Naomba kujuzwa gharama ya safari ya mbugani kwa njia ya Land Cruiser

Naomba kujuzwa gharama ya safari ya mbugani kwa njia ya Land Cruiser

Hivi kuna umbali wa muda gani kutoka Arusha hadi Ngorongoro Crater. Nafikiria kufanya hata day trip?
 
Shuka makuyuni au nyuma yake kidogo kuna campsite nyingi hapo utapata madereva wengi wa tours.. ila kuwa mjanja kwenye kupatana kwa maana pesa yako ni posho ya dereva..
Huku sio kwenda kutalii bali ni kuvizia kitalii
 
Hivi Tarangire na Ngorongoro wapi kuna wanyama wengi maana nimefika Ngoro2 ila Tarangire sijaenda.

Kutoka Arusha wapi ni karibu namaani shaweze kutoka Ar nikatalii na kugeuza kuepuka kulipa $500?
Ngorongoro kivutio kikuu ni crater na sio wanyama, pili ngorongoro sio mbuga ya wanyama wanaita reserved area.
Tarangire ni mbuga ya wanyama na ina wanyama wengi sana.
Inasifika kwa simba wanaopanda kwenye miti na makundi mengi ya tembo
 
Ngorongoro kivutio kikuu ni crater na sio wanyama, pili ngorongoro sio mbuga ya wanyama wanaita reserved area.
Tarangire ni mbuga ya wanyama na ina wanyama wengi sana.
Inasifika kwa simba wanaopanda kwenye miti na makundi mengi ya tembo
[emoji1756][emoji1756][emoji1756]
 
Kwa kupunguza gharama. Tumia usafiri wa kawaida mpaka .Mto wa mbu / karatu..hapo kuna madereva wengi wa tours.. utaunganishwa na wageni wengine..
Shukrani
 
Mkuu mimi sio mtoa huduma, nimekupa gharama ili angalau uwe na wastani wa makadirio, ukihitaji labda nikuunganishe na watoa huduma mbalimbali naweza kufanya hivyo ili upewe itinerary.
Vinginevyo naomba nisijibu mengi.
Naomba nisogezee mawasiliano/page ya instagram ya watoa huduma tafadhali
 
bei ya mzawa je ?
Nimeenda Tarangire hiyo ni bei ya kitalii.Kama unataka ya kibongobongo. Tafuta watu binafsi wenye cruiser patanisha nao. Laki 2 na nusu Hadi 5 ukienda kibosi. Kuingia kichwa haizidi 15000 Kwa MTU mzima , watoto mpaka 18 yrs free. Kule inategenea anaenda MTU WA namna gani sie tulikodi hiece watu 12 tukachanga 30000 na tukaona wanyama.
 
Vitu nilishindwaga hivi. Yaani nitoe Laki 5 kukuona tembo? Dah me kweli bado sana nipo nyuma.
Mimi napenda sana yani, mara moja moja inakua nzuri sana
 
Back
Top Bottom