Naomba kujuzwa dawa ya maumivu ya mguu kwenye mfupa

Niache Nteseke

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2020
Posts
2,162
Reaction score
2,616
Heshima kwenu wadau.

Naomba kujuzwa dawa ya maumivu ya mfupa wa kwenye goti, tatizo lilitokana na ajali ya boda goti likavunjika hata kutembea ikawa shida kwa muda wa miezi 6+ ni kitandani tu.

Ikapatikana nafuu ya kuanza kutembea na mara kwa mara mfupa wa goti huwa unauma hasa kipindi cha baridi, lakini tangu jana kuna maumivu makali sana kwenye mfupa kiasi kwamba hata pain killer za kawaida zimeshindwa kutuliza maumivu hayo.

Naomba kujuzwa dawa gani ya maumivu makali itakayoweza kusaidia kupunguza hali hiyo ya maumivu ya mfupa kwenye goti wakuu.

Natanguliza shukran kwenu.
 
Pole sana hizi umemeza? Aceclofenac au Gofen....
Pia jaribu kupakaa fastum gel, usichue pakaa tu kama mafuta, pole sana
Hapana sijameza hizo mkuu. Hazina sulphur hizo, zikiwa na sulphur huwa inaleta shida mwilini.

Na pia vipi uponyaji wake hutuliza maumivu kwa haraka mkuu...?
 
Heshima kwenu wadau.

Naomba kujuzwa dawa ya maumivu ya mfupa wa kwenye goti, tatizo lilitokana na ajali ya boda goti likavunjika hata kutembea ikawa shida kwa muda wa miezi 6+ ni kitandani tu.

Ikapatikana nafuu ya kuanza kutembea na mara kwa mara mfupa wa goti huwa unauma hasa kipindi cha baridi, lakini tangu jana kuna maumivu makali sana kwenye mfupa kiasi kwamba hata pain killer za kawaida zimeshindwa kutuliza maumivu hayo.

Naomba kujuzwa dawa gani ya maumivu makali itakayoweza kusaidia kupunguza hali hiyo ya maumivu ya mfupa kwenye goti wakuu.

Natanguliza shukran kwenu.
Kiongozi
Natumia lugha isiyo rasmi kusema mi ni wajina wako kwenye Janga hilo

Dec 14 2023 nilipata ajali ya goti na kuvunjika mara mbili juu na chini (transverse patella fracture) Mungu mwema haikuwa (open fracture)

Nina mwezi sasa najitibu kiasili tangu nilipojitonesha tena baada ya matibabu ya hospitali na kikagawanyika tena kama awali

Aisee Goti sio mchezo, baada ya miezi miwili toka sasa nikipona sawasawa hakika nitakuwa nimejiridhisha Kuelekeza yeyote tiba hiyo ya asili
 
Nashkuru sana unajitibu mwenyewe au upo kwa mtaalamu wa mifupa mkuu...?
 
Kule kijijini kwetu kuna mzee anatibu kiienyeji yupo vizuri ,Nakumbuka mama yangu mdogo alikuja kijijini kipindi cha nyuma akapata ajali alikua amepakia pikipiki akaangushwa na bodaboda akavunjika mguu yule mzee alimtibu na ndani ya miez 3 akawa yupo vizur
 
Nipo kwa mtaalam wa mipupa wa dawa za asili

Hawa jamaa wanapishana sana na hospitali

Tangu nilivyojitegua tena sasa hivi nina mwezi na ninatembea zaidi ya km 2 na sina tatizo
Ni yule mzee wa Dodoma kiongozi au sio huyo...?
 
Kule kijijini kwetu kuna mzee anatibu kiienyeji yupo vizuri ,Nakumbuka mama yangu mdogo alikuja kijijini kipindi cha nyuma akapata ajali alikua amepakia pikipiki akaangushwa na bodaboda akavunjika mguu yule mzee alimtibu na ndani ya miez 3 akawa yupo vizur
Tiba yake inachukua muda gani kumtibu mgonjwa kiongozi...? Yaani mgonjwa anakaa hapo kwake kwa muda gani na yupo Mkoa gani pia...?
 
Ni yule mzee wa Dodoma kiongozi au sio huyo...?
Hapana sio wa dodoma, kuna Jamaa mmoja yupo Mbagala Chamanzi (alinitibu kwa Kutumia Mti wa Mtamba)
Kiukweli nimeshanaliza miezi mitatu na natembea Vizuri

Mafanikio
●naweza kutembea vizuri umbali mrefu bila ya shida
●maumivu hakuna Kabisa

Tatizo
●Fracture haijaunga
●siwezi kukimbia

Hivyo tu kiongozi
 
Safi sana na hongera pia ndugu yangu. Ili fracture iunge umeambiwa ufanye nini mkuu...?
 
Back
Top Bottom