Naomba kujua utofauti uliopo kati ya gari "manual" na "automatic" kifaida na kihasara. Na pia naomba kujua kiundani kidogo dondoo za RAV 4 manual

Ndo ukweli.wenzetu wanaotengeneza hivi vyombo walishatoka kwenye dunia ya kutumia nguvu kama ufahari,siku hizi vitu ni soft,unabonyeza tu ngoma inatembea,nguvu kidogo akili nyingi.Uku afrika ndo bado tunawaza ujinga wakati hakuna ata gear box moja tuliyotengeneza.Hatutaki kukimbizana na mabadiliko ya teknolojia.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Binafsi naprefer gari Auto kwa town trips. Na Manual kwa safari ndefu ama kwenye barabara zenye changamoto mfano milima, utelezi n.k.

Pia gari Ndogo hizi kama Harrier, Rav4, IST, n.k inapendeza zaidi ikiwa Auto kuliko manual.

Ila gari kuanzia Pick up, Binafsi hupendelea iwe Manual kuliko Automatic..
 
Mkuu kwanini? kwenye magari ya mashindano sijaona dereva anaendesha automatic.
 
Mimi si mtaalamu wa magari, lakini kufikia hapa, hakuna mwanajamvi aliyekata kiu cha mtoa hoja.

Ni nini tofauti ya msingi ya ubora kati ya Auto na manual?
Tofauti ya ubora kivip wakati unaona automatic ni advanced technology ya gearbox.Kwahiyo automatic ni bora zaidi kwasababu ni techolojia iliyokua kutoka kwenye uduni na ndiko dunia iliko.Itafika miaka manual zitakua hazitengenezwi au zitatengenezwa kwa oda.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Hilo sasa mkuu ndiyo jibu na kama vipi mada ifungwe!
 
Mkuu, kuna mtu anauza hiyo rav 4 manual ila ni namba A. Hapo una ushauri gani boss
 
Mkuu kwanini? kwenye magari ya mashindano sijaona dereva anaendesha automatic.
Mara nyingi yale ni matoleo maalum nando maana ata modification zake ziko tofauti na gari za kawaida kwasababu ya matumizi yake.Lakini haimaanishi kwamba iko tuendako hakutakua na auto.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
sawa, automatic ni more advanced technology. Vp khs changamoto ya auto vs manual
kimatumiizi
 
Mkuu, kuna mtu anauza hiyo rav 4 manual ila ni namba A. Hapo una ushauri gani boss
Kama ni chini ya milioni nne chukua, hautajutia. RAV 4 hiyo kama ni manual Nina uhakika haijatembea kms nyingi. Ila kama bei ni zaidi ya milioni nne basi achana mayo nunua automatic nyinginezo kama Vitz, IST, na Toyota nyingine za CC ndogo
 
Kama ni chini ya milioni nne chukua, hautajutia. RAV 4 hiyo kama ni manual Nina uhakika haijatembea kms nyingi. Ila kama bei ni zaidi ya milioni nne basi achana mayo nunua automatic nyinginezo kama Vitz, IST, na Toyota nyingine za CC ndogo
thanks boss, noted! Ila naomba ufafanue kidogo hapo kwenye cc, mimi ni mgeni kabisa.
 
Ajabu UK niliona gari nyingi sana manual.
Umetoka lini UK mkuu?? Now most of their Car ni Auto hata zile Land Rover zipo za kisasa zaidi, Manual UK ziko chache sana sio kwa uwingi huo unaousema hapa, i've been there miezi michache nyuma hapa. Nimeendesha sana AUDI, CHEVO, na hizo Land Rover zote nilikuta AUTO. itakuwa ulikwenda enzi ambapo Mjomba Magu anapiga MASTERS.
 
Adavantage za manual.
*Ni economy kwenye mafuta
*Ikiaribika inatengenezeka
*Watumiaji ni wachache so gari haiazimwi ovyo.
*service yake sio ya gharama sana
*Betri ikizingua unasukumwa chuma inawaka.
*Unaweza ukaendesha umbali mdogo ukiwa umemaliza gia zote ata kama ni mwendo wa taratibu au mkali

Automatic
*Raisi kuendesha
*Ni nzuri kwa mijini barabara zenye jam
*Rahisi kuuzika kama ukitaka kuiuza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…