Naomba kujua utofauti uliopo kati ya gari "manual" na "automatic" kifaida na kihasara. Na pia naomba kujua kiundani kidogo dondoo za RAV 4 manual

Naomba kujua utofauti uliopo kati ya gari "manual" na "automatic" kifaida na kihasara. Na pia naomba kujua kiundani kidogo dondoo za RAV 4 manual

Mtu anayehangaika kuendesha gari manual hasa private car miaka hii ni wale watu wanaoishi nyuma ya muda.......kwa sasa watu wapo kwenye teknolojia ya gari ambazo zinajiendesha zenyewe bila hata dereva kugusa sterling, leo hii mtu anajisifia kuendesha gari manual? siku hizi hata ndege unaweka kwenye autopilot na rubani anaweza kupiga usingizi kama abiria wengine......na inakoelekea ndege zitakuwa zinaendeshwa kutokea ardhini kwenye control room.
Ndo ukweli.wenzetu wanaotengeneza hivi vyombo walishatoka kwenye dunia ya kutumia nguvu kama ufahari,siku hizi vitu ni soft,unabonyeza tu ngoma inatembea,nguvu kidogo akili nyingi.Uku afrika ndo bado tunawaza ujinga wakati hakuna ata gear box moja tuliyotengeneza.Hatutaki kukimbizana na mabadiliko ya teknolojia.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Binafsi naprefer gari Auto kwa town trips. Na Manual kwa safari ndefu ama kwenye barabara zenye changamoto mfano milima, utelezi n.k.

Pia gari Ndogo hizi kama Harrier, Rav4, IST, n.k inapendeza zaidi ikiwa Auto kuliko manual.

Ila gari kuanzia Pick up, Binafsi hupendelea iwe Manual kuliko Automatic..
 
Kama ni ivyo itafika miaka wanaume watakua hawaendeshi magari.maana swala la manual au automatic linatokana na mabadiliko ya teknolojia.na kwakadri miaka inavyoenda vyombo vingi vya moto vitakua vinatengenezwa automatic.Ata ivyo ndege na meli ni automatic sasa sijui nazenyewe zilitengenezwa hivyo ili ziendeshwe na wanawake tu au ulimaanisha nini kusema auto nizakuendesha wanawake.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Mkuu kwanini? kwenye magari ya mashindano sijaona dereva anaendesha automatic.
 
Mimi si mtaalamu wa magari, lakini kufikia hapa, hakuna mwanajamvi aliyekata kiu cha mtoa hoja.

Ni nini tofauti ya msingi ya ubora kati ya Auto na manual?
Tofauti ya ubora kivip wakati unaona automatic ni advanced technology ya gearbox.Kwahiyo automatic ni bora zaidi kwasababu ni techolojia iliyokua kutoka kwenye uduni na ndiko dunia iliko.Itafika miaka manual zitakua hazitengenezwi au zitatengenezwa kwa oda.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Tofauti ya ubora kivip wakati unaona automatic ni advanced technology ya gearbox.Kwahiyo automatic ni bora zaidi kwasababu ni techolojia iliyokua kutoka kwenye uduni na ndiko dunia iliko.Itafika miaka manual zitakua hazitengenezwi au zitatengenezwa kwa oda.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Hilo sasa mkuu ndiyo jibu na kama vipi mada ifungwe!
 
Manual inaboa sana Barbara zetu hizi za foleni kali kama Dar

Ila barabara kama haina foleni sana ni fresh sana, automatic ni chaguo bora zaidi kwa RAV 4 sababu ya kusevu mafuta kwenye foleni ukilinganisha na manual.

Kiundani, RAV 4 manual inatumia mafuta vizuri sana na inadumu sana. Vifaa vyake vinapatikana kwa urahisi. Wengine watajazia...
Mkuu, kuna mtu anauza hiyo rav 4 manual ila ni namba A. Hapo una ushauri gani boss
 
Mkuu kwanini? kwenye magari ya mashindano sijaona dereva anaendesha automatic.
Mara nyingi yale ni matoleo maalum nando maana ata modification zake ziko tofauti na gari za kawaida kwasababu ya matumizi yake.Lakini haimaanishi kwamba iko tuendako hakutakua na auto.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Tofauti ya ubora kivip wakati unaona automatic ni advanced technology ya gearbox.Kwahiyo automatic ni bora zaidi kwasababu ni techolojia iliyokua kutoka kwenye uduni na ndiko dunia iliko.Itafika miaka manual zitakua hazitengenezwi au zitatengenezwa kwa oda.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
sawa, automatic ni more advanced technology. Vp khs changamoto ya auto vs manual
kimatumiizi
 
Mkuu, kuna mtu anauza hiyo rav 4 manual ila ni namba A. Hapo una ushauri gani boss
Kama ni chini ya milioni nne chukua, hautajutia. RAV 4 hiyo kama ni manual Nina uhakika haijatembea kms nyingi. Ila kama bei ni zaidi ya milioni nne basi achana mayo nunua automatic nyinginezo kama Vitz, IST, na Toyota nyingine za CC ndogo
 
thanks boss, noted! Ila naomba ufafanue kidogo hapo kwenye cc, mimi ni mgeni kabisa.
 
Ajabu UK niliona gari nyingi sana manual.
Umetoka lini UK mkuu?? Now most of their Car ni Auto hata zile Land Rover zipo za kisasa zaidi, Manual UK ziko chache sana sio kwa uwingi huo unaousema hapa, i've been there miezi michache nyuma hapa. Nimeendesha sana AUDI, CHEVO, na hizo Land Rover zote nilikuta AUTO. itakuwa ulikwenda enzi ambapo Mjomba Magu anapiga MASTERS.
 
Adavantage za manual.
*Ni economy kwenye mafuta
*Ikiaribika inatengenezeka
*Watumiaji ni wachache so gari haiazimwi ovyo.
*service yake sio ya gharama sana
*Betri ikizingua unasukumwa chuma inawaka.
*Unaweza ukaendesha umbali mdogo ukiwa umemaliza gia zote ata kama ni mwendo wa taratibu au mkali

Automatic
*Raisi kuendesha
*Ni nzuri kwa mijini barabara zenye jam
*Rahisi kuuzika kama ukitaka kuiuza
 
Back
Top Bottom