Naomba kujuzwa namna ya kutengeneza mbege

Kwa ufahamu wangu na uzoefu mdogo.
Cha kwanza Sio kila aina ya ndizi inafaa kutengeneza mbege.
Ukisha kuwa na ndizi husika , zikiwa tayari mbivu, zikishaondolewa maganda hupikwa kwwa mfumo wa kuchemsha.

Mahali pengine kabla ya kupikwa huachwa kwanza kwa siku moja zi chachuke ndio hupikwa.

Zikisha pikwa huepuliwa na kuwekwwa ama kwenye ndoo, pipa , au chungu.

Huachwa zikae kuanzia siku 3 mpaka saba, inategemea eneo hali ya hewa yake ni ya namna gani.

Baada ya kukaa kwa siku hizi zinazo faa, zenyewe huwa zinanisha kuona zinafaa sasa kuandaliwa.

Kwwa juu hutoa povu na zinakuwa zinafoka kama zipo kwenye moto.

Kinacho fuata ni kuchanganya na maji kiasi kinachotakiawa, hapa kwenye kuchanganya na maji pana ufundi wake maana hapo ndio pataamua mbege yako iwe ya namna gani.

Kama si kwaajili ya biashara inaweza kuchanga na maji kwa mfumo wa 40% maji na 60% ndizi.

Zinatakiwa kukorogwa kwa muda na mrefu, unaziacha kwenye utulivu si chini ya saa sita, kisha unazichuja, kwa mfumo wa kukamua.

Baada ya hapo unandaa unga wa ulezi, ambao huo ulezi unakuwa umelowekwa na maji au unyenyevu mpaka unaota, ukisha ota unaanikwa na kukauka , ukisha kauka unasagwa na kuwa unga.
Huu mchakato wa maandalizi ya ulezi unankuwa siku kadhaa nyuma kabla ya maandalizi ya ndizi.

Baada ya kuwa na unga unaupika kama uji na unapika usiwe mzito kabisa na wala usiwe mwepesi, ukoroge usiwe na mabunda, ukisha iva sawa na uji wa kawaida unaucha upoe.

Ukisha poa unachikua unaweka kwenye yale maji uliochuja au kukamua kwwenye ndizi.

Kiasi cha uji wa ulezi unachotakiwa kuweka kwenye mbege yako ni kiwe 10-15 cha mbege ulioandaa.

Baada ya kuchanganya koroga vizuri na kwa muda kidogo kisha acha kwa saa sita hadi 12 mbege inakuwa tayari.
 
Huo ulezi unasagwa kwenye hizi mashine au? Maana yale “machicha”hayajakaa kama kitu kilichosangwa kisasa.
 
Ndio unasagwa kwenye mashine za kawaida ila kwenye ulezi mashine hubadilishwa chekecheo .
La unga wa kawaida na unga wa uji ni tofauti na unga wa ulezi wa kutengeneza mbege.
 
Back
Top Bottom