Mbona simple tu. Km ulivyopewa utaratibu we nenda mahakani ukaape na siyo kazi. Unapoambiwa kuapa siyo kwenda kunyanyua Biblia au Quran km Wabunge bungeni bali ni kwenda kupewa barua ya uthibitisho wa kisheria kuwa umemuacha MKEO na ni rahisi ukienda na taraka km huna pitia mlango wa uani (nadhani umenifahamu nachomaanisha) kupata hicho kiapo. Haisumbui kabisa ni wewe tu.
Km unashindwa kwenda mahakani pia ni simple tu, Kila atakapoenda kutumia hiyo kadi ya Bima lazima ujumbe utakuja kwako ukikutaka kubatilisha hiyo huduma km hiyo kadi huitambui na huwa wanaweka na namba ya kujibu hiyo sms. Hapo wewe chap una reply kuwa hauitambui hiyo kadi, then wao kule kwenye mtandao Wanaiblock. Akienda tena hospitali ataanbiwa bima yake imefungiwa maana haitambuliki kwenye mfumo. Atahangaika kuirudisha lakini atapata kazi na hata akipitia mlango wa nyuma, wewe unakuwa tu unasubiri sms, ikiingia tu kuwa katibiwa unawajibu kuwa hiyo kadi huitambui hadi ataitupa mwenyewe.
NB
Vijana msikurupuke kuwakatia bima za afya hao wake zenu harakaharaka kwa sababu za utamu wa uchi wanaowapa, ipo siku itawagharim, km wewe. Unakuta kijana anakataa kumuingiza baba au mama yake ktk bima kwa sababu ya mwanamke tena MKE kimeo ambae baada ya miaka 3 au 6 mnaachana na anaondoka na Bima yako huku wazazi wako wakiteseka na maradhi ya uzeeni.
Jifunzeni, siku zote MKE siyo ndugu yako bali ni rafiki tu wa karibu Wala hamna vinasaba hata chembe, sasa kwa nini umthamini kuliko wazazi wako. Na bado urithi unamuandikisha harakaharaka utadhani hamjawahi kuona uchi za wanawake. Kwani wakati mnazaliwa mlipita wapi. Acheni ulimbukeni. Mkikua mtaacha tu, sisi wazazi wenu tulishafika ukomo wa tamaa.