Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 20,561
- 24,428
- Thread starter
-
- #21
Inavunwaje mpaka kuona hii ni kilo moja?Mkuu asante kwa maelezo, lakini napenda kujua msitu uwe na miaka mingapi toka kupanda? Je ni mti wowote? Kuna neema naiona
Mzee acha basi .daahViko vifaa vyake maalum vya kuvunia, vinauzwa China Alibaba
Haaa haaa haaa, mkuu unataka nikuagizie vifaa?Mzee acha basi .daah
Kuna Mwamba mmoja alinicheka na Alisema kama wewe. Nilivyompa idea akabaki anani blue 🔵🔵 tick. Pumbaaaavu yule mshenziMkuu,Carbon Trading au Biashara ya hewa ukaa inahusika zaidi na Kufanya kitu kinaichwa Carbon Offsetting.Inakuwa na masoko ya aina mbalimbali ambapo kampuni inayozalisha hewa ukaa pamoja hewa nyingine Chafuzi za mazingira inafanya Offsetting ya uchafuzi kwa kulipia uhifadhi wa mazingira.
Hili kufanya hivyo unaweza kuwa na miradi inayohamasisha matumizi ya Nishati endelevu,Usafishaji wa mazingira na uhifadhi wa mazingira kwa ujumla wake.Ili kuamua Bei ya hizi Carbon Credit inabidi uoneshe kwa takwimu za uhakika na kwa kiasi gani shughuli zako zinachangia katika uondoshaji wa hewa chafu uhifadhi wa mazingira n.k.Kipimo hicho kitatumika kuamua bei ya hizo Offset Credits ambazo sasa uaweza kuziuza katika masoko ya aina tofauti.Kwa sasa hivi hii ni fursa ingawa hata hivyo bado elimu inahtajika ili kueleweka zaidi.Hata hivyo kama unapenda kuingia katika eneo hili unaweza kkuwasiliana nami zaidiili tuweze kushirikishana zaidi kuhusu fursa hii ambayo nami ninaitazama kwa jicho la kibiashara.
Ushenzi wake ni nini?Kuna Mwamba mmoja alinicheka na Alisema kama wewe. Nilivyompa idea akabaki anani blue 🔵🔵 tick. Pumbaaaavu yule mshenzi
Miaka kumi iliyopita nilishiriki hili zoezi na watalaam toka SUA, tulizurula Njombe, Kilolo, Makete na Mufindi, kama ingefanikiwa ile kazi, labda Wakinga wengi wangekuwa kundi la Dangote. Kilichokuwa kinafanyika tukifika shambani ilikuwa ni kuchukua sample za miti kwenye shamba la mkulima, tunapima diameter, wanachukua umri wa mti na aina yake na urefu. Hizi data zilitumika kutafuta kiasi cha CO2 kilichovutwa na ule mmea toka angani. Hesabu zake zilikuwa balaa. Baada ya zoezi, taarifa zikaenda ofisi VP mazingira, ndo ikawa mwisho wa hadithi yetu pendwa.Msitu una kuwa na umri gani
Tafuta watu wa maliasili hasa walioko Mafinga, pale kuna taasisi zilizowahi kuvuna hewa ya ukaa kama GRLNaomba kujuzwa kwa anayefahamu biashara ya hewa ukaa atujuze hapa
Wanatumia kipimo gani kujua uzito wa hewa husika?Mara nyingi msitu wa kutoa hewa kilo moja kwa mwaka ni kama hekta 7 hivi, ni biashara nzuri ukiwa na hekta 70 kwa mwaka unaweza kupata hewa kilo 20 ambayo ni milioni 700 hiyo
Kwa Nini wasiweke wazi kwenye public Kila kitu kama uchawi ooh fika ofisini utaelekezwa rushwa rushwa rushwaNchi zenye viwanda ambavyo huchafua hewa hununua misitu katika nchi zisizochafua hewa,hivyo hiyo misitu hununuliwa kwa lengo la kupunguza hewa ukaa,miti ya hiyo misitu huhifadhiwa na kuendelezwa kupandwa.
Kiufupi wananunua haki ya kuchafua hewa kupitia uwepo wa misitu,hivyo kama una msitu wako umeuhifadhi na kuutunza fika nemc au wizara ya mazingira utapata utaratibu wa kufanya biashara hiyo ya hewa ukaa
Sasa serikali Kwa Nini hawatangazi hizo fursa?Mara nyingi msitu wa kutoa hewa kilo moja kwa mwaka ni kama hekta 7 hivi, ni biashara nzuri ukiwa na hekta 70 kwa mwaka unaweza kupata hewa kilo 20 ambayo ni milioni 700 hiyo
Japo Nimechelewa But kwa ufupi Sana Hii Ni Biashara Inayolenga Kuweka Mlinganyo Sahihi Kati ya Viumbe hai Vya Aina Mbili Ambavyo ni wanyama Na Mimea, Viumbe Hivi Vinategemeana Katika Kuishi Na Ukuaji Mimea ina Sifa Ya Kuvuta Hewa Ya Ukaa Na Pia Wanyama Wanavuta Hewa ya Oksijen Ambayo Inatoka Kwa Mimea. Kulingana Na Shughuli Za Kibinadamu Kuchangia Mabadiliko Makubwa Ya Tabia ya nchi Hivyo kumekuwa na Ongezeko Kubwa la Hewa za Ukaa, Ambalo Kimsingi Ikiongezeka Ina Madhara Mengi Kuliko Faida IlizonazoNaomba kujuzwa kwa anayefahamu biashara ya hewa ukaa atujuze hapa
Good.Be BlessedJapo Nimechelewa But kwa ufupi Sana Hii Ni Biashara Inayolenga Kuweka Mlinganyo Sahihi Kati ya Viumbe hai Vya Aina Mbili Ambavyo ni wanyama Na Mimea, Viumbe Hivi Vinategemeana Katika Kuishi Na Ukuaji Mimea ina Sifa Ya Kuvuta Hewa Ya Ukaa Na Pia Wanyama Wanavuta Hewa ya Oksijen Ambayo Inatoka Kwa Mimea. Kulingana Na Shughuli Za Kibinadamu Kuchangia Mabadiliko Makubwa Ya Tabia ya nchi Hivyo kumekuwa na Ongezeko Kubwa la Hewa za Ukaa, Ambalo Kimsingi Ikiongezeka Ina Madhara Mengi Kuliko Faida Ilizonazo
Kumbuka Hewa Ya Ukaa au CO2 Sio Hewa Mbaya ina faida Nyingi tu,,, Lkn Ikizidi Ina madhara pia yapo ambayo Yalishaonekana Na yanategemewa kuja Mengi Zaidi, So ili Kunusuru Hili Yapo Makampuni From Developed country Yameifanya hii Kuwa Biashara kwa Mfumo huu.
Ukiwa na Msitu Wa Kwako Wa Asili Utafuata hatua Ili uweze kusajiliwa na kulipwa Kwa Kila Mti Utakaokuwepo Shambani Kwako,,
Njia Ya Pili Ambayo Ndo Bora zaidi Ni Tafuta kampuni Inayosimamia Ununuaji Wa Hewa hiyo Ya Ukaa mfano Kwa Ukanda Wa Kusini Iringa zna Njombe Kuna Kmapuni Inaitwa (One Acre Fund) Upande Miti Kwenye Eneo Ambalo Halikuwa Na Miti Then Baada Ya Miaka Mitatu utaanza Kupokea Malipo Ya Miti Yako Yote iliyoko Shambani.