Naomba kujuzwa namna ya kutuma simu kutoka Dar es Salaam kwenda mkoani

Naomba kujuzwa namna ya kutuma simu kutoka Dar es Salaam kwenda mkoani

MZEE MSASAMBEGU

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2013
Posts
2,776
Reaction score
2,556
Wakuu habari zenu,

Kuna simu nataka nimtumie mtu kutoka Dar kwenda mkoani...naomba kwa mwenye uzoefu wa mtu ambaye amewahi kutuma simu kwa mtu aliyopo mkoani anipe uzoefu kwenye mambo yafuatayo:

1. Njia ipi ya haraka na ya usalama ya kutuma huo mzigo
2. Gharama zake huwa zikoje
 
Alooo nilitumaga simu Dar to Mwanza ikapotelea mikononi mwa konda, japo niliwasumbua mpk wakanilipa...

Njia ambayo kdg naona ni nzuri...
Tumia haya haya mabasi ila simu usikubali uikabidhi leo jioni eti ndio kesho iondoke, vitu ving vinapotea usiku, maana wanaolala ofisini wengi sio wahusika wakuu.
Wewe nenda asubuhi na mapema ubungo, gari inaondoka ndio unakabidh simu..

Usiwe mbahili, lipia gharama za usafiri wakupe na receipt kbsa, waifunge kwenye package, waandike sehemu itakapo pokelewa, jina la mpokeaji, namba yake, yako kwa nyuma na TAREHE.

Jitahidi aliyeipokea ndio huyo huyo atakayeisafirisha na kumkabidh mlengwa(mimi hapa ndio nilibugi, ilipitia mikononi kwa wengi).

Pata jina lake na liandikwe kwenye receipt, hakikisha ni mfanyakazi halali ya kampuni husika ya gari, chukua namba zake, na za ofisi, pia km unampa konda hakikisha na dereva anajua, japo nakushauri sana mkabidh dereva, mpokeaji naye aache wenge, awe anapatikana kwenye simu, asubiri gari sio gari imsubiri, akiacha gari ikipita simu ikaenda kulala....anaongeza risk.

KUBWA KULIKO YOTE.
hakikisha receipt ya simu, receipt ya usafirishaji UNABAKI NAVYO visiende na gari, na imei umeirecord somewhere,
Piga picha mtumie mpokeaji,

Ukichukulia poa hayo maandishi makubwa hapo juu, likitokea la kutokea, kwisha habari yako
 
Tumia basis
ungeandika inakwenda mkoa Gani,Pengine ungeunganishwa na madereva waendao huko.
 
Epuka kumshikish konda au dereva simu mkononi. Fika ofisi ya basi husika lipia package na chukua risiti halali.

N vizuri hyo simu ukaifunga ndani ya box la simu alafau uizungushe seal tape na juu utaandika jina na namba ya mpokeaji.

Kila la kheri


Sent using Jamii Forums mobile app
 
reyzzap,
Ahsante sana kwa kunipa uzoefu wako...so inatakiwa nikalipe moja kwa moja kwenye ofisi za bus husika..vipi na gharama zao zina range sh ngapi???
 
Ahsante sana kwa kunipa uzoefu wako...so inatakiwa nikalipe moja kwa moja kwenye ofisi za bus husika..vipi na gharama zao zina range sh ngapi???
NDIOO...hili lifanyike ofisini, hakikisha ni kampuni ya kueleweka yenye ofisi kbsa sio wale wa kudandia.
Unatoa simu wanakukatia receipt yao, inayoonesha gharama ya simu, aina ya simu
Km ina receipt, unapiga picha vyote pale, simu yenyewe, reseat ya simu, receipt ya usafirishaji na mwisho hakikisha imei namba unayo, either kwa picha au umeandika sehemu...

NARUDIA KUKUAMBIA.
Hakikkisha receipt zote mbili unabaki nazo na imei namba unaijua.
Yaani ukibugi hapa, likitokea la kutokea wewe huna chako wala huna haki.....
Maana huna ushahidi wowote zaidi ya essay.

Andaa angalau elf 10.
 
Ok...ahsante sana kwa mchango wako,and naenda kuituma kwenye ofisi ya bus or naongea tu na dereva moja kwa moja

Office kwa usalama zaidi.

Japo mimi natumaga kwa dereva/kodakta sometimes na ni kwa vile nawajua.

vinginevyo peleka mzigo ofisini
 
Wakuu habari zenu,kuna simu nataka nimtumie mtu kutoka dar kwenda mkoani...naomba kwa mwenye uzoefu wa mtu ambaye amewahi kutuma simu kwa mtu aliyopo mkoani anipe uzoefu kwenye mambo yafuatayo

1.Njia ipi ya haraka na ya usalama ya kutuma huo mzigo
2.Gharama zake huwa zikoje
Mimi huwa natuma kupitia Precision Airways toka Dsm kwenda KIA
 
Back
Top Bottom