Uwe na pesa tu kwa maana utatoa vingi kwanza ukienda huko kutoa barua ya uchumba lazima uje na pombe za kutosha debe 5 na vitu vya jumla vya kutosha sio sukari kg1 , sijui nini hapana maana hata wao wakioa wanajitoa sana, hata kama mwanamke sio bikra wewe utamkuta ni bikra maana unaenda kuoa kijijini.
Halafu siku unaenda kutoa posa ndio unakuja na pombe zingine debe 10 , ndio utaratibu, halafu mashuka yale yakimasai watakuambia ulete sasa sijajua wazee wapo wangapi, fimbo ya babu wa msichana, khanga za mama na mashangazi, na mama wadogo, pea moja sawa tu ila kwa heshima ni pea 2 kwa kila mmoja , halafu koti lababu , ugoro, kilo za nyama zakuchomwa hiyo siku na utagharamia zote hizo. Kingine blanketi ya babu na bibi, baba na mama, napesa taslim kama huna ng'ombe wakutoa ila lazima dume achinjwe jiandae kama watakubali , kukukaribisha kwenye boma kuna tambiko litafanywa utavaa kimasai .
Hili jingine utapewa baada ya ndoa ikikamilika utakabidhiwa ng'ombe na mbuzi zakutosha kama wana mashamba utapewa kidogo. Halafu ndio Mkaanze maisha yenu. Ila hawapendi mkienda mbali.
Mahari kwa hizo ng'ombe ni ifuatavyo kama anabikra ng'ombe ni 80 ila kwa sasa ni 50 jua hilo, ambaye amezaa ukaamua kumuoa watano tu. Kwa ambaye hana mtoto na anaelimu na hana bikra ni ng'ombe 15 .
Haya kazi kwako sasa