Msitu una kuwa na umri gani
Miaka kumi iliyopita nilishiriki hili zoezi na watalaam toka SUA, tulizurula Njombe, Kilolo, Makete na Mufindi, kama ingefanikiwa ile kazi, labda Wakinga wengi wangekuwa kundi la Dangote. Kilichokuwa kinafanyika tukifika shambani ilikuwa ni kuchukua sample za miti kwenye shamba la mkulima, tunapima diameter, wanachukua umri wa mti na aina yake na urefu. Hizi data zilitumika kutafuta kiasi cha CO2 kilichovutwa na ule mmea toka angani. Hesabu zake zilikuwa balaa. Baada ya zoezi, taarifa zikaenda ofisi VP mazingira, ndo ikawa mwisho wa hadithi yetu pendwa.
Mahitaji muhimu ili upimiwe na ulipwe hewa ya ukaa.
1. unatakiwa uanzishe shamba sehemu ambayo haikuwa na miti, jangwa au grassland ili tuone kweli hewa umevuta
2. Hakikisha shamba lina cordinates na lina hati kubwa, siyo za kimila ( tulikwamia hapa)
3. Documents zote za umiliki wa shamba ziwe zimenyooka, wazungu ambao ndio madalali hawataki mbambamba ( Rabo bank kwa sasa ndo naona wanatia team)
4. Kwa mtu binafsi, msitu wa kuotesha mwenyewe ndo wenye deal, vijiji vinatumia misitu ya kiasili zaidi.
5. Kama msitu wako unaharibu mazingira hupati hela.
Kwa wenye ujasiri, mtafuteni Mkuu wa mkoa wa Dsm, Bwana Chalamila, alipokuwa Kagera alizindua biashara hii kule.