Naomba kujuzwa kama TSh milioni 10 inatosha kwenda kutembea Dubai

Naomba kujuzwa kama TSh milioni 10 inatosha kwenda kutembea Dubai

Loimata

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2022
Posts
749
Reaction score
1,741
Habari ya usiku wakuu,

Natamani kupata ka vaccation kidogo nipunguze machungu ya hii dunia.

Nimekua nikitamani kwenda Dubai na kwa mambo ninayopitia naona kama huu ndio wakati muafaka wa kwenda huko nikiamini nitafurahi kidogo na kusahau kidogo mateso ya dunia hii.

So wakuu hiyo pesa itatosha kwa watu wazima wawili na mtoto? Kama itatosha, je itatosha kwa muda gani?

Pia naomba miongozo ya mfano hotel nzuri za bei nafuu na vitu kama hivyo.

DOS and DONTs nk.

Mbarikiwe sana🙏
 
Hata sijasoma Uzi Hila nimependa title tu. Watz hatuna kasumba ya kutembea. Wengi tukipata pesa tunakimbilia kujenga au kuinvest. Tuna uoga na maisha.

Kwenye hata maisha Ili ujione umeishi angalau utembee hata nchi 20 uone mambo mapya ya maisha. Wazungu wanalijua Ili Leo hii wametembea Africa nzima. Sisi hata waafrica tunafikiria hatujui maisha ya kuspend.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Ukifika Dubai fikia Deira na sio kule unapoonaga kwenye TV. Kule Milioni 10 ni sawa na Tsh 10. Fikieni Deira kwenye Hotel za kawaida kama tsh 100k hadi 150k kwa siku. Kule kwenye majengo marefu mnakuwa mnaenda mida ya mchana kutembelea kisha mnarudi Deira kulala. Mkienda mitaa ya Burj Khalifa hela yenu itaisha kwa siku moja.
 
Hata sijasoma Uzi Hila nimependa title tu. Watz hatuna kasumba ya kutembea. Wengi tukipata pesa tunakimbilia kujenga au kuinvest. Tuna uoga na maisha.

Kwenye hata maisha Ili ujione umeishi angalau utembee hata nchi 20 uone mambo mapya ya maisha. Wazungu wanalijua Ili Leo hii wametembea Africa nzima. Sisi hata waafrica tunafikiria hatujui maisha ya kuspend.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
Kweli kabisa mkuu ila binafsi naona ni hekima uwe japo na kanyumba kazuri na ka usafiri kabla hujaanza kuspend kwenye ma vacation.
 
Okay.
Wiki moja naamini tutafurahi vya kutosha
Ukihitaji mlinzi binafsi wa kwenda naye huko Dubai, nipo hapa. Nichukue nafasi ya huyo mtu mzima mwingine. Nina uzoefu wa miaka mingi kwenye hii fani.
 
aongeze tano tena ya wewe au sio
Hapana! Nimemshauri amuondoe mtu mzima mmoja! Na hivyo kwenda yeye, mtoto mmoja, na mlinzi binafsi wa kumlinda wakati wote wa hiyo vacation.
 
Dah kiongoz hapo kwenye m10 fanya unikope kwanza m3 ili nibetie kwanza mkuu mkeka ukitiki nakupa 30 milion, ili ukakae hata wiki mbili, dah ila jaman wengine tunawaza tunapataje japo lak5 tuinuke kiuchumi chalii yangu yeye ana m10 ya kurefresh akili jaman maisha haya mungu kwann mimi sina hela hata ya chai kesho, na sina uhakika wa kula achilia mbali kulipa pango
 
Back
Top Bottom