Naomba kujua utaratibu wa Kumtoa Mtu kwenye Orodha ya wanufaika wa Bima ya Afya

Naomba kujua utaratibu wa Kumtoa Mtu kwenye Orodha ya wanufaika wa Bima ya Afya

kama unataka kumtoa mtu kwenye Bima, wamekupa utaratibu huo ikiwa ni takwa la kisheria ili wathibitishe ukweli kabisa isije ukawa unamtoa kumbe ni uongo.. Sheria inakulinda wewe na wao ndio maana wanakwambia ukaape
Thank you very much, I agree
 
Ukiwa mwanachama wa bima ya afya umewaunganisha baba, mama na watoto ikatokea mume au mke mmeachana ukataka kumtoa kwenye mfumo wa bima mbona wanakata mpaka uende mahakamani uape.

Hapo vipi?
Sasa mbona umesha pewa utaratibu
Tofauti na Waislam dini zingine hazina TALAKA, sasa watahakikishaje kuwa mmeachana?
Ndio sababu ukapewa huo utaratibu mbadala badala ya kukutaka ulete cheti cha talaka
Ila kama hujapata mbadala, nakushauri umuache tu aendelee kupata huduma kwani haikupunguzii chochote...
 
Sasa mbona umesha pewa utaratibu
Tofauti na uislam Dini zingine hazina TALAKA, sasa watahakikishaje kuwa mmeachana?
Ndio sababu ukapewa huo utaratibu mbadala badala ya cheti cha talaka
Ila kama hujapata mbadala, nakushauri umuache tu aendelee kupata huduma kwani haikupunguzii chochote...
Thank you very much my brothers, I love you very much
 
Naomba kujua, utaratibu wa kupata kadi nyingine baada ya kadi ya mtegemezi kupotea.
Nenda ofisi za NHIF ukachukue form Kama Ile ya mwanzo wakati unaijaza Kwa ajili ya usajili.

Kwenye Ile form Kwa juu wameoanisha Aina ya maombi Kama ni maombi mapya, maombi ya nyongeza ya wategemezi au ni maombi ya upotevu wa Kadi.

Jaza taarifa Kwa ukamilifu Kama ulivyojaza mwanzo then Rudisha form NHIF baada ya siku tano watakutumia Control number ulipie Kwa ajili ya kadi mpya ni elfu 20 Tu.
 
Nenda ofisi za NHIF ukachukue form Kama Ile ya mwanzo wakati unaijaza Kwa ajili ya usajili.

Kwenye Ile form Kwa juu wameoanisha Aina ya maombi Kama ni maombi mapya, maombi ya nyongeza ya wategemezi au ni maombi ya upotevu wa Kadi.

Jaza taarifa Kwa ukamilifu Kama ulivyojaza mwanzo then Rudisha form NHIF baada ya siku tano watakutumia Control number ulipie Kwa ajili ya kadi mpya ni elfu 20 Tu.
Asante mwamba
 
Mbona simple tu. Km ulivyopewa utaratibu we nenda mahakani ukaape na siyo kazi. Unapoambiwa kuapa siyo kwenda kunyanyua Biblia au Quran km Wabunge bungeni bali ni kwenda kupewa barua ya uthibitisho wa kisheria kuwa umemuacha MKEO na ni rahisi ukienda na taraka km huna pitia mlango wa uani (nadhani umenifahamu nachomaanisha) kupata hicho kiapo. Haisumbui kabisa ni wewe tu.

Km unashindwa kwenda mahakani pia ni simple tu, Kila atakapoenda kutumia hiyo kadi ya Bima lazima ujumbe utakuja kwako ukikutaka kubatilisha hiyo huduma km hiyo kadi huitambui na huwa wanaweka na namba ya kujibu hiyo sms. Hapo wewe chap una reply kuwa hauitambui hiyo kadi, then wao kule kwenye mtandao Wanaiblock. Akienda tena hospitali ataanbiwa bima yake imefungiwa maana haitambuliki kwenye mfumo. Atahangaika kuirudisha lakini atapata kazi na hata akipitia mlango wa nyuma, wewe unakuwa tu unasubiri sms, ikiingia tu kuwa katibiwa unawajibu kuwa hiyo kadi huitambui hadi ataitupa mwenyewe.

NB
Vijana msikurupuke kuwakatia bima za afya hao wake zenu harakaharaka kwa sababu za utamu wa uchi wanaowapa, ipo siku itawagharim, km wewe. Unakuta kijana anakataa kumuingiza baba au mama yake ktk bima kwa sababu ya mwanamke tena MKE kimeo ambae baada ya miaka 3 au 6 mnaachana na anaondoka na Bima yako huku wazazi wako wakiteseka na maradhi ya uzeeni.

Jifunzeni, siku zote MKE siyo ndugu yako bali ni rafiki tu wa karibu Wala hamna vinasaba hata chembe, sasa kwa nini umthamini kuliko wazazi wako. Na bado urithi unamuandikisha harakaharaka utadhani hamjawahi kuona uchi za wanawake. Kwani wakati mnazaliwa mlipita wapi. Acheni ulimbukeni. Mkikua mtaacha tu, sisi wazazi wenu tulishafika ukomo wa tamaa.
 
Back
Top Bottom