Naomba kujuzwa jinsi ya kuanzisha kampuni ya tours!

Naomba kujuzwa jinsi ya kuanzisha kampuni ya tours!

Beige

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2022
Posts
234
Reaction score
515
Habarini wana JF,

Naomba kujua jinsi ya kuanzisha kampuni ya tours. Nitakuwa tu na ofisi ila magari sina Nategemea kukodisha magari na kutia nembo ya hiyo kampuni tarajiwa. Ninaomba ABCD tafadhali kwa wenye idea. Natanguliza shukurani za dhati.
 
Kuanzisha kampuni ya tours ni muhimu kwanza ufahamu tourism vizuri au utatumia pesa nyingi na faida kidogo.

1. Umewahi kufanya kazi au una experience ya safaris, excursions hapa Tanzania & Zanzibar?

2. Kusajili kampuni ya tour na kupata wageni ni vitu viwili tofauti. Je ushawahi kupata wageni na uka arrange nao tours/excursion/safaris

Hapo ukijibu Vizuri nadhani tutaendelea

NB: utalii unapesa nyingi bahati ikija kwako
....
 
Huu ushauri ni poa saana,

na anatakiwa atambue sio rahisi kihivyo, angesoma kwa waliofanikiwa....mimi mara nyingi nawashauri

1. Tafutata mtu anayefanya hii biashara au mtafute mtu ambaye kaajiriwa hususani kwa makampuni makubwa awe mshauri wako,, hii itakusaidia

2. Kama huna mtaji usisajili kampuni wapo watu kibao wanamakampuni na magari hawana wateje tumia majina ya kampuni Zao kwa kukodisha anZa kufanya biashara

3,tafuta makundi yako ya wageni both inside and outside ukipata hata kundi moja la nje ndio fikiria kuusajili

wakati unasajili uwe na ufahamu ndio utatakiwa ulipe kodi na compliance kibao, kama huna mtaji...uhakika wa kupata wageni utajichosha saana

Tambua wapo ma giant kwa game , wana pesa connection wageni na kadhalika, wanao ubavu wa kublock room Zote Za hotel kipindi cha peak seasons hata kama unawageni wako hutopata pa kuwalaZa...ukiwa ni mtu amabaye unajua haya mambo ni rahisi kupambana na hiZi changamoto

Kikubwa nikutakie kila la kheri
chamuhimu jifunZe changamoto Za waliokutangulia jitahidi usiZirudie utasonga mbele

kila la kheri
waslaam
 
Back
Top Bottom