1: Unahitaji kusikilizwa na kufanyiwa tathmini upya kama kweli tatizo ni migraine.
2: Kama ni migraine, huwa kuna dawa za kutibu na kuzuia.
3: Kama ni migraine, zaidi ya dawa kuna haja ya kuwa na mabadiliko ya kimaisha kwa ujumla ili kupunguza baadhi ya vitu vinavyoanzisha attack kama:
A: Mwanga mkali
B: Harufu kali/ pafyumu
C: Matumizi ya pombe
D: Stress
E: Matumizi ya mtindi, kahawa na chocolates
D: Vyakula vya kusindikwa/makopo na soda
F: Usikae na njaa muda mrefu
G: Kutokuvuruga ratiba yako ya usingizi na uwe wa kutosha (saa 8).
H: Kwa akina mama, asitumie mfumo wa homoni wa uzazi wa mpango.
I: Usiwe mtu wa kukasirika mara kwa mara.
J: Kutokujichosha sana/kupita kiasi.
K: Kunywa maji ya kutosha, kulingana na eneo ulilopo, uzito wa mwili na aina ya kazi.
L: kujiepusha na maeneo yenye sauti kali/kelele.