Naomba kujuzwa gharama za msingi kwa nyumba ya ghorofa moja

I think unahitaji kusema zaidi unaijenga wapi maana gharama za Dar ni tofauti na mbeya, Moshi au Dodoma.
 
Natumia uzoefu wangu maana vipimo havionekani vizuri. Hapo roughly andaa 15M mpaka 17M kutegemea na mahali ulipo bei ya materials ikoje na utatumia njia ipi kujenga i.e mkandarasi (kampuni), fundi maiko au utanunua materials na kumtafuta mtaalam (engineers) akujengee.
Vipimo vingeonekana ningekusaidia vizuri zaidi mkuu.
 
Ni kweli chuma iko juu Sana, Ila 50M ni mbali Sana mkuu. Hiyo ramani yake hata sio kubwa kivile.
ushauri tu awe na hiyo kitu. kuna chuma zinasukwa chini (base) na kuzunguka msigi wote, kuna tofali zinazikwa kozi zaidi ya saba za kulaza, kuna mkanda unapigwa mzunguko wote, kuna zege chini kwenye base na huo mkanda, kuna kifusi cha kujaza, kuna framework za kufunga na mambo ya mafundi. Basically, ata cement. mchanga, na kokoto zote zimepanda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…