiye na dini.

Suala kubwa linalonitatiza ni kuhusu ukweli wa siku ya kiama, jehanamu na pepo. Je kweli hivi vitu vipo kweli? Nikiri wazi kabisa kwamba mimi ni mkristo mkatoliki na nimekua nikifundishwa haya kama sio kukaririshwa toka nikiwa mdogo katika mafundisho ya komunio ya kwanza na kipaimara kwamba kuna hivyo vitu 3 nilivyovitaja.

Yafuatayo ni maswali ambayo najiuliza na ningefurah kama nitapata majibu ya kina na kuridhisha.

1. Je ni kweli kuna siku ya kiama?

2. Na kama kweli ipo kwanini MUNGU aliwaadhibu na kuviangamiza baadhi ya vizazi kwa matendo yao machafu na kutosubiri siku ya kiama?

3. Je hawa walioadhibiwa na kuangamizwa siku za nyuma walikuwa waovu kuliko sisi wa zama hizi?

4. Je hao walioangamizwa wataletwa tena mbele ya hukumu? Na nini hatima yao na ilihali walishaadhibiwa kwa kuangamizwa?

Baada ya kupata ufafanuzi wa kutosha wa maswali hayo nadhani suala la pepo na jehanamu nitaweza kulielewa kwa urahisi.

Inawezekana kabisa kuwa kuna mada kama hii imeshawahi kujadiliwa kama hamtojali naomba kuwekewa link yake.

NB: Nimetumia zama za nabii Nuhu na gharika kuu kuuliza maswali hayo.

Shukrani.
Ndio maana nasema vitabu vya dini vinajichanganya. Ukitafakari kwa undani unaona kuwa haya mambo ya dini ni stories za kutunga tu, hazina uhalisia wowote. Hakuna mambo ya kiama. Ni kutishana tu ili watu wawe na amani. Sisi wakatoliki tulikuwa tunaambiwa kuwa kabla ya kupokea mwili wa Bwana lazima ipite angalau saa moja bila kuweka chochote mdomoni. Reason: Waafrika walikuwa hawana utamaduni wa kupiga mswaki, hivyo ukiruhusu watu wale muda huo , padre anapokukomunisha kinywani kutakuwa kumejaa vyakula na hivyo itakuwa kumpumulia harufu mbaya! Lakini tuliambiwa kuwa ni dhambi ukila one hour within communion. Sijui dhambi hiyo iliishia wapi sasa
 
Ulimwengu huru ulijitengeneza wenyewe?

Who created the laws of nature?

Nimesikia hata computers na manowari zilijitengeneza zenyewe, karibuni kwenye ulimwengu wa full(fool?)automation!

Ni nani aliyeutengeneza huo ulimwengu huru unaosema?

Huwezi kumtambua Mungu unaposhindwa kujitambua mwenyewe. Na hiyo ndio Changamoto yako.

Link The Noble Quran - القرآن الكريم

Ni wendawazimu kukataa kwamba ulimwengu ulitokea out of nothing halafu hapo hapo ukaamini kuwa eti mungu alitokea tu!.Think big!

Karibu katika ulimwengu huru!
..........Free ideas.......
 
Ni wendawazimu kukataa kwamba ulimwengu ulitokea out of nothing halafu hapo hapo ukaamini kuwa eti mungu alitokea tu!.Think big!

Karibu katika ulimwengu huru!
..........Free ideas.......
Samahani mkuu, hili LA ulimwengu kutokea "out of nothing" unalithibitisha vipi?
 
Kwakuwa umeuliza kwa imani zote nami nisemi kidogo. Katika uisilam kiama ni siku ngumu kuliko ugumu wowote ambao mwanadamu anaweza waza. Ni siku ya hukumu. Kabla ya kusimama kiama ni wazi kuwa viumbe wote watakafu(wakiwemo maaika wote mpaka mtoa roho-Izraeli).
Kisha watu watafufuliwa kutoka katika matumbo ya ardhi wakiwa katika hali tofauti tofauti.kulingana na matendo yao. Hata hivyo bado siku hiyo itakuwa ngumu sana isipokuwa tu kwa wale waliridhiwa na mola wao.
Hapo ndipo watu watahukumiwa kwa matendo yao. Kuna mchakato mrefu.sana siku hiyo. Hakuna kujuana hapo baba hatamjua mwana wala mwana hatamjua mama. Kila mtu nafsi yake itakuwa imeshughulishwa na mambo yake. Kisha watu watahukumiwa kwa kuulizwa juu ya.yale waloyatenda. Na pindi watakapo danganya,itafungwa midomo yao kisha kila kiungo kipekee kitatoa ushahidi wa kila ulichokifanya.
Kwa wale wanodhani ukifa ndio kiama chako,hakika hawapo sahihi hata.kidogo. Kufa ni katika kitendo cha kufika.mwisho.wa dumia.na mwanzo wa akhera. Kaburi watu watu wataanza kukutana na kheri zao ama shari zao kulingana na matendo yao. Hapo ni adhabu kwa makosa hadi itakapo fika kiama. Na adhanu hii haipunguzi.adhabu atakayoipata mwanadamu siku ya kiama baada ya kuhukumiwa.
Hakika kiama ni siku nzito na tunamuomba Molla wetu atufishe.ili hali yu radhi na sisi ili tuweze kuongoka adhabu zake. Amin.

Well written. Mashallah
Mwenyezi Mungu atufanyie wepesi pindi tuifkiapo siku hiyo
 
Samahani mkuu, hili LA ulimwengu kutokea "out of nothing" unalithibitisha vipi?

Kila kitu kiko wazi sayansi inaeleza hatua zote labda ni uvivu wa kusoma tu!
............free ideas.....
 
Siku ya kufufuliwa tutatoka ktk tumbo la ardhi na kuulizana ardhi hii leo ina nini?!na kila atakaejiuliza amekaa mda gn kaburini jibu lake ni siku moja au ktk shm ya siku tu!km umelala then ukaamka.
Izrail mtoa roho kabla ya kiama atatumwa atoe roho viumbe wote waliobaki akimaliza atamuuliza mungu nimeshamaliza mungu atamjibu bado jamaa atarudi atazunguka kote hadi kw malaika atakuta wamekufa kisha atamrudia mungu kumueleza kwmb hamna kilichobaki.
Hapo mungu atamjibu ni ww pekee ndo umebaki jitoe roho unikabidhi ataitoa huku akilia kwa uchungu.
Baada ya hapo huku duniani itanyesha mvua ya shahawa na watu wataanza kufufuka na kujiuliza kuna nini tena tunaamshwa usungizi ulikuwa mtamu?!
Hapo ndo mungu muumba atasimama na kusema leo ndo siku ya haki hakuna atakaeonewa isipokuwa kwa aliyoyatenda.hii siku haina shaka ndugu zangu sbb huku duniani hakuna haki mkubwa anaonea mdogo tajir anatesa maskini
hahaa nawewe unaamoni ujinga ulioandika
 
Ni wendawazimu kukataa kwamba ulimwengu ulitokea out of nothing halafu hapo hapo ukaamini kuwa eti mungu alitokea tu!.Think big!

Karibu katika ulimwengu huru!
..........Free ideas.......
Huo ndio uwendawazimu wa wanaoamini katika ulimwengu huru. Sheria za ulimwengu huru kazitunga nani? Zimejitunga zenyewe?

Unaelewa Mungu ni nani?
Unaelewa dhana ya " space, time and matter" na uhusiano wake na ulimwengu huru?

Jitumbue majipu ili uingie katika ulimwengu huru. Wewe hutakiwi kufikiri kabisa!

Ulimwengu huru ulijitengeneza wenyewe?

Who created the laws of nature?

Nimesikia hata computers na manowari zilijitengeneza zenyewe, karibuni kwenye ulimwengu wa full(fool?)automation!

Ni nani aliyeutengeneza huo ulimwengu huru unaosema?

Huwezi kumtambua Mungu unaposhindwa kujitambua mwenyewe. Na hiyo ndio Changamoto yako.

Link The Noble Quran - القرآن الكريم
safi sana mkuu umepiga ya kichwa,huo ulimwengu huru unatokea tu bila kua created.
 
Huo ndio uwendawazimu wa wanaoamini katika ulimwengu huru. Sheria za ulimwengu huru kazitunga nani? Zimejitunga zenyewe?

Unaelewa Mungu ni nani?
Unaelewa dhana ya " space, time and matter" na uhusiano wake na ulimwengu huru?

Jitumbue majipu ili uingie katika ulimwengu huru. Wewe hutakiwi kufikiri kabisa!

Kabla hujauliza iweje ulimwengu utokee tu,tafakari iweje mungu(kama yupo)atokee tu.!

Najua mungu ni Idea tu
Space time and matter nazijua labla wewe ndo huzijui!

Karibu katika ulimwengu huru
.........Free ideas.....
 
Kwa hiyo kwako wewe ulimwengu huru ni Idea tu?

Unazungumzia mungu au Mungu?

Kabla hujauliza iweje ulimwengu utokee tu,tafakari iweje mungu(kama yupo)atokee tu.!

Najua mungu ni Idea tu
Space time and matter nazijua labla wewe ndo huzijui!

Karibu katika ulimwengu huru
.........Free ideas.....
Free ideas
Unaye mama/baba? Baba yako anaye baba?
Unaamini Babu ya mababu zako alikuwa ni nyani au binadamu/mtu?
 
Kabla hujauliza iweje ulimwengu utokee tu,tafakari iweje mungu(kama yupo)atokee tu.!

Najua mungu ni Idea tu
Space time and matter nazijua labla wewe ndo huzijui!

Karibu katika ulimwengu huru
.........Free ideas.....
Ulimwengu huru ni Idea tu?

all livings things hapa dunian vimeshapitia kihama in a sense of exntiction the major one ilikua the permian exntiction ambayo ilitokea almost miaka milioni 250 iliyopita na almost 96% of species were wiped out.

Kihama cha all mankind katika karne yetu kinaweza kusababishwa na either kimondo chenye ukubwa kuipiga dunia, au vita ya nuclear katika ya nchi kubwa au ugonjwa wowote wa mlipuko unaosababishwa na super virus au bacteria.

Pia kuharibu ozone layer kutokana na uchafuzi wa mazingira kunaweza kuchangia kuleta kihama kwetu binadamu na all land animals. Bila ozone layer ambayo imechukua zaidi ya miaka milioni 120 kutengenezwa kutokana na oxygen ilikuwa inatoka baharini na kufanya chemical reaction na sunrays maisha ya viumbe hai ardhini yasingewezekana kwasababu ya dangerous radiation kutoka kwenye jua.

Lakini kiama cha dunia kama dunia ni almost miaka billion moja ijayo in which jua litakua limetumia hydrogen yake vya kutosha na likisha'exhaust elements zote kama fuel then litapanuka kwa ukubwa in which dunia inaweza kuwa swallowed na gravity ya jua.
Kweli umepiga domo.
 
Back
Top Bottom