Naomba kujua utaratibu wa wanandoa walio ajiriwa serikalini kuhama

Naomba kujua utaratibu wa wanandoa walio ajiriwa serikalini kuhama

1Africa54

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2025
Posts
464
Reaction score
549
Habari wana JAMII FORUM naomba kuuliza ni taratibu zipi kwa mwanandoa kuhama kikazi serikalini na kumfata mwenza wake ambae kapangwa mbali yaani halmashauri tofauti

Pia mume anaruhisiwa kumfata mke au ni mke ndio Sheria inamtaka tu ?

Je inachukua mda gani kwa mwanandoa wa ajira mpya kuhama kikazi serikalini kumfata mwenza wake (ni miaka mingapi baada ya kuanza kazi)?
 
Mbona kama zoezi lilikuwa la mda fulani

Dodoma. Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imewataka watumishi wa umma wanaotaka kuhama kwa lengo la kuwafuata wenza wao wa ndoa kuwasilisha taarifa kwa waajiri wao kabla au ifikapo Oktoba 5, 2024.

Hata hivyo, waziri mwenye dhamana na wizara hiyo, George Simbachawene amesema kuna utaratibu utafuatwa, akionya wale watakaobainika kudanganya watafukuzwa kazi.

Barua kuhusu wito huo imetolewa na Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, Juma Mkomi Septemba 24, 2024 kwenda kwa viongozi wa umma kwa ajili ya utekelezaji.
 
Waziri wa Utumishi aliruhusu hili jambo na akaagiza waajiri wasikwamishe maombi ya watumishi walio chini yao. Sasa sijui kama Wizara ya Utumishi inasimamia utekelezaji wa agizo hilo
 
Hakuna utaratibu ila utaratibu uliopo ni kutoa rushwa tu ndio utafanikisha jambo lako,hii nchi ni corrupted.
 
Back
Top Bottom