ni utaratibu na taadhima tuliyorithi toka enzi ya mkoloni tukainasibu kama mfumo wa kuonyesha utii na heshima kwa utawala,.hiyo sio kwa mkuu wa nchi tu, hata mkuu wa mkoa/ mkuu wa wilaya akitoka kwenda kikazi mahali protokali ya mapokezi/kuagana huwa inafanania ..yaani wale wanaowajibika chini ya mamlaka yake huwepo /hupaswa kuwepo.
Inawezekana sana kubadili uwepo wa mlundikano wa wasindikizaji /wapokeaji ila ni jambo la kimfumo ambalo kwa hulka ya watawala waliopo na wataokuja wasipoona haja ya kubadilisha hayo tutaendelea kuliongelea huku mitandaoni. fikiria kuna kipindi hadi vikundi vya ngoma kwaya na brass band vilikuwa vinaenda kuaga na kupokea viongozi wa ndani ya nchi [emoji2][emoji2], haishindikani kupunguza na kuondoa lundo iwapo nia ya dhati ikiwepo.